歌罗西书 2 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

歌罗西书 2:1-23

1我希望你们知道,为了你们和老底嘉人,以及那些从未和我见过面的人,我怎样努力奋斗, 2为要使你们众人心受鼓励,在爱中联结,有丰富笃定的真知灼见,可以认识上帝的奥秘。这奥秘就是基督, 3祂里面蕴藏着一切智慧和知识的宝藏。 4我讲这番话是为了防止有人用花言巧语迷惑你们。 5现在,我人虽不在你们那里,心却和你们在一起,看到你们井然有序,对基督坚信不移,我很喜乐。

生活以基督为中心

6你们既然接受了基督耶稣为主,就当继续遵从祂, 7按照你们所受的教导在祂里面扎根成长,信心坚固,满怀感恩。

8你们要谨慎,免得有人用空洞虚假的哲学把你们掳去。这些哲学不是出于基督,而是出于人的传统和世界的基本规条。 9因为上帝的本质全部有形有体地蕴含在基督里, 10你们在基督里得到了丰盛的生命。祂是一切执政者和掌权者的元首。

11你们也在基督里受了非人手所行的割礼,是基督为除掉你们罪恶本性而行的割礼。 12你们接受洗礼时已经与基督一同埋葬了,并借着相信上帝使基督从死里复活的大能,与基督一同复活了。 13你们从前死在过犯和未被割除的本性中,但现在上帝却使你们与基督一同活了过来。上帝赦免了我们一切的过犯, 14撤销了指控我们违背律法的罪状,把它钉在十字架上,将它消除。 15祂扫除了灵界的诸多权势,用十字架上的胜利公开羞辱它们。

16所以,不可让人在饮食、节期、朔日2:16 “朔日”即每月初一。或安息日的事上论断你们。 17这些都不过是将来之事的影子,实体就是基督。 18有些人喜欢故作谦卑,敬拜天使,沉迷于所看见的幻象,你们不要因他们而失去得奖赏的资格。他们随从自己堕落的思想无故自高自大, 19没有与身体的头基督联结。其实,全身靠关节和筋络维系,从基督得到供应,按上帝的旨意渐渐成长。

20你们既然和基督一同死了,摆脱了世界的基本规条,为什么仍像活在世俗中, 21服从“不可拿、不可尝、不可摸”等规条呢? 22这些规条不过是人的戒律和说教,经不起应用, 23看似充满智慧,其实只不过是自创宗教、自表谦卑、苦待己身,对于克制邪情私欲毫无用处。

Kiswahili Contemporary Version

Wakolosai 2:1-23

12:1 Kol 1:29; 4:12; 4:13, 15, 16; Ufu 1:11Nataka mjue jinsi ninavyojitaabisha kwa ajili yenu na kwa ajili ya wale walioko Laodikia, na pia kwa ajili ya wote ambao hawajapata kuniona mimi binafsi. 22:2 Efe 6:22; Kol 4:8; Rum 16:25Kusudi langu ni watiwe moyo na kuunganishwa katika upendo, ili wapate ule utajiri wa ufahamu mkamilifu, ili waijue siri ya Mungu, yaani, Kristo mwenyewe, 32:3 Isa 11:2; Yer 23:5; Rum 11:33; 1Kor 1:24, 30ambaye ndani yake kumefichwa hazina zote za hekima na maarifa. 42:4 Rum 16:18Nawaambia mambo haya ili mtu yeyote asiwadanganye kwa maneno ya kuwashawishi. 52:5 1Kor 5:4; 1The 2:17Kwa kuwa ingawa mimi siko pamoja nanyi kimwili, lakini niko pamoja nanyi kiroho, nami nafurahi kuuona utaratibu wenu na jinsi uthabiti wa imani yenu katika Kristo ulivyo.

Ukamilifu Wa Maisha Katika Kristo

62:6 Yn 13:13; Kol 1:10Hivyo basi, kama vile mlivyompokea Kristo Yesu kuwa Bwana, endeleeni kukaa ndani yake, 72:7 Efe 3:17; 4:22mkiwa na mizizi, na mmejengwa ndani yake, mkiimarishwa katika imani kama mlivyofundishwa, na kufurika kwa wingi wa shukrani.

82:8 1Tim 6:20; Kol 2:20; Gal 4:2Angalieni mtu yeyote asiwafanye ninyi mateka kwa elimu batili na madanganyo matupu yanayotegemea mapokeo ya wanadamu na mafundisho ya ulimwengu badala ya Kristo.

92:9 Yn 1:16Maana ukamilifu wote wa Uungu umo ndani ya Kristo katika umbile la mwili wa kibinadamu, 102:10 Efe 1:22; Mt 28:18nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Kristo, ambaye ndiye mkuu juu ya kila enzi na kila mamlaka. 112:11 Rum 2:29; Flp 3:3; Gal 5:24Katika Kristo pia mlitahiriwa kwa kutengwa mbali na asili ya dhambi, si kwa tohara inayofanywa kwa mikono ya wanadamu, bali kwa ile tohara iliyofanywa na Kristo, 122:12 Mt 28:19; Rum 6:5; Mdo 2:24mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo, na kufufuliwa pamoja naye kwa njia ya imani yenu katika uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.

132:13 Efe 2:15; 2:5; 4:32Mlipokuwa wafu katika dhambi zenu na kutokutahiriwa katika asili yenu ya dhambi, Mungu aliwafanya mwe hai pamoja na Kristo. Alitusamehe dhambi zetu zote, 142:14 Efe 2:15; 1Pet 2:24akiisha kuifuta ile hati yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili, pamoja na maagizo yake. Aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenye msalaba wake. 152:15 Kol 2:10; Efe 6:12; Mt 12:29; Lk 10:18; Yn 12:31Mungu akiisha kuzivua enzi na mamlaka, alizifanya kuwa kitu cha fedheha hadharani kwa kuziburura kwa ujasiri, akizishinda katika msalaba wa Kristo.

162:16 Rum 14:3, 4; Mk 7:19; Rum 14:17; Law 23:2; Rum 14:5Kwa hiyo mtu asiwahukumu ninyi kuhusu vyakula au vinywaji, au kuhusu kuadhimisha sikukuu za dini, au Sikukuu za Mwezi Mwandamo au siku ya Sabato. 172:17 Ebr 8:5; 10:1Hizi zilikuwa kivuli cha mambo ambayo yangekuja, lakini ile iliyo halisi imo ndani ya Kristo. 182:18 Kol 2:23; 1Kor 9:24; Flp 3:14Mtu yeyote asiwaondolee thawabu yenu kwa kusisitiza kunyenyekea kwake na kuabudu malaika. Mtu kama huyo hudumu katika maono yake, akijivuna bila sababu katika mawazo ya kibinadamu. 192:19 Efe 1:22; 1Kor 2:8; Gal 4:3, 9, 14, 16Yeye amepoteza ushirikiano na Kichwa, ambaye kutoka kwake mwili wote unalishwa na kushikamanishwa pamoja kwa viungo na mishipa, nao hukua kwa ukuaji utokao kwa Mungu.

Maonyo Dhidi Ya Walimu Wa Uongo

20Kwa kuwa mlikufa pamoja na Kristo, mkayaacha yale mafundisho ya msingi ya ulimwengu huu, kwa nini bado mnaishi kama ninyi ni wa ulimwengu? Kwa nini mnajitia chini ya amri: 212:21 1Tim 4:3“Msishike! Msionje! Msiguse!”? 222:22 1Kor 6:13; Isa 29:13; Mt 15:9; Tit 1:14Haya yote mwisho wake ni kuharibika yanapotumiwa, kwa sababu msingi wake ni katika maagizo na mafundisho ya wanadamu. 232:23 Kol 2:18Kwa kweli amri kama hizo huonekana kama zina hekima, katika namna za ibada walizojitungia wenyewe, na unyenyekevu wa uongo na kuutawala mwili kwa ukali, lakini hayafai kitu katika kuzuia tamaa za mwili.