2 Nyakati 6 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

2 Nyakati 6:1-42

Kuweka Hekalu Wakfu

(1 Wafalme 8:12-21)

16:1 1Fal 8:12; Kut 19:9; Law 16:2; Ebr 12:18; Kut 20:21; 24:15-18; Za 18:8-11Ndipo Solomoni akasema, “Bwana alisema kwamba ataishi katika giza nene. 26:2 Ezr 7:15; Za 135:21Nimejenga Hekalu zuri kwa ajili yako, mahali pako pa kukaa milele.”

3Kusanyiko lote la Israeli lilipokuwa limesimama hapo, mfalme akageuka na kuwabariki. 4Kisha akasema:

“Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mikono yake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema, 5‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, wala sikumchagua mtu yeyote kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli. 66:6 Za 78:68-70; Kum 12:5; Kut 20:24; 2Nya 12:13; 1Nya 28:4; 1Sam 16:1; Za 89:19-20Lakini sasa nimeuchagua Yerusalemu ili Jina langu lipate kuwamo humo, na nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

76:7 2Sam 7:2; 1Nya 28:2; Mdo 7:46; 1Fal 7:3“Ilikuwa moyoni mwa Daudi baba yangu kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 86:8 1Fal 8:18-21; 2Kor 8:12Lakini Bwana akamwambia Daudi baba yangu, ‘Kwa sababu ilikuwa moyoni mwako kujenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu, ulifanya vyema kuwa na jambo hili moyoni mwako. 9Hata hivyo, sio wewe utakayenijengea Hekalu, bali mwanao, ambaye ni nyama yako na damu yako mwenyewe, yeye ndiye atakayejenga Hekalu kwa ajili ya Jina langu.’

10Bwana ametimiza ahadi aliyoiweka: Nimeingia mahali pa Daudi baba yangu na sasa ninakikalia kiti cha ufalme cha Israeli, kama vile Bwana alivyoahidi, nami nimejenga Hekalu kwa ajili ya Jina la Bwana, Mungu wa Israeli. 116:11 Kut 40:20; 10:2; Za 50:5; 1Fal 8:9-21; 2Nya 5:10Nimeliweka humo Sanduku la Agano, ambamo ndani yake kuna lile Agano la Bwana alilofanya na watu wa Israeli.”

Maombi Ya Solomoni Ya Kuweka Wakfu

(1 Wafalme 8:22-53)

126:12 1Fal 8:22; Ebr 9:5; 1Tim 2:8Kisha Solomoni akasimama mbele ya madhabahu ya Bwana machoni pa kusanyiko lote la Israeli, naye akakunjua mikono yake. 136:13 Neh 8:4; Za 95:6Basi Solomoni alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, urefu wake dhiraa tano, na upana wake dhiraa tano na kimo chake dhiraa tatu, naye akaliweka katikati ya ukumbi wa nje. Akapanda juu ya hilo jukwaa kisha akapiga magoti mbele ya kusanyiko lote la Israeli, akanyoosha mikono yake kwelekea mbinguni. 146:14 Kut 15:11; 8:10; Mwa 5:24; Kum 7:9; Dan 9:4; 2Sam 7:22; Za 86:8Akasema:

“Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni wala chini duniani, wewe unayetunza Agano lako la upendo na watumishi wanaodumu katika njia yako kwa moyo wote. 156:15 1Nya 22:9-10Umetimiza ahadi yako kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, kwa kinywa chako uliahidi na kwa mkono wako umetimiza, kama ilivyo leo.

166:16 1Fal 2:4; 2Nya 7:18; Za 132:12; 2Sam 7:12-16; 1Fal 6:12“Sasa Bwana, Mungu wa Israeli, mtimizie mtumishi wako Daudi baba yangu ahadi zako ulizomwahidi uliposema, ‘Kamwe hutakosa kuwa na mtu atakayeketi mbele zangu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli, kama wanao wakiangalia yote wayafanyayo kuenenda mbele zangu kama vile ulivyofanya.’ 17Sasa, Ee Bwana, Mungu wa Israeli, acha neno lako lile ulilomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu litimie.

186:18 Ufu 21:3; Isa 40:22; Mdo 7:49; Za 113:5-6; 2Nya 2:6“Lakini kweli, je, Mungu atafanya makao duniani na wanadamu? Mbingu, hata mbingu zilizo juu sana, haziwezi kukutosha wewe. Sembuse Hekalu hili nililojenga! 19Hata hivyo sikiliza dua ya mtumishi wako na maombi yake kwa huruma, Ee Bwana Mungu wangu. Sikia kilio na dua ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako siku hii ya leo. 206:20 Dan 6:10; Kut 3:16; Kum 12:11; 2Nya 7:14; 30:20; Za 33:18; 34:15Macho yako na yafumbuke kuelekea Hekalu hili usiku na mchana, mahali hapa ambapo ulisema, ‘Jina langu litakuwako humo,’ ili kwamba upate kusikia maombi ambayo mtumishi wako ataomba kuelekea mahali hapa. 216:21 Isa 43:25; 55:7; Mik 7:18; Isa 44:22Usikie maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli wakati wanapoomba kuelekea mahali hapa. Sikia kutoka mbinguni, mahali pa makao yako na usikiapo, samehe.

226:22 Kut 22:11“Mtu anapomkosea jirani yake na akatakiwa kuapa, akija na kuapa mbele ya madhabahu yako ndani ya Hekalu hili, 236:23 Isa 3:11; Rum 2:8; Mt 16:27basi, sikia kutoka mbinguni na ukatende. Hukumu kati ya watumishi wako, ukimwadhibu yule mwenye hatia kwa kuleta juu ya kichwa chake yale aliyoyatenda. Umtangazie mwenye haki kwamba hana hatia, hivyo ukathibitishe kuwa haki kwake.

246:24 Law 26:17; Kum 32:15; Amu 2:11-15; Za 51:4“Wakati watu wako Israeli watakapokuwa wameshindwa na adui kwa sababu ya dhambi walizofanya dhidi yako, watakapokugeukia na kulikiri jina lako, wakiomba na kufanya dua kwako katika Hekalu hili, 25basi usikie kutoka mbinguni, ukasamehe dhambi ya watu wako Israeli na kuwarudisha katika nchi uliyowapa baba zao.

266:26 2Sam 1:21; Lk 4:25; 1Fal 17:1; Law 26:10“Wakati mbingu zitakapokuwa zimefungwa kusiwe na mvua kwa sababu watu wako wametenda dhambi dhidi yako, watakapoomba kuelekea mahali hapa na kulikiri jina lako nao wakageuka kutoka dhambi zao kwa sababu umewaadhibu, 276:27 2Nya 7:14; Yn 6:45; Zek 10:1; 1Fal 8:35, 36; Za 94:12basi usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi ya watumishi wako, watu wako Israeli. Wafundishe njia sahihi ya kuishi na ukanyeshe mvua juu ya nchi uliyowapa watu wako kuwa urithi.

286:28 2Nya 20:9“Wakati njaa au tauni vikija juu ya nchi, au koga au kawa, nzige au panzi, au wakati adui atakapowazingira katika mji wao wowote, maafa ya namna yoyote au ugonjwa wowote unaoweza kuwajia, 29wakati dua au maombi yatakapofanywa na mmojawapo wa watu wako Israeli, kila mmoja akitambua taabu zake na uchungu wake, naye akainyoosha mikono yake kuelekea Hekalu hili, 306:30 1Sam 2:3; 1Nya 28:9; Za 11:4basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote), 316:31 Kum 6:13; Za 34:7-9ili wakuogope kwa wakati wote watakaoishi katika nchi uliyowapa baba zetu.

326:32 2Nya 9:6; Kum 4:6-8; Yn 12:20; Mdo 8:27; Kut 3:19-20; Kum 4:6-8; Za 113:3; Isa 56:3-8; Yn 10:16“Kwa habari ya mgeni ambaye si miongoni mwa watu wako Israeli, lakini amekuja kutoka nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako kuu na mkono wako wenye nguvu ulionyooshwa, atakapokuja kuomba kuelekea Hekalu hili, 336:33 Kut 12:43; 2Nya 7:14basi na usikie kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, ukafanye lolote ambalo mgeni huyo anakuomba, ili mataifa yote ya dunia wapate kujua jina lako na wakuogope kama wafanyavyo watu wako Israeli nao wapate pia kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa Jina lako.

346:34 Kum 28:7; 1Nya 5:20“Wakati watu wako watakapokwenda vitani dhidi ya adui zao, popote utakapowapeleka, wakati watakapoomba kwa Bwana kuelekea mji ambao umeuchagua, na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, 35basi usikie dua na maombi yao kutoka mbinguni, ukawatetee haki yao.

366:36 1Fal 8:46; Law 26:44; Rum 3:9; Ay 15:14-16; Mit 20:9; Mhu 7:20; Yak 3:2“Watakapotenda dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna mtu yeyote ambaye hatendi dhambi, nawe ukachukizwa nao na kuwakabidhi kwa adui, ambaye atawachukua utumwani katika nchi iliyo mbali au karibu 376:37 1Fal 8:48; Isa 58:3; Yer 24:6-7na kama watabadilika mioyo yao katika nchi wanakoshikiliwa mateka, nao wakatubu na kukulilia katika nchi ya utumwa na kusema, ‘Tumetenda dhambi, tumefanya makosa na tumetenda uovu’; 386:38 Yer 29:12-13kama wakikugeukia kwa moyo wao wote na nafsi zao katika nchi ya adui zao ambao waliwachukua mateka, wakakuomba kuelekea nchi uliyowapa baba zao, kuelekea mji uliouchagua na Hekalu nililolijenga kwa ajili ya Jina lako, 39basi kutoka mbinguni, mahali pa makao yako, usikie dua yao na maombi yao na kuitetea haki yao. Uwasamehe watu wako, waliotenda dhambi dhidi yako.

406:40 Za 130:2; Isa 37:17“Sasa, Mungu wangu, macho yako na yafumbuke na masikio yako yasikie maombi yaombwayo mahali hapa.

416:41 Isa 33:10; Neh 9:25; Isa 51:10; Za 132:16; 1Nya 28:2“Sasa inuka, Ee Bwana Mungu,

na uje mahali pako pa kupumzikia,

wewe na Sanduku la nguvu zako.

Makuhani wako, Ee Bwana Mungu,

na wavikwe wokovu,

watakatifu wako na wafurahi

katika wema wako.

426:42 Za 89:24-28; Isa 55:3Ee Bwana Mungu, usimkatae

mpakwa mafuta wako.

Kumbuka upendo mkuu uliomwahidia

Daudi mtumishi wako.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

歷代志下 6:1-42

1那時,所羅門說:

「耶和華啊,

你曾說你要住在密雲中,

2現在我為你建造了雄偉的殿宇,

作你永遠的居所。」

所羅門為民眾祝福

3然後,王轉身為站立在那裡的以色列全體會眾祝福。 4他說:「以色列的上帝耶和華當受稱頌!祂親口給我父大衛的應許,現在祂親手成就了! 5祂曾說,『自從我帶我的子民出埃及以來,我並沒有在以色列各支派中選出一座城來建造殿宇,作為我名所在之地,也沒有選立一人做我以色列子民的君王。 6但如今,我揀選了耶路撒冷作為我名所在之地,又揀選了大衛來治理我的以色列子民。』」

7所羅門又說:「我父大衛曾想為以色列的上帝耶和華的名建一座殿, 8但耶和華對我父大衛說,『你想為我的名建造殿宇,這番心意是好的, 9但你不可建,要由你的親生兒子為我的名建殿。』 10現在耶和華已經成就祂的應許。我繼承了我父大衛的王位統治以色列,又為以色列的上帝耶和華的名建了殿。 11我把約櫃安放在裡面,約櫃裡有耶和華與以色列人所立的約。」

所羅門的禱告

12所羅門當著以色列會眾的面,站在耶和華的壇前,向天伸出雙手。 13他曾造一個長兩米二,寬兩米二,高一米半的銅臺,放在院子中間。他站在臺上,當著以色列會眾的面雙膝跪下,向天伸出雙手, 14禱告說:「以色列的上帝耶和華啊,天上地下沒有神明可以與你相比!你向盡心遵行你旨意的僕人守約、施慈愛。 15你持守對你僕人——我父大衛的應許,你曾親口應許,你今天親手成就了。 16以色列的上帝耶和華啊,你曾對你僕人——我父大衛說,『若你的子孫像你一樣謹慎行事,遵行我的律法,你的王朝就不會中斷。』求你信守這應許。 17以色列的上帝耶和華啊,求你實現你對你僕人大衛的應許。

18「然而,上帝啊,你真會住在人間嗎?看啊,至高的諸天尚且容不下你,更何況我建造的這殿呢? 19可是,我的上帝耶和華啊,求你垂顧你僕人的禱告和祈求,垂聽你僕人在你面前的呼求和禱告。 20願你晝夜看顧這殿,就是你應許立你名的地方!你僕人向著這地方禱告的時候,求你垂聽。 21你僕人和你的以色列子民向這地方祈禱的時候,求你從你天上的居所垂聽,赦免我們的罪。

22「如果有人得罪鄰舍,被叫到這殿中,在你的壇前起誓, 23求你從天上垂聽,在你眾僕人當中施行審判,按他們的行為罰惡賞善。

24「當你的以色列子民因得罪你而敗在敵人手中時,如果他們回心轉意歸向你,承認你的名,在這殿裡向你祈禱, 25求你從天上垂聽,赦免他們的罪,帶領他們回到你賜給他們和他們祖先的土地上。

26「當你的子民得罪你,你懲罰他們,讓天不降雨時,如果他們向著這地方禱告,承認你的名,並離開罪惡, 27求你在天上垂聽,赦免你僕人以色列子民的罪,教導他們走正道,降下甘霖滋潤你賜給你子民作產業的土地。

28「如果國中有饑荒、瘟疫、旱災、黴病、蝗災、蟲災,或是城邑被敵人圍困,無論遭遇什麼災禍疾病, 29只要你的以色列子民,或個人或全體,自知心中痛苦並向著這殿伸手禱告,無論祈求什麼, 30求你從天上的居所垂聽,赦免他們。唯獨你能洞察人心,你必按各人的行為施行賞罰, 31使你的子民在你賜給我們祖先的土地上終生敬畏你,遵行你的道。

32「如果遠方有不屬於你以色列子民的外族人聽說你的大能大力,慕名而來,向著這殿禱告, 33求你從天上的居所垂聽,應允他們的祈求,好叫天下萬民都像你的以色列子民一樣認識你的名、敬畏你,並知道我建造的這殿屬於你的名下。

34「你的子民奉你的命令上陣與敵人作戰,無論他們在哪裡,如果他們向著你選擇的這城和我為你名建造的這殿禱告, 35求你從天上垂聽他們的祈禱,為他們伸張正義。

36「世上沒有不犯罪的人,如果你的子民得罪你,以致你向他們發怒,讓敵人把他們擄走,不論遠近, 37若他們在被擄之地回心轉意,向你懇求,承認自己犯罪作惡了; 38若他們全心全意地歸向你,在被擄之地朝著你賜給他們祖先的這片土地、你選擇的這城和我為你建的這殿向你禱告, 39求你從天上的居所垂聽他們的祈禱,為他們伸張正義,赦免得罪你的子民。

40「我的上帝啊,

求你睜眼看、側耳聽在這殿裡獻上的禱告。

41耶和華上帝啊,

求你起來和你大能的約櫃一同進入你的安息之所!

耶和華上帝啊,

願你的祭司披上救恩,

願你忠心的子民蒙福歡樂!

42耶和華上帝啊,

求你不要棄絕你所膏立的人,

顧念你曾應許以慈愛待你的僕人大衛。」