民数记 30 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

民数记 30:1-16

许愿的条例

1摩西以色列各支派的首领说:“以下是耶和华的吩咐。

2“人若在什么事上向耶和华许愿或起誓,就不可食言,必须履行诺言。 3倘若未出嫁的少女在什么事上向耶和华许愿或起誓, 4她父亲得知她许的愿或起的誓后没有反对,她许的愿和起的誓就都有效; 5倘若她父亲得知后加以反对,她许的愿和起的誓就无效。耶和华必不追究她,因为她父亲反对。

6“倘若有女子出嫁前许了愿或信口起了誓, 7她丈夫得知后没有反对,她许的愿和起的誓就都有效; 8倘若她丈夫得知后加以反对,她许的愿和起的誓就无效,耶和华必不追究她。 9寡妇或被休的妇人若在什么事上许愿或起誓,就必须履行誓言。

10“倘若已婚妇女在夫家许愿或起誓, 11她丈夫得知后没有反对,她许的愿和起的誓就都有效; 12倘若她丈夫在得知当天加以否定,她口中许的愿和起的誓就无效。她丈夫已经使之无效,耶和华必不追究她。 13丈夫有权赞同或否定妻子禁食所许的愿或起的誓。 14倘若丈夫得知妻子许愿或起誓当天一直没有反对,她就必须履行誓言,因为丈夫当天默认了。 15倘若丈夫当天默认了,后来又加以反对,他就要承担妻子的罪责。”

16以上是耶和华借摩西颁布的有关丈夫和妻子、父亲和未出嫁的女儿要遵守的条例。

Kiswahili Contemporary Version

Hesabu 30:1-16

Nadhiri

130:1 Hes 1:4, 16; 7:2; Kum 1:13, 17Mose akawaambia viongozi wa makabila ya Israeli: “Hili ndilo Bwana analoagiza: 230:2 Kum 23:21-23; Amu 11:23, 30; Ay 22:27; Za 22:25; 50:14; 61:5; 76:11; 116:14; Mit 20:25; Mhu 5:4; Isa 19:21; Yon 1:16; 2:9; Mwa 28; 20; Law 27:2; Za 56:12; 119:106; Law 5:4Mwanaume awekapo nadhiri kwa Bwana, au anapoapa kujifunga kwa ahadi, kamwe asitangue neno lake, bali ni lazima afanye kila kitu alichosema.

3“Wakati mwanamwali anayeishi bado nyumbani kwa baba yake atakapoweka nadhiri kwa Bwana, ama amejifunga mwenyewe kwa ahadi, 4na baba yake akasikia kuhusu nadhiri au ahadi yake lakini asimwambie lolote, ndipo nadhiri zake zote na kila ahadi aliyoiweka na kujifunga kwayo itathibitika. 5Lakini kama baba yake akimkataza wakati anapoisikia, hakuna nadhiri wala ahadi yake yoyote aliyojifunga kwayo itakayosimama; Bwana atamweka huru huyo mwanamwali kwa sababu baba yake amemkataza.

630:6 Law 5:4“Ikiwa ataolewa baada ya kuweka nadhiri au baada ya midomo yake kutamka ahadi fulani bila kufikiri akawa amejifunga hivyo, 7na mume wake akasikia habari hiyo asimwambie neno lolote, ndipo nadhiri zake ama ahadi zake ambazo alikuwa amejifunga nazo zitathibitika. 830:8 Mwa 3:6; 1Kor 7:4; 14:34; Efe 5:22-24; Kol 3:18; 1Tim 2:11-12; 1Pet 3:1Lakini ikiwa mume wake atamkataza atakaposikia kuhusu hilo, atakuwa ametangua nadhiri ambazo zilikuwa zimemfunga mkewe, ama ahadi aliyotamka pasipo kufikiri ambayo amejifunga kwayo, naye Bwana atamweka huru yule mwanamke.

930:9 Law 21:7“Nadhiri yoyote ama patano ambalo limefanywa na mjane ama mwanamke aliyeachwa vitakuwa vimemfunga.

10“Ikiwa mwanamke anayeishi na mumewe ataweka nadhiri ama kujifunga mwenyewe kwa ahadi chini ya kiapo, 11na mumewe akasikia kuhusu jambo hili lakini asimwambie lolote wala hakumkataza, ndipo viapo vyake vyote au ahadi zinazomfunga zitakapothibitika. 1230:12 Efe 5:22; Kol 3:18Lakini ikiwa mumewe atabatilisha nadhiri hizo baada ya kuzisikia, basi hakuna nadhiri au ahadi zozote alizoziweka kwa midomo yake zitakazothibitika. Mumewe atakuwa amezibatilisha, na Bwana atamweka huru yule mwanamke. 13Mumewe anaweza kuthibitisha au kutangua nadhiri yoyote anayoweka, au ahadi yoyote aliyoweka kwa kuapa ili kujikana mwenyewe. 14Lakini ikiwa mumewe hasemi lolote kwake kuhusu jambo hilo siku baada ya siku, basi mumewe atakuwa amethibitisha nadhiri zote, na ahadi zote zinazomfunga mkewe. Anavithibitisha kwa kutokusema lolote kwa mkewe anapoyasikia hayo. 15Hata hivyo, ikiwa mumewe atavibatilisha baada ya kusikia hayo, basi atawajibika kwa hatia ya mkewe.”

16Haya ndiyo masharti ambayo Bwana alimpa Mose kuhusu mahusiano kati ya mtu na mkewe, na kati ya baba na binti yake ambaye bado anaishi nyumbani kwa baba yake.