1 Wafalme 7 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Wafalme 7:1-51

Solomoni Ajenga Jumba Lake La Kifalme

17:1 Ezr 4:7; Neh 2:1; 1Nya 6:14Ilimchukua Solomoni miaka kumi na mitatu kukamilisha ujenzi wa Jumba lake la kifalme. 27:2 1Fal 2:35; Neh 11:11Alijenga Jumba la Kifalme la Msitu wa Lebanoni, urefu wake ulikuwa dhiraa 100,7:2 Dhiraa 100 ni sawa na mita 45. upana wake dhiraa hamsini na kimo chake dhiraa thelathini,7:2 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13.5. likiwa na safu nne za nguzo za mierezi zikishikilia boriti za mierezi zilizorembwa. 3Ilipauliwa kwa mierezi juu ya boriti zile zilizolala juu ya nguzo arobaini na tano, kumi na tano kwa kila safu. 4Madirisha yake yaliwekwa juu kwa safu tatu, yakielekeana. 5Milango yote ilikuwa na miimo ya mstatili, ilikuwa upande wa mbele katika safu tatu, ikielekeana.

67:6 Neh 12:36; Ezr 5:5; Isa 41:20; Mwa 32:28; Neh 1:10-11Akajenga ukumbi wa nguzo, ambao urefu wake ulikuwa dhiraa hamsini7:6 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22.5. na upana wake dhiraa thelathini. Mbele ya jengo hilo kulikuwepo baraza. Mbele ya baraza kulikuwepo na nguzo na paa lililoningʼinia.

77:7 Ezr 8:1; 2:43Akajenga ukumbi wa kiti cha enzi, Ukumbi wa Hukumu, mahali ambapo angelitolea hukumu, akaufunika kwa mierezi kutoka sakafuni hadi darini. 8Kwenye jumba la kifalme ambamo angeliishi, aliiweka nyuma zaidi, ikiwa na mjengo wa aina moja na hiyo nyingine. Pia Solomoni akajenga jumba la kifalme linalofanana na huo ukumbi mkubwa kwa ajili ya binti Farao, aliyekuwa amemwoa.

97:9 Neh 2:8Ujenzi huu wote, kuanzia nje mpaka kwenye ua mkuu na kuanzia kwenye msingi hadi upenuni, ulifanywa kwa mawe ya ubora wa hali ya juu yaliyokuwa yamechongwa kwa vipimo na kusawazishwa kwa msumeno nyuso zake za ndani na za nje. 107:10 Kum 33:10; Neh 8:1-8; 2Tim 4:2; 1Sam 7:3; 2Nya 12:14; Za 10:18; 119:45; Mal 2:7Misingi iliwekwa kwa mawe makubwa yaliyo bora, yenye urefu wa dhiraa kumi7:10 Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5. na mengine yenye urefu wa dhiraa nane7:10 Dhiraa nane ni sawa na mita 3.6. 11Sehemu za juu kulikuwepo na mawe yenye ubora wa hali ya juu, yaliyokatwa kwa vipimo na boriti za mierezi. 127:12 Dan 2:37; Ezr 4:10Ule ua mkuu ulizungukwa na ukuta wa safu tatu za mawe yaliyochongwa na safu moja ya boriti za mierezi zilizorembwa, kama ulivyokuwa ua wa ndani wa Hekalu la Bwana na baraza yake.

Samani Za Hekalu

(2 Nyakati 4)

13Mfalme Solomoni akatuma watu Tiro kumleta Hiramu, 147:14 Es 1:14ambaye mama yake alikuwa mjane kutoka kabila la Naftali na baba yake alikuwa mtu wa Tiro tena fundi wa shaba. Hiramu alikuwa na ustadi wa hali ya juu na mzoefu katika aina zote za kazi ya shaba. Alikuja kwa Mfalme Solomoni na kufanya kazi zake zote alizopangiwa.

157:15 Kum 12:5; 1Nya 29:6; 2Nya 6:2; Za 135:21Hiramu akasubu nguzo mbili za shaba, kila moja ikiwa na urefu wa dhiraa kumi na nane,7:15 Dhiraa 18 ni sawa na mita 8.1. kila nguzo ikiwa na mzingo wa dhiraa kumi na mbili7:15 Dhiraa 12 ni sawa na mita 5.4. kwa mstari. 167:16 Kut 3:22; Ezr 8:25; Zek 6:10; 1Nya 29:6Pia alitengeneza mataji mawili ya shaba ya kusubu ili kuyaweka juu ya hizo nguzo; kila taji lilikuwa na kimo cha dhiraa tano7:16 Dhiraa 5 ni sawa na mita 2.25. kwenda juu. 177:17 2Fal 3:5; Hes 15:5-12Wavu wa mikufu iliyosokotewa kwenye zile taji juu ya zile nguzo, saba kwa kila taji. 18Akatengeneza makomamanga katika safu mbili kuzunguka kila wavu kuremba mataji yaliyo juu ya nguzo. Alifanya hivyo kwa kila nguzo. 197:19 Ezr 5:14; Yer 27:22Mataji yaliyokuwa juu ya nguzo kwenye baraza, yalikuwa katika umbo la yungiyungi, kimo chake ni dhiraa nne7:19 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. 207:20 Ezr 6:4; 1Kor 4:1-2Juu ya mataji ya zile nguzo mbili, juu ya ile sehemu yenye umbo kama bakuli, karibu na ule wavu, kulikuwa na yale makomamanga 200 katika safu kuzunguka pande zote. 217:21 Ezr 4:16-20; 5:3-6Hiramu akasimamisha nguzo kwenye baraza ya Hekalu. Nguzo ya upande wa kusini akaiita Yakini,7:21 Yakini maana yake Mungu atafanya imara. na ile ya upande wa kaskazini Boazi.7:21 Boazi maana yake Ndani ya Mungu kuna nguvu. 22Mataji yaliyokuwa juu yalikuwa na umbo la yungiyungi. Hivyo kazi ya nguzo ikakamilika.

237:23 Ezr 6:10; Isa 60:12; Yer 12:14; Za 68:29; 1Tim 2:1-2Hiramu akasubu Bahari ya chuma, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Mzunguko wake ulikuwa dhiraa thelathini. 247:24 Ezr 4:13; 8:36Chini ya ukingo, ilizungukwa na maboga, kumi kwenye kila dhiraa moja. Maboga yalikuwa yamesubiwa katika safu mbili ili kuwa kitu kimoja na hiyo bahari.

257:25 Kut 18:21-26; 16:18; Za 19:7; Kol 1:28; Kum 16:18; 2Nya 17:7; Mal 2:7; Mt 13:52Bahari iliwekwa juu ya mafahali kumi na wawili, watatu wakielekea kaskazini, watatu wakielekea magharibi, watatu wakielekea kusini na watatu wakielekea mashariki. Bahari iliwekwa juu yao na sehemu zao za nyuma zilielekeana. 267:26 Eze 6:11Ilikuwa na unene wa nyanda nne7:26 Nyanda nne ni sawa na sentimita 32. Nyanda moja ni sawa na upana wa kiganja kimoja, ambacho ni sawasawa na sentimita 8. na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Iliweza kuchukua bathi 2,000.7:26 Bathi 2,000 ni sawa na lita 40,000.

277:27 Ezr 6:22; 1Nya 29:12; Neh 2:12; 2Kor 8:16; Flp 4:10; Mit 16:7Pia akatengeneza vitako kumi vya shaba vinavyoweza kuhamishika, kila kimoja kilikuwa na urefu wa dhiraa nne, upana dhiraa nne na kimo chake dhiraa tatu7:27 Dhiraa 3 ni sawa na mita 1.35. 287:28 2Fal 25:28; Ezr 5:5; 9:9; Neh 1:11Hivi ndivyo vile vitako vilivyotengenezwa: Vilikuwa na mbao za pembeni zilizoshikamanishwa na mihimili. 29Juu ya mbao kati ya hiyo mihimili kulikuwa na simba, mafahali na makerubi, pia kwenye mihimili yake. Juu na chini ya simba na mafahali kulikuwa kumesokotewa taji za kufuliwa. 30Kila kitako kilikuwa na magurudumu manne ya shaba, na vyuma vya katikati vya kuyazungusha hayo magurudumu na kila kimoja kilikuwa na sinia kwenye vishikizo vinne vya taji iliyosubiwa kila upande. 31Ndani ya kitako kulikuwa na nafasi ya wazi iliyokuwa na umbile la mviringo lenye kina cha dhiraa moja.7:31 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. Nafasi hii ya wazi ilikuwa ya mviringo, pamoja na kitako chake ilikuwa dhiraa moja na nusu.7:31 Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5. Kuzunguka huo mdomo wake kulitiwa nakshi. Papi za vitako zilikuwa mraba na si za mviringo. 32Magurudumu manne yalikuwa chini ya papi, na vyuma vya katikati vya kuzungushia magurudumu hayo vilikuwa vimeunganishwa kwenye kitako. Kipenyo cha kila gurudumu kilikuwa dhiraa moja na nusu. 33Magurudumu yalitengenezwa kama ya magari ya vita ya kukokotwa, vyuma vya katikati vya magurudumu, duara zake, matindi yake na vikombe vyake vyote vilikuwa vya kusubu.

34Kila kitako kilikuwa na mikono minne, moja kwenye kila pembe, ukitokeza kutoka kwenye kitako. 35Juu ya kitako kulikuwepo na utepe wa mviringo wenye kina cha nusu dhiraa. Vishikio na papi vilishikamana upande wa juu wa kitako. 36Alitia nakshi za makerubi, simba na miti ya mitende juu ya uso wa vishikio na juu ya papi, katika kila nafasi iliyopatikana, pamoja na mataji yaliyosokotwa kuzunguka pande zote. 37Hivi ndivyo Hiramu alivyotengeneza vile vitako kumi. Vyote vilikuwa vya kusubu kwenye kalibu za kufanana kwa vipimo na kwa umbo.

38Kisha akatengeneza masinia kumi ya shaba, kila moja likiwa na ujazo wa bathi arobaini,7:38 Bathi 40 ni sawa na lita 800. yakiwa na kipenyo cha dhiraa nne7:38 Dhiraa nne ni sawa na mita 1.8. kila sinia moja kwa kila kimoja ya vile vitako kumi. 39Aliweka vitako vitano upande wa kusini wa Hekalu na vingine vitano upande wa kaskazini. Akaweka ile bahari upande wa kusini, katika pembe ya kusini ya Hekalu. 40Pia akatengeneza masinia, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi zote katika Hekalu la Bwana kama vile Mfalme Solomoni alikuwa amemwagiza, yaani:

41nguzo mbili;

mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo;

nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo;

42makomamanga 400 kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);

43vitako kumi pamoja na masinia yake kumi;

44ile Bahari ya chuma na yale mafahali kumi na wawili chini yake;

45masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia.

Vyombo hivi vyote ambavyo Huramu alimtengenezea Mfalme Solomoni kwa ajili ya Hekalu la Bwana vilikuwa vya shaba iliyongʼarishwa. 46Mfalme akaamuru wavisubu katika kalibu ya udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani ulio kati ya Sukothi na Sarethani. 47Solomoni akaviacha vitu hivi vyote bila kupima uzani wake, kwa sababu vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzito wa shaba haungekadirika.

48Solomoni pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Bwana:

madhabahu ya dhahabu;

meza ya dhahabu za kuweka mikate ya Wonyesho;

49vinara vya taa vya dhahabu safi (vitano upande wa kuume na vitano upande wa kushoto, mbele ya Patakatifu pa Patakatifu);

kazi ya maua ya dhahabu na taa na makoleo;

50masinia ya dhahabu safi, mikasi ya kusawazishia tambi, mabakuli ya kunyunyizia, vyano na vyetezo;

na bawaba za dhahabu kwa ajili ya milango ya chumba cha ndani sana, yaani Patakatifu pa Patakatifu, na pia kwa ajili ya milango ya ukumbi mkuu wa Hekalu.

51Hivyo Mfalme Solomoni alipomaliza kazi ya Hekalu la Bwana, akaviingiza ndani vile vitu ambavyo Daudi baba yake alikuwa ameviweka wakfu: yaani fedha, dhahabu na samani; kisha akaviweka katika hazina za Hekalu la Bwana.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

列王紀上 7:1-51

所羅門的王宮

1所羅門用了十三年的時間為自己興建王宮。 2他建造的黎巴嫩林宮長四十五米,寬二十二米半,高十三米半,有四行香柏木柱,柱子支撐著香柏木橫梁。 3每一行木柱有十五根,共四十五根。殿頂鋪香柏木板。 4宮殿有三排窗戶,窗與窗相對; 5宮殿的門框和窗戶都是方形的,三排窗戶彼此相對。

6他又建了一座有柱子的廊子,長二十二米半,寬十三米半,前面還有帶柱子的門廊和篷子。 7此外,他又建造了一個判案的公堂。堂內從地板到天花板都鋪上了香柏木。 8所羅門的寢宮就在公堂後面的院內,建築樣式和公堂相同。所羅門又為所娶的法老之女造了一座與公堂相同的宮室。

9這些宮殿,從根基到牆頂,從外院到內殿用的都是上等的石頭,按規格裡外用鋸切割整齊。 10根基用的是非常珍貴的石頭,它們的體積巨大,有些甚至是長達三米半至四米半的巨石, 11上面是按照規格鑿好的上等石頭以及香柏木。 12大院周圍的牆由三層鑿好的石頭和一層香柏木建成,正如耶和華殿的內院和殿廊的牆。

戶蘭造聖殿的器具

13所羅門王派人從泰爾戶蘭召來。 14戶蘭拿弗他利支派一個寡婦的兒子,父親是泰爾的銅匠。戶蘭聰明伶俐,技術高超,擅長製造各種銅器。他前來朝見所羅門王,領命負責一切銅器工程。

15他鑄造了兩根銅柱,每根高八米,周長五米四, 16然後用銅鑄造了兩個高兩米二的柱冠,安在柱頂上。 17每一個柱冠上裝飾著七條鏈子織成的網, 18網周圍環繞著兩行石榴,用來遮蓋柱冠。 19門廊的柱冠高一米八,形狀像百合花。 20在每個柱冠靠近網子鼓起來的地方圍著兩行石榴,共二百個。 21他把兩根柱子立在殿廊前,南邊那根稱為雅斤,北邊那根稱為波阿斯22柱冠的形狀像百合花。這樣,銅柱就造成了。

23他又鑄了一個圓形銅海,高兩米二,直徑四米半,周長十三米半。 24銅海邊緣下面有兩圈野瓜圖案,每米有二十個野瓜,是跟銅海一起鑄造的。 25有十二頭銅牛馱著銅海,三頭向北,三頭向西,三頭向南,三頭向東。銅海安在牛上,牛尾向內。 26銅海厚八釐米,邊如杯邊,又如百合花,容量是四萬四千升。 27戶蘭用銅造了十個盆座,每個長一米八,寬一米八,高一米三。 28盆座四面裝上鑲板,鑲板固定在框架上。 29鑲板和框架上刻著獅子、牛和基路伯天使,獅子和牛的上面和下面雕刻著花環。 30每一個盆座都有四個銅輪和銅軸,盆放在有四個支腳鑄成的盆架上,盆架周圍有花環圖案。 31盆座的開口呈圓形,深四十五釐米,直徑七十釐米,開口周圍有雕刻。鑲板是方形的,不是圓形的, 32下面有四個七十釐米高的輪子,輪軸固定在盆座上。 33輪子的樣式像戰車的輪子,軸、輞、輻、轂都是鑄成的。 34每個盆座的四角都有支腳,支腳和盆座鑄成一體。 35盆座上有一個高二十三釐米的圓架,上面的支架和鑲板與盆座鑄成一體。 36支架和鑲板都刻上基路伯天使、獅子和棕樹的圖案,周圍有花環圖案。 37十個盆座的鑄法、大小和形狀相同。 38他又用銅製造了十個盆,盆徑一米八,容量八百八十升。十個銅盆分別放在十個盆座上。 39殿門左右各放五個盆座。銅海放在殿的東南角。

40戶蘭又造了鍋、鏟和碗。他為所羅門王完成了耶和華殿的一切工作。 41他所製造的有兩根柱子,兩個碗狀的柱冠,兩個裝飾柱冠的網子, 42四百個安在網子上的石榴,每個網子上兩行石榴,用來裝飾碗狀的柱冠; 43十個盆座及盆座上的十個盆; 44銅海和銅海下面的十二頭銅牛; 45鍋、鏟、碗。這些都是戶蘭所羅門王用磨亮的銅為耶和華的殿造的器具。 46這些都是照王的命令在疏割撒拉但之間的約旦平原用泥模鑄成的。 47所羅門沒有稱過這些器具,因為太多,銅的重量無法統計。

48所羅門又為耶和華的殿造了以下器具:金壇和放供餅的金桌; 49至聖所前面的純金燈臺,左右各五個;燈臺上的金花、燈盞和燈剪; 50純金造的杯、燈剪、碗、碟和火鼎,以及至聖所和外殿入口的金門樞。

51所羅門王完成耶和華殿的一切工作後,就把他父親大衛獻給耶和華的金銀和器具都搬進耶和華殿的庫房。