1 Samweli 8 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 8:1-22

Israeli Waomba Mfalme

18:1 Kum 16:18-19; Amu 10:4; 12:14Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli. 28:2 1Nya 6:28; Mwa 22; 19; 1Fal 19:3; Amo 5:4-5Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba. 38:3 1Sam 2:12; Neh 9:29; Ay 34:27; Za 14:3; 58:3; Isa 53:6; Kut 23:8; 1Sam 12:3; Mit 17:23; Kut 23:2; Kum 16:19Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.

48:4 Amu 11:11; 1Sam 11:3; 7:17Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama. 58:5 Kum 17:14-20; 1Sam 10:19; 12:12-13; 3:20; 12:2; Hos 13:11Wakamwambia, “Wewe umekuwa mzee, nao wanao hawaenendi katika njia zako, sasa tuteulie mfalme wa kutuongoza, kama ilivyo kwa mataifa mengine yote.”

68:6 Hos 13:10; 1Sam 12:17; 15:11; 16:1Lakini wao waliposema, “Tupe mfalme wa kutuongoza,” hili lilimchukiza Samweli, hivyo akamwomba Bwana. 78:7 1Sam 12:1; Hes 11:20; Kut 16:8; Mt 10:24-25; Lk 10:16; Yn 13:16; 1Sam 10:19Naye Bwana akamwambia: “Sikiliza yale yote watu wanakuambia. Si wewe ambaye wamekukataa, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme wao. 88:8 1Sam 12:10; 2Fal 21:22; Yer 2:17Kama vile walivyofanya tangu siku nilipowapandisha kutoka Misri mpaka siku hii ya leo; wakiniacha mimi na kutumikia miungu mingine, ndivyo wanavyokufanyia wewe. 98:9 Kum 17:14-20; 1Sam 8:11-18; 10:25Sasa wasikilize, lakini waonye kwa makini na uwafahamishe yale watakayotendewa na mfalme atakayewatawala.”

108:10 Kut 19:7Samweli akawaambia wale watu waliokuwa wakiomba wapewe mfalme maneno yote ya Bwana. 118:11 1Sam 10:25; 14:52; Mwa 41:46; Kum 17:16; 2Sam 15:1; 2Nya 1:14; 9:25; Wim 3:7; 1Nya 1:5Akasema, “Hivi ndivyo atakavyowatendea mfalme atakayewatawala. Atawachukua wana wenu na kuwafanya watumike kwa magari yake ya vita na farasi, nao watakimbia mbele ya magari yake. 128:12 Kum 1:15; 1Sam 22:7Baadhi yao atawaweka kuwa majemadari wa jeshi wa maelfu na majemadari wa jeshi wa hamsini, wengine kulima mashamba yake na kuvuna mavuno yake, pia na wengine kutengeneza silaha za vita na vifaa kwa ajili ya magari yake. 13Atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi na waokaji. 148:14 1Sam 28:6; Ay 27:9; 35:12-13; Za 18:41; 66:18; Mit 1:28; Isa 58:4; 59:2; Yer 14:12; Eze 8:18; Mik 3:4; 1Sam 10:25; 1Fal 12:4Atayachukua mashamba yenu yaliyo mazuri, mashamba ya mizabibu na mashamba yenu ya mizeituni na kuwapa watumishi wake. 158:15 Mwa 41:34; 1Sam 17:25Ataichukua sehemu ya kumi ya nafaka yenu na ya zabibu zenu na kuwapa maafisa wake na watumishi wake. 16Atawachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike, na ngʼombe wenu walio wazuri sana na punda kwa matumizi yake mwenyewe. 17Atachukua sehemu ya kumi ya makundi yenu ya kondoo na mbuzi, na ninyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. 188:18 1Sam 28:6; Ay 27:9; 35:12-13; Za 18:41; 66:18; Mit 1:28; Isa 58:4; 59:2; Yer 14:12; Eze 8:18; Mik 3:4; 1Sam 10:25; 1Fal 12:4Siku ile itakapowadia, mtalia kwa kutaka msaada kutokana na mfalme mliyemchagua, naye Bwana hatawajibu.”

198:19 Mit 1:24; Isa 50:2; 66:4; Yer 7:13; 8; 12; 13; 10; 44:16; Mdo 13:21Lakini watu wakakataa kumsikiliza Samweli wakasema, “Hapana! Tunataka mfalme wa kututawala. 20Kisha tutakuwa kama mataifa mengine yote, tukiwa na mfalme wa kutuongoza na kwenda mbele yetu na kutupigania vita vyetu.”

218:21 Amu 11:11Samweli aliposikia yote watu waliyosema, akarudia kuyasema mbele za Bwana. 228:22 Hos 13:11Bwana akamjibu, “Wasikilize na uwape mfalme.”

Kisha Samweli akawaambia watu wa Israeli, “Kila mmoja arudi mjini kwake.”

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

撒母耳記上 8:1-22

以色列人要求立王

1撒母耳在年老的時候立了他的兒子做以色列人的士師。 2他的長子是約珥,次子是亞比亞,他們在別示巴做士師。 3然而,他們沒有效法自己的父親,反而愛慕不義之財,貪贓枉法。

4於是,以色列的長老一起到拉瑪去見撒母耳5說:「你年紀大了,你的兒子不效法你。現在求你為我們立一個王治理我們,像其他國家一樣。」 6撒母耳聽到他們要求立一個王治理他們,心中不悅,就向耶和華禱告。 7耶和華對撒母耳說:「你照他們所說的去做吧,因為他們不是拒絕你,而是拒絕我做他們的王。 8自從我帶他們出埃及那天一直到今日,他們常常背棄我,去供奉其他神明。現在,他們也這樣對待你。 9你就照他們所求的去做吧!但你要嚴厲地警告他們,讓他們知道將來王會怎樣管轄他們。」

10撒母耳就把耶和華的話轉告給那些請求他立王的民眾,說: 11「將來管轄你們的王會徵用你們的兒子做他的戰車兵、騎兵,要他們跑在他的戰車前面。 12他會派一些人做千夫長、五十夫長,一些人為他耕種田地、收割莊稼,一些人製造兵器和戰車的裝備。 13他會把你們的女兒帶走,要她們給他造香膏、煮飯和烤餅。 14他會奪去你們最好的田地、葡萄園和橄欖園,送給他的臣僕。 15他會從你們的糧食和葡萄園的出產中收取十分之一,送給他的官員和臣僕。 16他會徵用你們的僕婢及最好的牛8·16 「牛」有古卷作「青年」。和驢來為他效勞。 17他會拿去你們羊群的十分之一,你們必做他的奴僕。 18那時你們會因所選之王的壓迫而呼求耶和華,耶和華卻不會垂聽。」

19民眾卻不肯聽從撒母耳的話。他們說:「不,我們想要一個王治理我們, 20這樣我們就會像其他國家一樣,有王來統治我們,率領我們,為我們作戰。」 21撒母耳聽後,就把民眾這些話轉告耶和華。 22耶和華對撒母耳說:「照他們說的去為他們立一個王吧。」於是,撒母耳以色列人說:「你們各人回自己的城去吧。」