士師記 20 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

士師記 20:1-48

討伐基比亞

1於是,從別示巴以及基列的全體以色列人齊心來到米斯巴,聚集在耶和華面前。 2以色列各支派的首領都參加了這次上帝子民的聚會,當時有四十萬持刀的步兵。 3便雅憫人也聽見以色列人聚集在米斯巴的消息。以色列人問那個利未人:「請告訴我們,這件邪惡的事是怎麼發生的?」 4利未人,就是被害女子的丈夫說:「我和我的妾到便雅憫基比亞住宿。 5那天晚上,基比亞人攻擊我,包圍我們住宿的房子,要殺死我。他們把我的妾蹂躪致死。 6我就把她的屍體切成塊,送到以色列的各個地區,因為基比亞人做了邪惡、無恥的事。 7以色列人啊,你們看該怎麼處理吧!」

8眾人起來異口同聲地說:「我們誰也不回帳篷,誰也不回家。 9現在我們要抽籤去攻打基比亞10我們要從各支派中抽出十分之一的人負責運糧,等軍隊到達便雅憫基比亞後,就可以討伐在以色列做出這種卑鄙之事的基比亞人。」 11於是,以色列人團結一致,一起去攻打那城。

12以色列各支派差人去對便雅憫各地的人說:「你們中間怎麼發生了這種邪惡的事! 13現在把那些基比亞的無賴交出來,我們要處死他們,從以色列剷除罪惡。」便雅憫人卻充耳不聞, 14還從各城聚集到基比亞,要跟以色列人打仗。 15便雅憫人從各城召集了兩萬六千刀兵,還從基比亞召集了七百精兵。 16軍中有七百精兵善用左手甩石,毫髮不差。 17其他十一個以色列支派則召集了四十萬刀兵,個個善戰。

18以色列人到伯特利去求問上帝,說:「我們當中哪個支派應當先去攻打便雅憫人呢?」耶和華說:「猶大支派。」

19第二天清早,以色列人起來在基比亞附近安營, 20朝著便雅憫人擺開陣勢,準備攻打他們。 21便雅憫人從基比亞出來,當天殺了以色列軍兩萬二千人。 22以色列人重整士氣,仍在前一天列陣的地方列陣。 23列陣之前,他們在耶和華面前一直哀哭到晚上。他們求問耶和華,說:「我們應該再上去攻打我們的同胞便雅憫人嗎?」耶和華說:「要上去攻打他們。」

24第二天,以色列人前去攻打便雅憫人。 25便雅憫人從基比亞出來迎戰,又殺了以色列軍一萬八千刀兵。 26以色列全軍來到伯特利,坐在耶和華面前哀哭,那天他們一直禁食到晚上,又在耶和華面前獻上燔祭和平安祭。 27-28那時,上帝的約櫃就在那裡,亞倫的孫子、以利亞撒的兒子非尼哈任祭司。以色列人求問耶和華,說:「我們應該再去攻打我們的同胞便雅憫人嗎?還是退兵?」耶和華說:「去攻打吧,因為明天我必把他們交在你們手中。」

29以色列人在基比亞周圍設下伏兵。 30第三天,以色列人又像前兩次一樣在基比亞列陣,攻打便雅憫人。 31便雅憫人前來迎戰,被以色列人誘到城外。他們又像前兩次一樣擊殺以色列人,大約三十名以色列人死在通往基比亞伯特利的兩條路上。 32便雅憫人說:「我們又像以前一樣打敗他們了。」但以色列人已經商議好,用詐敗的方法誘敵離城到大路上來。 33以色列全軍在巴力·他瑪列陣反攻,埋伏在基比亞西面的以色列人也衝了出來。 34有一萬以色列精兵從正面攻打基比亞,戰事非常激烈。便雅憫人大禍臨頭了仍懵然不知。 35耶和華幫助以色列人戰勝了便雅憫人。那天,以色列人殺了便雅憫兩萬五千一百刀兵。 36便雅憫人這才意識到自己戰敗了。

原來以色列人在便雅憫人面前詐敗,因為他們仰仗在基比亞附近設下的伏兵。 37那些伏兵迅速衝進基比亞,用刀殺了全城的人。 38以色列人和伏兵已有約定,伏兵在城內點起一股濃煙時, 39以色列人便轉身殺回。便雅憫人殺了詐敗的以色列軍大約三十人,以為像以前一樣打敗了他們。 40這時基比亞城已濃煙滾滾,便雅憫人回頭觀望,只見全城濃煙四起。 41以色列人轉身殺了回來,便雅憫人大驚失色,知道大禍臨頭了。 42他們從以色列人面前轉身逃往曠野,卻無法逃脫。以色列人從各城出來夾攻他們。 43以色列人圍攻便雅憫人,一路追殺他們直到基比亞的東邊。 44便雅憫人共死了一萬八千名勇士。 45餘下的人都逃往曠野的臨門巖,沿途有五千人被殺。以色列人追殺他們,一直追到基頓,又消滅了他們兩千人。 46那天,便雅憫人共死了兩萬五千名英勇的刀兵, 47只有六百人逃到了臨門巖,在那裡住了四個月。 48以色列人回師便雅憫境內,用刀將各城的男女老少以及牲畜全部殺死,又放火燒毀所有的城邑。

Kiswahili Contemporary Version

Waamuzi 20:1-48

Waisraeli Wapigana Na Wabenyamini

120:1 Amu 21:5; Mwa 21:14; 1Sam 3:20; 2Sam 17:11; 24:15; 1Fal 4:25; 1Sam 11:7; 7:5; Yos 11:3Ndipo Waisraeli wote kuanzia Dani hadi Beer-Sheba na wa kutoka nchi ya Gileadi wakatoka kama mtu mmoja wakakusanyika mbele za Bwana huko Mispa. 220:2 1Sam 11:8; Amu 8:10Viongozi wote wa kabila za Israeli wakakaa kwenye nafasi zao katika kusanyiko la watu wa Mungu, askari 400,000 waendao kwa miguu wenye panga. 3(Wabenyamini wakasikia kuwa Waisraeli wamepanda kwenda Mispa.) Ndipo Waisraeli wakasema, “Tuelezeni jinsi jambo hili ovu lilivyotendeka.”

420:4 Yos 15:57; Mwa 24:23; Amu 19:15Hivyo yule Mlawi, mume wa yule mwanamke aliyeuawa, akasema, “Mimi na suria wangu tulifika Gibea ya Benyamini ili tulale huko. 5Wakati wa usiku watu wa Gibea wakanijia na kuizingira nyumba, wakitaka kuniua. Wakambaka suria wangu mpaka akafa. 620:6 Amu 19:29; 19:23; 2Sam 13:12; Yos 7:15Ndipo nikamchukua suria wangu, nikamkatakata vipande vipande na kuvipeleka katika nchi yote ya urithi wa Israeli, kwa kuwa wametenda uasherati mkubwa na jambo la aibu katika Israeli. 720:7 Amu 19:30Sasa, ninyi Waisraeli wote, semeni na mtoe uamuzi wenu.”

8Watu wote wakainuka wakasema, kama mtu mmoja, “Hakuna hata mmoja wetu atakayekwenda nyumbani. Wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake. 920:9 Law 16:8Sasa hili ndilo tutakaloitendea Gibea: Tutaikabili jinsi kura itakavyotuongoza. 10Tutatoa watu kumi katika kila 100 kutoka kwenye kabila zote za Israeli, watu 100 katika watu 1,000 na watu 1,000 katika 10,000, ili waende wakalete mahitaji kwa ajili ya jeshi. Basi wakati jeshi litakapofika Gibea ya Benyamini, watawatendea yale wanayostahili, kwa ajili ya uovu huu wa aibu waliotenda katika Israeli.” 11Hivyo wanaume wote wa Israeli wakakutanika pamoja na kujiunga kama mtu mmoja dhidi ya huo mji.

1220:12 Kum 13:13-14Makabila ya Israeli yakatuma watu kwenda katika kabila la Benyamini lote na kuwaambia, “Ni uovu gani huu wa kutisha uliotendeka katikati yenu? 1320:13 Kum 13:13; 1Kor 5:13; Kum 13:5Basi watoeni hao watu waovu kabisa walioko Gibea, ili tupate kuwaua na kuondoa uovu katika Israeli.”

Lakini Wabenyamini hawakuwasikia ndugu zao, Waisraeli. 14Wakatoka katika miji yao, wakakutanika Gibea ili kupigana na Waisraeli. 15Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea. 1620:16 Amu 3:15Miongoni mwa hao askari wote kulikuwa na watu 700 bora waliochaguliwa watumiao mkono wa kushoto, kila mmoja wao aliweza kutupa jiwe kwa kombeo na kulenga unywele mmoja bila kukosa.

17Nao watu wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, wakakusanya watu waume 400,000, wenye kutumia panga, wote hao walikuwa mashujaa.

1820:18 Yos 12:9; Amu 18:31; 18:5; Mwa 49:10Waisraeli wakapanda Betheli na kumuuliza Mungu, “Ni nani miongoni mwetu atakayetangulia mbele yetu ili kupigana na Wabenyamini?”

Bwana akawajibu, “Yuda ndiye atakayetangulia.”

19Asubuhi yake Waisraeli wakaamka na kupiga kambi karibu na Gibea. 20Waisraeli wakatoka kupigana na Wabenyamini, nao Waisraeli wakajiweka kwenye nafasi zao katika vita dhidi yao huko Gibea. 21Wabenyamini wakatoka Gibea na kuwaua watu 22,000 wa Israeli siku ile. 22Lakini Waisraeli wakatiana moyo kila mmoja na mwenzake, nao wakajiweka kwenye nafasi zao katika vile vita mara ya pili mahali pale walipokuwa wamejiweka mara ya kwanza. 2320:23 Hes 14:1; Yos 7:6; Amu 18:5Waisraeli wakapanda mbele za Bwana na kulia mbele zake mpaka jioni, nao wakamuuliza Bwana wakisema, “Je, tupande tena kupigana vita na Wabenyamini, ndugu zetu?”

Bwana akajibu, “Pandeni mkapigane nao.”

24Ndipo Waisraeli wakawakaribia Wabenyamini siku ya pili. 25Wakati huu, Wabenyamini walipotoka Gibea ili kupigana nao, wakawaua watu Waisraeli 18,000, wote wakiwa wamejifunga panga.

2620:26 Hes 14:1; 2Sam 12:21; Kut 32:6; Amu 21:4; Law 1:3Ndipo Waisraeli, watu wote, wakapanda Betheli, huko wakakaa mbele za Bwana wakilia. Wakafunga siku ile mpaka jioni na kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani kwa Bwana. 2720:27 Amu 18:5; Hes 10:33Nao Waisraeli wakauliza kwa Bwana. (Katika siku hizo Sanduku la Agano la Mungu lilikuwa huko 2820:28 Hes 25:7; Kum 18:5; Yos 2:24; 24:33; Amu 7:9na Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa Aroni, alikuwa anahudumu mbele za hilo Sanduku.) Wakauliza, “Je, tupande kwenda vitani kupigana tena na Wabenyamini ndugu zetu, au la?”

Bwana akajibu, “Nendeni, kwa kuwa kesho nitawatia mikononi mwenu.”

2920:29 Yos 8:2-4Basi Waisraeli wakaweka waviziao kuizunguka Gibea. 30Kisha Waisraeli wakapanda kupigana na Wabenyamini katika siku ya tatu na kujiweka kwenye nafasi zao dhidi ya Gibea kama walivyokuwa wamefanya hapo kwanza. 3120:31 Yos 8:16; 16:1Wabenyamini wakatoka ili kukabiliana nao, Waisraeli wakawavuta Wabenyamini watoke katika mji. Wakaanza kupigana na kuua watu wapatao thelathini wa Israeli, kama walivyofanya nyakati nyingine, katika njia kuu, moja iendayo Betheli na nyingine Gibea.

32Wabenyamini wakafikiri, “Wanapigwa mbele yetu kama hapo kwanza.” Waisraeli wakasema, “Sisi na turudi nyuma ili tuwavute wauache mji waende kuelekea barabarani.”

3320:33 Yos 8:19Watu wote wa Israeli wakaondoka kwenye sehemu zao na kujipanga huko Baal-Tamari, nao wale waviziaji wa Waisraeli, wakatoka hapo walipokuwa kwenye uwanda wa magharibi ya Gibea. 3420:34 Yos 8:14; Isa 47:11Ndipo watu 10,000 bora waliochaguliwa katika Israeli wote, wakaja kuishambulia Gibea. Vita vilikuwa vikali sana, hata Wabenyamini hawakutambua kuwa maangamizi yalikuwa karibu nao kwa kiasi hicho. 3520:35 1Sam 9:21Bwana akawashinda Wabenyamini mbele ya Waisraeli na siku ile Waisraeli wakawaua Wabenyamini watu waume 25,100, wote wakiwa wenye kujifunga silaha za vita. 3620:36 Yos 8:15Hivyo Wabenyamini wakaona kuwa wamepigwa.

Basi Waisraeli walikuwa wameondoka mbele ya Wabenyamini, kwa sababu Waisraeli waliwategemea hao waviziaji waliokuwa wamewaweka dhidi ya Gibea. 3720:37 Yos 8:19Wale waviziaji wakafanya haraka kuingia Gibea, wakasambaa na kuwaua watu wote wa mji kwa upanga. 3820:38 Yos 8:20; 8:4-8Waisraeli walikuwa wamepatana na hao waviziaji kuwa wangefanya lipande wingu kubwa la moshi kutoka huo mji, 3920:39 Za 78:9ndipo watu wa Waisraeli wangegeuka kupigana.

Watu wa Benyamini walikuwa wameanza kuwapiga na kuua watu wa Israeli (wapatao thelathini), hivyo wakafikiri, “Hakika tutawapiga, kama tulivyowashinda katika vita hapo kwanza.” 4020:40 Yos 8:20Lakini wakati lile wingu la moshi lilipoanza kupanda kutoka ule mji, Wabenyamini wakageuka na kuona moshi wa mji mzima unapaa juu angani. 4120:41 Yos 8:21Ndipo watu wa Israeli wakawageukia, nao Wabenyamini wakatiwa hofu, kwa kuwa walitambua kwamba maafa yamewajia. 42Basi wakakimbia mbele ya Waisraeli kuelekea nyikani, lakini hawakuweza kukwepa vile vita. Nao watu wa Israeli waliotoka katika ile miji wakawaua huko. 43Wakawazingira Wabenyamini pande zote, wakawafuatia na kuwapata hapo walipopumzika katika viunga vya Gibea upande wa mashariki. 4420:44 1Sam 10:26; Za 76:5Wakaanguka Wabenyamini 18,000 ambao wote ni mashujaa. 4520:45 Yos 15:32; Amu 21:13Walipogeuka na kukimbia kuelekea nyikani hata kufikia mwamba wa Rimoni, Waisraeli wakawaua watu 5,000 wakiwa njiani. Wakawafuata kwa kasi mpaka Gidomu huko wakawaua watu wengine 2,000.

4620:46 1Sam 9:21Siku ile wakawaua Wabenyamini 25,000 waliokuwa mashujaa wa vita. 47Lakini watu 600 wakakimbia kuelekea nyikani katika mwamba wa Rimoni, na kukaa huko muda wa miezi minne. 4820:48 Amu 21:23Waisraeli wakarudi na kuua watu wote wa Benyamini, pamoja na wanyama na kila walichokikuta. Pia kila mji waliouona waliuchoma moto.