撒母耳记上 6 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记上 6:1-21

约柜回归以色列

1耶和华的约柜在非利士人的地方停留了七个月。 2非利士人叫来他们的祭司和占卜者,问道:“我们该怎样处理耶和华的约柜呢?请告诉我们怎样把它送回原处?” 3他们答道:“你们若把以色列上帝的约柜送回去,不可空手送去,一定要向祂献上赔罪的礼物,这样你们就可以得到医治,也可以知道祂为什么惩罚你们。” 4非利士人问:“我们该送什么作赔罪的礼物呢?”他们答道:“你们要按非利士首领的数目,送五个金毒疮和五只金鼠,因为你们和你们的首领都遭受了同样的灾难。 5所以,你们要制作金毒疮和毁坏田地的老鼠的像,尊崇以色列的上帝,也许祂会放过你们、你们的神明及田地。 6你们为什么像法老和埃及人那样心里顽固呢?当上帝严厉地对待他们时,他们岂没有让以色列人离开埃及吗? 7现在,你们快去准备一辆新车,把两头还在哺养小牛、从未负过轭的母牛套在车上,然后把小牛带回牛圈里。 8你们要把耶和华的约柜放在车上,旁边放箱子,里面装赔罪的金物,然后送这辆车上路。 9你们要留意观察,如果车朝以色列边境的伯·示麦去,这大灾难就是耶和华降给我们的。如果不朝那方向走,我们就知道不是祂惩罚我们,是偶然发生的。”

10于是,非利士人一一照做,他们牵来两头还在哺养小牛的母牛,把它们套在车上,把小牛关在圈里, 11然后把耶和华的约柜和装金鼠以及金毒疮的箱子放在车上。 12母牛边走边叫,不偏不离,径直朝伯·示麦走去。非利士的首领跟着它们一直来到伯·示麦的边界。

13当时,伯·示麦人正在山谷里收割麦子。他们抬头看见约柜,非常高兴。 14车子来到伯·示麦约书亚的田间,在一块巨石旁边停下来。民众劈开车子,把两头母牛献给耶和华作燔祭。 15利未人抬下耶和华的约柜和装着金物的箱子,把它们放在巨石上。那天,伯·示麦人向耶和华献上了燔祭和其他祭物。 16那五个非利士首领看见了这一切后,就在当天回以革伦去了。 17非利士人献给耶和华的金毒疮是分别为亚实突迦萨亚实基伦迦特以革伦赔罪的。 18那五只金鼠是按着非利士五个首领的坚固城邑和村庄的数目献上的。那块安放耶和华约柜的巨石至今还在伯·示麦约书亚的田间。 19那一天,耶和华击杀了七十个6:19 “七十个”有古卷作“五万零七十个”。伯·示麦人,因为他们擅自观看约柜里面。民众为此哀恸不已, 20伯·示麦人说:“谁能站立在这位圣洁的上帝耶和华面前呢?该把约柜送到谁那里呢?” 21后来,他们就派使者到基列·耶琳的居民那里,说:“非利士人已经把耶和华的约柜送回来了,你们下来把它接到你们那里吧。”

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 6:1-21

Sanduku La Mungu Larudishwa Israeli

1Sanduku la Bwana lilipokuwa limekaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba, 26:2 Kut 7:11; Isa 44:25; Mwa 41:8; Dan 2:2; 5:7; Mit 2:4Wafilisti waliwaita makuhani wa Dagoni na waaguzi, na kuwaambia, “Tutafanya nini na hili Sanduku la Bwana? Tuambieni jinsi tutakavyolirudisha mahali pake.”

36:3 Kut 22:29; 34:20; Law 5; 15; Kum 16:16Wakajibu, “Kama mtalirudisha Sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe mikono mitupu bali kwa vyovyote mpelekeeni sadaka ya hatia. Kisha mtaponywa, nanyi mtafahamu kwa nini mkono wake haujaondolewa kwenu.”

46:4 Yos 13:3; Amu 3:3; 2Sam 24:25Wafilisti wakawauliza, “Ni sadaka gani ya hatia tutakayompelekea?”

Wakajibu, “Majipu matano ya dhahabu na panya wa dhahabu watano, kulingana na idadi ya watawala wa Wafilisti, kwa sababu tauni iyo hiyo imewaua ninyi na watawala wenu. 56:5 1Sam 5:6; Yos 7:19; Ufu 14:7; Isa 42:12; Yn 9:24; 1Nya 16:28; Mal 2:2; Kut 9:3; Za 39:10; Mdo 13:11Tengenezeni mifano ya majipu na ya panya wale wanaoharibu nchi yenu, nanyi mheshimuni Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka kwenu na kwa miungu yenu na nchi yenu. 66:6 Kut 4:21; 10:2; 12:33; 7:13; 9:34; Za 105:38Kwa nini ninyi mnafanya mioyo yenu migumu kama Wamisri na Farao walivyofanya? Je, alipowatendea kwa ukali, hawakuwaachia Waisraeli wakaenda zao?

76:7 2Sam 6:3; 1Nya 13:7; Hes 19:2“Sasa basi, wekeni gari jipya la kukokotwa pamoja na ngʼombe wawili ambao wamezaa lakini ambao kamwe hawajafungwa nira. Fungieni hao ngʼombe hilo gari, lakini ondoeni ndama wao na mwaweke zizini. 8Chukueni hilo Sanduku la Bwana na mliweke juu ya gari la kukokotwa, na ndani ya kasha kando yake wekeni hivyo vitu vya dhahabu mnavyompelekea Bwana kama sadaka ya hatia. Lipelekeni, 96:9 Yos 15:10; 21:16lakini liangalieni kwa makini. Iwapo litakwenda katika nchi yake lenyewe, kuelekea Beth-Shemeshi, basi tutajua kwamba Bwana ndiye alileta haya maafa makubwa juu yetu. Lakini kama halikwenda, basi tutajua kwamba haukuwa mkono wa Bwana uliotupiga na kwamba iliyotokea kwetu ni ajali.”

10Basi wakafanya hivyo. Wakachukua ngʼombe wawili wa aina hiyo, wakawafungia hilo gari la kukokotwa, nao ndama wao wakawekwa zizini. 11Wakaliweka Sanduku la Bwana juu ya hilo gari la kukokotwa pamoja na lile kasha lenye ile mifano ya panya wa dhahabu na ya majipu ya dhahabu. 12Kisha hao ngʼombe wakaenda moja kwa moja kuelekea Beth-Shemeshi, wakishuka bila kugeuka kuume au kushoto, huku wakilia njia yote. Watawala wa Wafilisti waliwafuata hao ngʼombe hadi mpakani mwa Beth-Shemeshi.

136:13 Mwa 30:14; Rut 2:23; 1Sam 12:17Wakati huu watu wa Beth-Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao huko bondeni, walipoinua macho yao na kuona lile Sanduku, wakafurahi kuliona. 146:14 1Sam 11:7; 2Sam 24:22; 1Fal 9:21Lile gari la kukokotwa lilikuja mpaka kwenye shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi, nalo likasimama kando ya mwamba mkubwa. Watu wakapasua mbao za lile gari la kukokotwa na kutoa dhabihu wale ngʼombe kama sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana. 156:15 Yos 3:3; 21:16Walawi walilishusha Sanduku la Bwana, pamoja na lile kasha lililokuwa na vile vitu vya dhahabu na kuviweka juu ya ule mwamba mkubwa. Siku ile watu wa Beth-Shemeshi wakatoa sadaka za kuteketezwa na dhabihu kwa Bwana. 166:16 Yos 13:3; Amu 16:23; 1Sam 29:2Wale watawala watano wa Wafilisti waliona haya yote, nao wakarudi siku ile ile mpaka Ekroni.

176:17 Yos 13:3Haya ndiyo yale majipu ya dhahabu Wafilisti waliyotuma kama sadaka ya hatia kwa Bwana, moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni. 18Nayo hesabu ya wale panya wa dhahabu ilikuwa kulingana na idadi ya miji ya Wafilisti ya watawala watano wa Wafilisti: miji yao iliyozungukwa na maboma, pamoja na vijiji vya miji hiyo. Ule mwamba mkubwa, ambao juu yake waliliweka lile Sanduku la Bwana, ni ushahidi hadi leo katika shamba la Yoshua wa Beth-Shemeshi.

196:19 2Sam 6:7; Kut 19:21; Hes 4:5; Law 10:1-3; 2Sam 6:7; Kol 2:8; 1Pet 4:17Lakini Mungu aliwapiga baadhi ya watu wa Beth-Shemeshi, akiwaua watu sabini miongoni mwao kwa sababu walichungulia ndani ya Sanduku la Bwana. Watu wakaomboleza kwa sababu ya pigo zito kutoka kwa Bwana, 206:20 2Sam 6:9; Za 130:3; Ufu 6:17; Mal 3:2; Law 11:45nao watu wa Beth-Shemeshi wakauliza, “Ni nani awezaye kusimama mbele za Bwana, huyu Mungu aliye mtakatifu? Sanduku litapanda kwenda kwa nani kutoka hapa?”

216:21 Yos 9:17; 15:9, 60; 1Nya 13:5-6; Amu 18:12Kisha wakatuma wajumbe kwa watu wa Kiriath-Yearimu, wakisema, “Wafilisti wamerudisha Sanduku la Bwana. Shukeni na mlipandishe huko kwenu.”