撒迦利亚书 14 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒迦利亚书 14:1-21

耶和华的日子

1看啊,耶和华的日子快到了,那时你那里的财物必被抢掠和瓜分。 2因为我必招聚万国去攻打耶路撒冷。那时,城必失守,房屋必被洗劫,妇女必被玷污。半城的人必被掳去,剩下的人必不会从城中被铲除。 3那时,耶和华必出来与万国争战,像从前争战的日子一样。 4到那天,祂的脚必踏在耶路撒冷东面的橄榄山上,这山必从东至西分成两半,一半向北移,一半向南移,中间形成极大的山谷。 5你们要从我的山谷逃跑,因为山谷必延伸到亚萨。你们必逃跑,像犹大乌西雅年间的人躲避大地震一样。我的上帝耶和华必带着所有的圣者降临。 6到那天,将没有光、严寒和冰霜。 7那将是奇特的日子,没有昼夜之分,晚上仍然有光,只有耶和华知道那日何时来临。

8到那天,必有活水从耶路撒冷涌出,一半流向死海,一半流向地中海,冬夏不变。 9耶和华必做普世的王。到那天,必唯祂独尊,唯祂的名独尊。 10迦巴直到耶路撒冷南边的临门,整个地区都要变为平原。从便雅悯门到旧门,再到角门,从哈楠业楼到王的榨酒池,耶路撒冷必仍然矗立在原处。 11城内必有人居住,不再遭毁灭的咒诅。耶路撒冷必安享太平。

12耶和华必降瘟疫给攻打耶路撒冷的万邦,使他们活着的时候皮肉已经腐烂,眼睛烂在眼眶中,舌头烂在口中。 13到那天,耶和华必使他们慌乱不堪,彼此揪住,互相殴打。 14犹大也必在耶路撒冷争战,四围列国的财物,包括大量的金银和衣服,必被收聚起来。 15同样的瘟疫也必降在马匹、骡子、骆驼、驴和营中的其他牲畜身上。

16前来攻打耶路撒冷的万国中的幸存者,必每年上来敬拜大君王万军之耶和华,并且守住棚节。 17地上万族中若有人不上耶路撒冷敬拜大君王万军之耶和华,他们必得不到雨水。 18埃及人若不上来敬拜,也必得不到雨水,耶和华必使他们和不上来守住棚节的列国一样遭受瘟疫。 19这将是埃及和不上来守住棚节的万国所得的惩罚。 20到那天,马铃上也必刻上“耶和华的圣物”的字样。耶和华殿内的锅必像祭坛前的碗一样圣洁。 21耶路撒冷犹大的锅都是万军之耶和华的圣物,来献祭的人都可以用这些锅煮祭肉。到那天,万军之耶和华的殿中必再也没有商人。

Kiswahili Contemporary Version

Zekaria 14:1-21

Bwana Yuaja Kutawala

114:1 Isa 13:6; 23:18; Yoe 1:15; Mal 4:1Siku ya Bwana inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

214:2 Isa 2:3; Zek 12:3; 13:8; Eze 5:8; Mwa 34:29; Mao 5:11; Isa 13:6; Yoe 3:2Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini.

314:3 Zek 9:14-15; 8:9; Isa 8:9Kisha Bwana atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita. 414:4 Eze 11:23; Hes 16:31; Mdo 1:11-12; Yoe 3:12Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. 514:5 Isa 29:6; 66:15-16; Mt 16:27; 25:31; Yud 14; Mt 24:30; Yoe 3:11Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Bwana Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.

614:6 Isa 13:10; Yer 4:23Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. 714:7 Yer 30:7; Ufu 21:23-25; 22:5; Isa 13:10; 30:26Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Bwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo.

814:8 Eze 47:1-12; Yn 7:38; Ufu 22:1-2; Isa 30:25; Yoe 2:20; Mwa 8:22Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,14:8 Yaani Bahari ya Chumvi au Bahari Mfu. na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi14:8 Yaani Bahari ya Mediterania. wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

914:9 Za 22:28; 47:7; Oba 1:21; Kum 6:4; Isa 45:24; Ufu 15:1; Hab 2:14; Efe 4:5-6; Za 2:8Bwana atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo Bwana mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.

1014:10 1Fal 15:22; Yos 15:32; Isa 2:2; Yer 20:2; 30:18; Amo 9:11; Zek 12:6; 2Fal 14:13; Neh 3:1Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.14:10 Araba maana yake Nchi tambarare. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. 1114:11 Zek 2:4; Za 48:8; Eze 34:25-28; Yer 31:40Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.

1214:12 Isa 11:4; Law 26:16; Kum 28:22; Ay 18:13Hii ndiyo tauni ambayo Bwana atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. 1314:13 Mwa 35:5; Amu 7:22; Zek 11:6; 1Sam 14:15Katika siku hiyo Bwana atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana. 1414:14 Zek 12:2; Isa 23:18Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. 15Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.

1614:16 2Fal 19:31; Za 22:29; 86:9; Isa 19:21; 60:6-9; Oba 1:21; Kut 23:16; Isa 66:23; 1Tim 6:15; Law 23:34; Neh 8:14; Hos 12:9Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 1714:17 2Nya 32:23; Yer 14:4; Amo 4:7; Isa 60:12Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao. 1814:18 Mwa 27:29Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. Bwana ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 1914:19 Ezr 3:4Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

2014:20 Kut 39:30; Eze 46:20; Zek 9:15Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: Takatifu kwa Bwana, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya Bwana vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. 2114:21 Yer 31:40; Rum 14:6-7; 1Kor 10:31; Neh 8:10; 11:1; Eze 44:9; Kol 3:17; Isa 35:8; Ufu 21:27; Efe 2:19Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote.