2 Samweli 10 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 10:1-19

Daudi Awashinda Waamoni

(1 Nyakati 19:1-19)

110:1 1Sam 11:1; 2Sam 17:27; 1Nya 19:1Baada ya muda, mfalme wa Waamoni akafa, naye Hanuni mwanawe akaingia mahali pake. 210:2 1Sam 11:1Daudi akawaza, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kama vile baba yake alivyonitendea mimi wema.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe kuonyesha wema wake kwa Hanuni kuhusu baba yake.

Watu wa Daudi walipofika katika nchi ya Waamoni, 310:3 Hes 21:32wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “unadhani Daudi anamheshimu baba yako kwa kukutumia watu ili kuonyesha masikitiko? Je, Daudi hakuwatuma watu hawa kuchunguza na kuupeleleza mji ili kuupindua?” 410:4 Law 19:27; Isa 7:20; 15:2; 50:6; 52:14; Yer 48:37; Eze 5:1; Isa 20:4; 3:17; Yer 13:22; Eze 16:37; Mik 1:11; Nah 3:5Basi Hanuni akawakamata watu wa Daudi, akawanyoa kila mmoja ndevu zake nusu, akakata mavazi yao nyuma katikati kwenye matako, akawaacha waende zao.

5Daudi alipoambiwa jambo hili, akatuma wajumbe ili kwenda kuwalaki, kwa maana walikuwa wamevunjiwa heshima sana. Mfalme akasema, “Kaeni huko Yeriko mpaka ndevu zenu ziote ndipo mje.”

610:6 Mwa 34:30; 2Sam 8; 5; Hes 13:21; 1Sam 14:47; Kum 3:14; Amu 11:3-5; 18:28; Kut 5:21; 1Sam 13:4Waamoni walipotambua kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wakaajiri askari wa miguu 20,000 Waaramu kutoka Beth-Rehobu na Soba, pia mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na vilevile watu 12,000 kutoka Tobu.

710:7 2Sam 2:18; 23:8Daudi aliposikia jambo hili, akamtuma Yoabu na jeshi lote la wapiganaji. 8Waamoni wakatoka wakajipanga wakiwa tayari kwa vita langoni la mji wao, wakati Waaramu wa Soba, wa Rehobu, watu wa Tobu na Maaka walikuwa peke yao kwenye eneo la wazi.

9Yoabu akaona kuwa mbele yake na nyuma yake kumepangwa vita; kwa hiyo akachagua baadhi ya vikosi vilivyo bora sana katika Israeli akavipanga dhidi ya Waaramu. 1010:10 1Sam 26:6Akawaweka waliobaki chini ya uongozi wa Abishai nduguye na kuwapanga dhidi ya Waamoni. 11Yoabu akasema, “Kama Waaramu watanizidi nguvu, basi itawabidi mje kunisaidia. Lakini kama Waamoni watawazidi nguvu, basi nitakuja kuwasaidia. 1210:12 Kum 1:21; 31:6; Efe 6:10; Amu 10:15; Neh 4:14; 1Kor 16:3; 1Sam 3:18; 2Nya 19:11; 1Sam 4:9; 2Sam 15:26; 22:31-32; Za 20:7; 37:4-5; Mit 29:25Uwe hodari na tupigane kwa ujasiri kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu. Bwana atafanya lile lililo jema machoni pake.”

13Basi Yoabu na vikosi vyake wakasonga mbele kupigana na Waaramu, nao Waaramu wakakimbia mbele yake. 1410:14 2Sam 8:12Waamoni walipoona Waaramu wanakimbia, nao wakakimbia mbele ya Abishai na kuingia ndani ya mji. Basi Yoabu akarudi kutoka kupigana na Waamoni na kufika Yerusalemu.

15Baada ya Waaramu kuona wameshindwa na Israeli, wakajikusanya tena. 16Hadadezeri akaagiza Waaramu walioletwa kutoka ngʼambo ya Mto Frati, wakaenda Helamu pamoja na Shobaki jemadari wa jeshi la Hadadezeri akiwaongoza.

17Daudi alipoambiwa haya, akawakusanya Israeli wote, wakavuka Mto Yordani, wakaenda Helamu. Waaramu wakapanga vikosi vyao vya askari kukabiliana na kupigana dhidi ya Daudi. 18Lakini Waaramu wakakimbia mbele ya Israeli, naye Daudi akawaua waendesha magari mia saba na askari wao wa miguu 40,000. Vilevile alimpiga Shobaki jemadari wa jeshi lao, naye akafa huko. 1910:19 2Sam 8:6; 1Fal 11:25; 22:31; 2Fal 5:1; Mwa 14:4Wafalme wote waliokuwa wanamtumikia Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, wakafanya amani na Waisraeli na wakawa chini yao.

Hivyo Waaramu wakaogopa kuwasaidia Waamoni tena.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒母耳記下 10:1-19

以色列人戰勝亞捫人

1後來,亞捫王死了,他兒子哈嫩繼位。 2大衛說:「我要恩待拿轄的兒子哈嫩,就像他父親曾經恩待我一樣。」他便派臣僕去安慰喪父的哈嫩大衛的臣僕來到亞捫境內, 3亞捫的官長卻對哈嫩說:「大衛派人來安慰你,你以為他是來弔唁你父親嗎?他派臣僕來見你,不過是要探聽虛實,想摧毀這城。」 4哈嫩便把大衛的臣僕抓起來,剃去他們一半鬍鬚,從臀部割去他們下半身的衣服,然後放走他們。 5消息傳到大衛那裡,他就派人去迎接他們,因為他們倍受羞辱。王告訴他們留在耶利哥,等鬍鬚長好了再回來。

6亞捫人知道得罪了大衛,便派人到伯·利合瑣巴招募了兩萬名亞蘭步兵、瑪迦王的一千人和一萬二千名陀伯人。 7大衛聽見消息後,就派約押率領全體勇士出戰。 8亞捫人在城門前列陣,瑣巴利合亞蘭人、陀伯人以及瑪迦人在郊野列陣。 9約押見自己腹背受敵,就從以色列軍中挑選一些精兵列陣迎戰亞蘭人, 10把餘下的軍兵交給他的兄弟亞比篩帶領,列陣迎戰亞捫人。

11他對亞比篩說:「倘若我勝不過亞蘭人,你便過來支援我;倘若你勝不過亞捫人,我便過去支援你。 12你要剛強,我們要為我們的人民和我們上帝的城邑奮勇作戰。願耶和華成全祂自己的旨意!」

13於是,約押率領軍兵進攻亞蘭人,亞蘭人敗逃。 14亞捫人見亞蘭人敗逃,便也從亞比篩面前逃回城去。約押就離開亞捫人,回師耶路撒冷

15亞蘭人見自己敗給以色列人,便再次聚集起來。 16哈大底謝派人把幼發拉底河那邊的亞蘭人調到希蘭來,由他的將軍朔法率領。 17大衛聽到消息後,就召集以色列全軍,渡過約旦河,來到希蘭亞蘭人列陣迎戰大衛18結果又在以色列人面前敗逃。大衛殺了七百名戰車兵、四萬騎兵,還殺了他們的將軍朔法19哈大底謝屬下的諸王見自己敗給以色列人,便向以色列人求和,臣服於他們。從此,亞蘭人不敢再支援亞捫人了。