撒母耳记下 20 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记下 20:1-26

示巴反叛大卫

1有一个无赖名叫示巴,是便雅悯比基利的儿子,当时刚好在吉甲。他吹响号角,大喊:“我们与大卫毫无关系,耶西儿子的产业没有我们的份。以色列人啊,各自回家去吧!” 2于是,以色列人都离开了大卫,跟随了比基利的儿子示巴。但犹大人仍然紧紧跟随他们的王,从约旦河一直来到耶路撒冷3大卫回到耶路撒冷的宫里,把从前留下来看守王宫的十个妃嫔关进冷宫,供养她们,却不再和她们同房。她们像寡妇一样在软禁中度过余生。

4王对亚玛撒说:“你要在三天内招聚犹大人,跟他们一起来见我。” 5亚玛撒就去招聚犹大人,但他超过了王所定的期限。 6大卫亚比筛说:“现在比基利的儿子示巴给我们带来的危害恐怕比押沙龙还要大。你带领我的部下去捉拿他,免得他占据了坚固的城池,得以逃脱。”

7于是,约押的部下和基利提人、比利提人,以及所有的勇士都跟随亚比筛离开耶路撒冷,去追赶比基利的儿子示巴8他们来到基遍的巨石旁,见亚玛撒迎面而来。约押当时身穿战袍,腰间佩刀,他迎上去的时候,刀从鞘中滑落出来。 9约押亚玛撒说:“兄弟,你好吗?”他用右手抓住亚玛撒的胡子,亲吻他。 10亚玛撒毫无防备,被约押一刀刺入肚子,肚破肠流而死。然后,约押和他兄弟亚比筛继续追赶比基利的儿子示巴

11约押的一个部下站在亚玛撒的尸体旁边说:“拥护约押大卫的人来跟随约押吧!” 12亚玛撒的尸体倒在路中间的血泊中。那人见众人驻足围观,便把尸体从路上拖到田里,扔了一件衣服盖上。 13尸体搬走以后,众人都跟随约押去追比基利的儿子示巴

14示巴走遍以色列各支派,一直到伯·玛迦亚比拉城。他的本族比利人都聚集起来跟随他。 15约押率大军来到伯·玛迦,把示巴围困在亚比拉城内,他们修筑攻城的高台,撞击城墙,要摧毁它。 16有一个聪明的妇人从城上喊:“请听我说!请听我说!请约押到这边来,我有话要对他说。” 17约押就走上前去,那妇人问道:“你是约押吗?”约押答道:“我就是。”妇人说:“请听婢女说几句。”约押说:“你说吧!” 18妇人说:“古时候人们常说,‘有事到亚比拉去请教,问题都会解决。’ 19我们这座城的人在以色列素来热爱和平、忠心耿耿,你却要毁灭这座大城。你为什么要吞掉耶和华的产业?” 20约押答道:“我根本不想吞掉或毁灭这城。 21事情不是这样。以法莲山区比基利的儿子示巴背叛大卫王,你们只要把他交出来,我就撤退。”那妇人说:“我们一定把他的首级从城上抛下来给你。” 22妇人把自己的良策告诉众人,他们便把比基利的儿子示巴的头割下来,抛给约押约押就吹响号角令军队各自回家,自己回耶路撒冷见王。

23约押负责统率以色列全军;耶何耶大的儿子比拿雅统管基利提人和比利提人; 24亚多兰管理服劳役的;亚希律的儿子约沙法做史官; 25示法做书记;撒督亚比亚他做祭司; 26雅珥以拉大卫的祭司。

Kiswahili Contemporary Version

2 Samweli 20:1-26

Sheba Aasi Dhidi Ya Daudi

120:1 Mwa 31:14; 29:14; 1Fal 12:16; 1Sam 22:7-8; 2Nya 10:16; 2Sam 12:10; Kum 13:13; Amu 19:22; 1Sam 2:12; 10:27; 1Fal 21:10-13; 2Nya 13:7; 2Sam 19:43Basi, kulikuwa na mtu mbaya sana aliyeitwa Sheba mwana wa Bikri, Mbenyamini, aliyekuwako huko. Akapiga tarumbeta na kupaza sauti,

“Hatuna fungu katika Daudi,

wala hatuna sehemu

katika mwana wa Yese!

Kila mtu aende hemani mwake,

enyi Israeli!”

220:2 Mit 17:14Kwa hiyo watu wote wa Israeli wakamwacha Daudi na kumfuata Sheba mwana Bikri. Lakini watu wa Yuda wakawa karibu na mfalme wao katika safari yote kutoka Yordani mpaka Yerusalemu.

320:3 2Sam 15:16; 16:21-22Daudi aliporudi katika jumba lake la kifalme huko Yerusalemu, aliwachukua wale masuria kumi aliokuwa amewaacha ili kuangalia jumba la kifalme na kuwaweka ndani ya nyumba chini ya ulinzi. Akawapa mahitaji yao lakini hakukutana nao kimwili. Waliwekwa kifungoni wakaishi kama wajane mpaka kifo chao.

420:4 2Sam 17:25; 19:13Ndipo mfalme akamwambia Amasa, “Waite watu wa Yuda waje kwangu katika muda wa siku tatu, nawe mwenyewe uwepo hapa.” 5Lakini Amasa alipokwenda kuwaita Yuda, alichukua muda mrefu zaidi ya ule mfalme aliokuwa amemwekea.

620:6 2Sam 21:17; 1Sam 26:6; 2Sam 18:2; 11:11; 1Fal 1:33Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatuletea madhara zaidi kuliko alivyofanya Absalomu. Wachukue watu wa bwana wako na umfuatie, la sivyo atapata mji wenye ngome na kututoroka.” 720:7 1Sam 30:14; 2Sam 15:18; 1Fal 1:38; 2Sam 8:18Hivyo watu wa Yoabu, na Wakerethi na Wapelethi, pamoja na wapiganaji mashujaa wote wakaondoka chini ya uongozi wa Abishai. Wakatoka Yerusalemu ili kumfuata Sheba mwana wa Bikri.

820:8 Yos 9:3; 2Sam 2:18Wakati walikuwa kwenye mwamba mkubwa huko Gibeoni, Amasa alikuja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa mavazi yake ya kijeshi; juu yake alifunga mkanda kwenye kiuno wenye upanga ndani ya ala. Alipokuwa akienda mbele, ule upanga ukaanguka kutoka kwenye ala.

920:9 Mt 26:49; Lk 22:47; Mwa 4:8; 2Sam 2:23; 3:27; 1Fal 2:5Yoabu akamwambia Amasa, “U hali gani, ndugu yangu?” Kisha Yoabu akamshika Amasa ndevu kwa mkono wake wa kuume ili ambusu. 1020:10 Amu 3:21; 2Sam 3:27; 1Fal 2:5Amasa hakuona upanga uliokuwa mkononi mwa Yoabu, naye Yoabu akamchoma nao tumboni, nayo matumbo yake yakamwagika chini. Pasipo kuchomwa mara ya pili, Amasa akafa. Basi Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.

11Mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa, akasema, “Yeyote ampendaye Yoabu na yeyote aliye upande wa Daudi, na amfuate Yoabu!” 1220:12 2Sam 2:23Amasa alikuwa akigaagaa katika damu yake katikati ya barabara; mtu mmoja akaona kwamba vikosi vyote vilikuwa vinasimama pale. Huyo mtu alipotambua kwamba kila aliyefika pale Amasa alipokuwa alisimama, alimburuta Amasa kutoka barabarani mpaka kwenye shamba na kutupia nguo juu yake. 13Baada ya Amasa kuondolewa kutoka barabarani, watu wote walienda pamoja na Yoabu kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.

1420:14 Hes 21:16; 1Fal 15:20; 2Fal 15:29; 2Nya 16:4Sheba akapita katika makabila yote ya Israeli hadi Abel-Beth-Maaka na kupitia eneo lote la Waberi ambao walijikusanya pamoja na kumfuata. 1520:15 1Fal 15:20; 2Fal 15:29; Isa 37:33; Yer 6:6; 32:24; Lk 19:43Vikosi vyote vya Yoabu vikaja na kumhusuru Sheba mwana wa Bikri huko Abel-Beth-Maaka. Wakauzingira mji kwa kuweka vikosi vya askari, ili kukabiliana na ngome ya mji. Walipokuwa wanagongagonga ukuta ili kuubomoa na kuuangusha chini, 1620:16 2Sam 14:2mwanamke mmoja mwenye busara akaita kutoka ndani ya mji, akisema, “Sikilizeni! Sikilizeni! Mwambieni Yoabu aje hapa ili niweze kuzungumza naye.” 17Yoabu alikwenda mbele yake, akamuuliza, “Wewe ni Yoabu?”

Akamjibu, “Ndiye mimi.”

Yule mwanamke akamwambia, “Sikiliza kile mtumishi wako atakachokuambia.” Akamwambia, “Ninasikiliza.”

18Huyo mwanamke akaendelea kusema, “Zamani za kale walikuwa wakisema, ‘Wakaulize ushauri huko Abeli,’ hivyo kulimaliza lile shauri. 1920:19 Kum 2:26; 1Sam 26:19; 2Sam 21:3Sisi ni watu wa amani na waaminifu katika Israeli. Wewe unajaribu kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kumeza urithi wa Bwana?”

20Yoabu akajibu, “Hilo liwe mbali nami. Hilo liwe mbali nami kumeza au kuharibu. 2120:21 2Sam 4:8Hivyo sivyo ilivyo. Mtu mmoja jina lake Sheba mwana wa Bikri, kutoka nchi ya vilima vya Efraimu, ameinua mkono wake dhidi ya mfalme, dhidi ya Daudi. Nikabidhini mtu huyu mmoja, nami nitajiondoa katika mji huu.”

Huyu mwanamke akamwambia Yoabu, “Kichwa chake mtatupiwa kupitia juu ya ukuta.”

2220:22 Mhu 9:13-14; 7:19Ndipo huyo mwanamke akaenda kwa watu wote akiwa na ushauri wake wa busara, nao wakakata kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumtupia Yoabu. Kwa hiyo Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wake wakatawanyika kutoka mjini, kila mmoja akirejea nyumbani kwake. Naye Yoabu akarudi kwa mfalme huko Yerusalemu.

2320:23 2Sam 2:28; 8:16-18; 24:2Yoabu alikuwa jemadari wa jeshi lote la Israeli; Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; 2420:24 1Fal 4:6; 5:14; 12:18; 2Nya 10:18; 2Sam 8:16; 1Fal 4:3Adoramu alikuwa kiongozi wa wale waliofanya kazi ya kulazimishwa; Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mweka kumbukumbu; 2520:25 1Sam 2:35; 2Sam 8:17Sheva20:25 Sheva mahali pengine ameitwa Shausha (1Nya 18:16; 1Fal 4:3). alikuwa mwandishi; Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani; 2620:26 2Sam 23:38na Ira, Myairi, alikuwa kuhani wa Daudi.