啟示錄 2 – CCBT & NEN

Chinese Contemporary Bible 2023 (Traditional)

啟示錄 2:1-29

給以弗所教會的信

1「你要寫信告訴以弗所教會的天使,那位右手拿著七顆星、往來於七個金燈臺中間的主說, 2『我知道你的行為、勞碌和堅忍,也知道你嫉惡如仇,曾查驗出那些假冒的使徒,揭穿他們的虛假。 3你曾堅定不移地為我的名受苦,沒有氣餒。 4但有一件事我要責備你,就是你把起初的愛心丟棄了。 5因此,要回想你在哪裡跌倒了,並且悔改,照起初所行的去行。否則,我就要到你那裡,將你的燈臺從原處拿走。 6然而你還有一點可取之處,就是你跟我一樣痛恨尼哥拉黨人的行徑。

7「『聖靈對各教會所說的話,凡有耳朵的都應當聽。我必將上帝樂園中生命樹上的果子賜給得勝者吃。』

給士每拿教會的信

8「你要寫信告訴士每拿教會的天使,那位首先的、末後的、死而復活的主說, 9『我知道你遭受的苦難和貧窮,其實你是富足的。我也知道那些人對你的毀謗,他們自稱是猶太人,其實他們不是,而是撒旦的會眾。 10你不要害怕將要遭受的苦難。看啊,魔鬼要將你們當中的一些人下在監牢,使你們受試煉,你們必遭受十天的迫害。你要至死忠心,我必賜給你生命的冠冕。

11「『聖靈對各教會所說的話,凡有耳朵的都應當聽。得勝者必不被第二次死亡所害。』

給別迦摩教會的信

12「你要寫信告訴別迦摩教會的天使,那位有兩刃利劍的主說, 13『我知道你住在撒旦稱王的地方。但你仍然堅守我的名,即使我忠心的見證人安提帕在你們這撒旦盤踞之處殉道的時候,你也沒有否認對我的信仰。 14不過有幾件事我要責備你:你那裡有人隨從巴蘭的教導,這巴蘭從前教巴勒以色列人面前設置絆腳石,使他們吃祭過偶像的食物並陷入淫亂。 15同樣,你那裡也有人附從尼哥拉黨的教導。 16所以你要悔改,否則我必迅速到你那裡,用我口中的劍攻擊他們。

17「『聖靈對各教會所說的話,凡有耳朵的都應當聽。我必將隱藏的嗎哪賜給得勝者。我也要賜給他一塊白石,石上寫著一個新名字,除了那領受的人以外,沒有人認識。』

給推雅推喇教會的信

18「你要寫信告訴推雅推喇教會的天使,雙目如炬、雙腳像閃亮精銅的上帝的兒子說, 19『我知道你的行為、愛心、信心、事奉和堅忍,也知道你現在所做的善事比起初更多。 20但有一件事我要責備你,就是你容許那自稱是先知的婦人耶洗別教導我的眾奴僕,誘騙他們陷入淫亂並吃祭過偶像的食物。 21我曾給她悔改的機會,她卻不肯痛改自己的淫亂行為, 22所以我必叫她臥病在床。那些與她有染的人若不悔改,也必遭受極大的苦難。 23我要擊殺她的爪牙2·23 「爪牙」希臘文是「兒女」。,使眾教會都知道我洞察人的心思意念,我要照你們各人的行為對待你們。

24「『至於你們其餘在推雅推喇的人,就是不聽那邪說,沒有學習所謂的撒旦玄學的人,我告訴你們,我不會將別的重擔放在你們身上。 25但你們要持守所擁有的,一直到我來。 26-27我怎樣從我父領受了權柄,也必照樣把統治列國的權柄賜給遵守我命令到底的得勝者,他必用鐵杖管轄列國,將他們如同陶器一般打得粉碎。2·26‑27 詩篇2·9 28我也要把晨星賜給他。

29「『聖靈對各教會所說的話,凡有耳朵的都應當聽。』

Kiswahili Contemporary Version

Ufunuo 2:1-29

Kwa Kanisa Lililoko Efeso

12:1 Ufu 1:16; 1:12-13“Kwa malaika wa kanisa lililoko Efeso andika:

“Haya ndiyo maneno ya yule aliyezishika zile nyota saba katika mkono wake wa kuume na ambaye hutembea kati ya vile vinara saba vya taa vya dhahabu. 22:2 1Yn 4:1; 2Kor 11:13Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo. 32:3 Yn 15:21Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.

42:4 Yer 2:2; Mt 24:12“Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza. 52:5 Ufu 1:20Kumbuka basi ni wapi ulikoangukia! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake. 62:6 Ufu 2:15; Za 139:21Lakini una jambo hili kwa upande wako: Unayachukia matendo ya Wanikolai, ambayo nami pia nayachukia.

72:7 Mt 11:15; Ufu 13:9; Mwa 2:9; Ufu 22:2, 14; Lk 23:43“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa haki ya kula matunda toka kwa mti wa uzima, ambao uko katika paradiso2:7 Paradiso hapa ina maana ya Bustani, yaani shamba dogo la miti izaayo matunda. ya Mungu.

Kwa Kanisa Lililoko Smirna

82:8 Ufu 1:11-13“Kwa malaika wa kanisa lililoko Smirna andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye wa Kwanza na wa Mwisho, aliyekufa kisha akafufuka. 92:9 Yak 2:5; Ufu 3:9; Mt 4:10Naijua dhiki yako na umaskini wako, lakini wewe ni tajiri! Nayajua masingizio ya wale wasemao kuwa ni Wayahudi lakini sio, bali wao ni sinagogi la Shetani. 102:10 Ufu 3:10; Dan 1:12-14Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.

112:11 Ufu 20:6-14; 21:8“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatadhuriwa kamwe na mauti ya pili.

Kwa Kanisa Lililoko Pergamo

122:12 Ufu 1:11-16; 1:17, 18; 2:7“Kwa malaika wa Kanisa lililoko Pergamo andika:

“Haya ndiyo maneno yake yeye aliye na upanga mkali wenye makali kuwili. 132:13 Ufu 14:12Ninajua unakoishi, ni kule ambako Shetani ana kiti chake cha enzi. Lakini umelishika Jina langu. Wala hukuikana imani yako kwangu hata katika siku za shahidi wangu mwaminifu Antipa, ambaye aliuawa katika mji mkuu wenu, ambako ndiko anakoishi Shetani.

142:14 1Pet 2:15; 1Kor 6:13“Hata hivyo, nina mambo machache dhidi yako: Unao watu wafuatao mafundisho ya Balaamu, yule aliyemfundisha Balaki kuwashawishi Waisraeli watende dhambi kwa kula vitu vilivyotolewa kafara kwa sanamu na kufanya uasherati. 152:15 Ufu 2:6Vivyo hivyo unao wale wayashikayo mafundisho ya Wanikolai. 162:16 2The 2:8Basi tubu! Ama sivyo, nitakuja kwako upesi na kupigana na watu hao kwa upanga wa kinywa changu.

172:17 Yn 6:49-50; Isa 62:2; Ufu 19:12“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.

Kwa Kanisa Lililoko Thiatira

182:18 Ufu 1:11-15“Kwa malaika wa kanisa lililoko Thiatira andika:

“Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, ambaye macho yake ni kama mwali wa moto na ambaye miguu yake ni kama shaba iliyosuguliwa sana. 192:19 Ufu 2:2Nayajua matendo yako, upendo wako na imani yako, huduma na saburi yako na kwamba matendo yako ya sasa yamezidi yale ya kwanza.

202:20 1Fal 21:25; 2Fal 9:7“Hata hivyo, nina neno dhidi yako: Unamvumilia yule mwanamke Yezebeli ambaye anajiita nabii, lakini anawafundisha na kuwapotosha watumishi wangu ili wafanye uasherati na kula vyakula vilivyotolewa kafara kwa sanamu. 212:21 Rum 2:4; Ufu 9:20Nimempa muda ili atubu kwa ajili ya uasherati wake, lakini hataki. 222:22 Ufu 17:2; 18:9Kwa hiyo nitamtupa kwenye kitanda cha mateso, na nitawafanya hao wanaozini naye kupata mateso makali wasipotubia njia zake. 232:23 1Sam 16:7; Yer 11:20Nami nitawaua watoto wake. Nayo makanisa yote yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake. 242:24 Mdo 15:28Basi nawaambia ninyi wengine mlioko Thiatira, ninyi ambao hamyafuati mafundisho ya Yezebeli, wala hamkujifunza hayo yanayoitwa mambo ya ndani sana ya Shetani (sitaweka mzigo mwingine wowote juu yenu): 252:25 Ufu 3:11Lakini shikeni sana mlicho nacho, mpaka nitakapokuja.

262:26 Za 2:8; Ufu 3:21“Atakayeshinda na kutenda mapenzi yangu mpaka mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa:

272:27 Ufu 12:5; Za 2:9; Yer 19:11“ ‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma,

atawavunja vipande vipande

kama chombo cha udongo’:

kama vile mimi nilivyopokea mamlaka kutoka kwa Baba yangu. 282:28 Ufu 22:16Nami nitampa pia ile nyota ya asubuhi. 29Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa.