1 Nyakati 24 – NEN & CCBT

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 24:1-31

Migawanyo Ya Makuhani

124:1 2Nya 5:11; Ezr 6:18; Kut 6:23; Hes 3:2-4; 26:60Hii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. 224:2 Law 10:1-2; Hes 3:4; 26:61Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. 324:3 2Sam 8:17Akisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. 4Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. 524:5 1Nya 26:13; Mdo 1:26; Yos 18:10; Mit 16:33; 18:18Waliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

624:6 1Nya 18:16; Neh 8:4; 1Fal 4:3Mwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

724:7 Ezr 2:36; Neh 7:39; 12:6Kura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,

ya pili Yedaya,

824:8 Ezr 10:21; Neh 12:4-6ya tatu Harimu,

ya nne Seorimu,

9ya tano Malkiya,

ya sita Miyamini,

1024:10 Neh 12:4, 17; Lk 1:5ya saba Hakosi,

ya nane Abiya,

11ya tisa Yeshua,

ya kumi Shekania,

12ya kumi na moja Eliashibu,

ya kumi na mbili Yakimu,

13ya kumi na tatu Hupa,

ya kumi na nne Yeshebeabu,

1424:14 Ezr 2:37; Yer 20:1ya kumi na tano Bilga,

ya kumi na sita Imeri,

1524:15 Neh 10:20ya kumi na saba Heziri,

ya kumi na nane Hapisesi,

16ya kumi na tisa Pethahia,

ya ishirini Yehezkeli,

17ya ishirini na moja Yakini,

ya ishirini na mbili Gamuli,

18ya ishirini na tatu Delaya,

ya ishirini na nne Maazia.

1924:19 1Nya 9:25; Hes 4:49; 2Fal 5:7; Lk 1:18-23Huu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

Walawi Waliobaki

2024:20 1Nya 23:6-17Kuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;

kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.

21Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:

Ishia alikuwa wa kwanza.

22Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,

kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.

2324:23 1Nya 23:19; 15:9Wana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.

24Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;

kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.

2524:25 1Nya 22:9Ndugu yake Mika: alikuwa Ishia;

na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.

2624:26 1Nya 6:19; 23:21; Hes 3:20; Kut 6:19Wana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.

Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.

27Wana wa Merari:

kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.

2824:28 1Nya 23:22Kutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.

29Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:

alikuwa Yerameeli.

3024:30 1Nya 23:23Nao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao. 31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

歷代志上 24:1-31

祭司的職務

1下面是亞倫子孫的班次。亞倫的兒子是拿答亞比戶以利亞撒以他瑪2拿答亞比戶比父親先死,而且沒有留下兒子,因此以利亞撒以他瑪做了祭司。 3以利亞撒的子孫撒督以他瑪的子孫亞希米勒的協助下,大衛亞倫的子孫分成班次,讓他們各司其職。 4以利亞撒的子孫中做首領的比以他瑪的子孫中做首領的多,他們被分成班次:以利亞撒的子孫中有十六個族長,以他瑪的子孫中有八個族長。 5因為以利亞撒以他瑪的子孫中都有人在聖所做首領事奉上帝,他們便用抽籤的方法公平地分班。 6利未拿坦業的兒子示瑪雅是書記。他在君王、首領、撒督祭司、亞比亞他的兒子亞希米勒、眾祭司和利未人的族長面前把抽出的名字記錄下來。他們從以利亞撒的子孫中抽出一族,從以他瑪的子孫中抽出一族。

7第一籤抽出來的是耶何雅立,第二籤是耶大雅8第三籤是哈琳,第四籤是梭琳9第五籤是瑪基雅,第六籤是米雅民10第七籤是哈歌斯,第八籤是亞比雅11第九籤是耶書亞,第十籤是示迦尼12第十一籤是以利亞實,第十二籤是雅金13第十三籤是胡巴,第十四籤是耶是比押14第十五籤是璧迦,第十六籤是音麥15第十七籤是希悉,第十八籤是哈辟悉16第十九籤是毗他希雅,第二十籤是以西結17第二十一籤是雅斤,第二十二籤是迦末18第二十三籤是第來雅,第二十四籤是瑪西亞19他們照這班次,按以色列的上帝耶和華藉他們的祖先亞倫所定的條例,在耶和華的殿裡司職。

20其他利未人還有暗蘭的後代書巴業書巴業的後裔耶希底亞21利哈比雅的長子伊示雅22以斯哈的後代示羅摩示羅摩的後代雅哈23希伯倫的長子耶利雅、次子亞瑪利亞、三子雅哈悉、四子耶加緬24烏薛的後代米迦米迦的後代沙密25米迦的弟兄伊示雅伊示雅的後代撒迦利雅26米拉利的兒子抹利姆示雅西雅雅西雅的兒子比挪27米拉利的後代雅西雅的兒子比挪朔含撒刻伊比利28抹利的兒子以利亞撒以利亞撒沒有兒子, 29基士的後代耶拉篾30姆示的兒子末力以得耶利摩。這些按宗族都是利未人的後代。 31他們也在大衛王、撒督亞希米勒、眾祭司和利未人的族長面前抽籤,不分長幼,正如他們的親族亞倫的後代所做的一樣。