撒母耳记上 20 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

撒母耳记上 20:1-42

大卫与约拿单

1大卫拉玛拿约逃出来去见约拿单,问他:“我做了什么?犯了什么罪?我什么地方对不起你父亲,他竟追杀我?” 2约拿单答道:“绝无此事,你不会死的!我父亲事无大小都会告诉我的,他不会瞒着我这件事,不会的。” 3大卫发誓说:“你父亲深知你恩待我,他为了不使你伤心,才瞒着你。但我凭永活的耶和华和你的性命起誓,我离死亡仅一步之遥!” 4约拿单说:“你有什么需要?我一定相助。” 5大卫答道:“明天是初一,我本该跟王一起用餐,请让我躲到田间,直到第三天晚上。 6如果你父亲问起我,你就说我恳求你允许我回到故乡伯利恒,因为我全家正在那里献年祭。 7如果你父亲说‘好吧’,仆人就平安无事了。如果他发怒,就表示他决意要杀我。 8请你善待仆人,因你与我在耶和华面前立了盟约。如果我有罪,就请你亲手杀了我,何必把我交给你父亲呢?” 9约拿单答道:“我决不会这样做。我如果知道父亲决意要杀你,怎能不通知你呢?” 10大卫说:“你父亲如果向你发怒,谁来告诉我呢?” 11约拿单说:“我们一起到田野去吧。”于是,二人一起去了田野。

12约拿单大卫说:“愿以色列的上帝耶和华作证,明天或后天这个时侯我就会打探到我父亲的意思,如果他善意待你,我会派人通知你。 13如果他有意杀你,而我却不告诉你让你安然逃走,愿耶和华重重地惩罚我。愿耶和华与你同在,像从前与我父亲同在一样。 14在我有生之年,请你照耶和华的慈爱恩待我,免我一死。 15在我死后,即使耶和华把你所有的仇敌都毁灭了,请你仍旧恩待我的后人。” 16于是,约拿单大卫家立下盟约,说:“如果大卫不守盟约,愿耶和华借着仇敌惩罚他。” 17约拿单因为像爱自己一样爱大卫,便叫他再次起誓。 18约拿单说:“明天是初一,人们会注意到你缺席。 19到了后天,你要赶快去上次出事时躲藏的以色磐石那里。 20我会朝磐石的旁边射三箭,好像射靶子。 21然后,我会叫一个少年把箭拾回来。如果你听到我对他说,‘箭就在你旁边,把箭拾回来。’那就表示你可以回来了,我凭永活的耶和华起誓,你必平安无事。 22但如果我对少年说,‘箭就在你前面。’你就要离开,因为是耶和华要你离开。 23至于我们之间所立的约,耶和华永远为我们作证。”

24于是,大卫就躲到田野。初一到了,扫罗王入席吃饭, 25他照常坐在靠墙的位置,约拿单坐在对面,押尼珥坐在王的身边,大卫的位子空着。 26那一天,扫罗并没有说什么,他以为大卫可能遇到了使自己不洁净的事,不能赴宴。 27可是到了第二天,就是初二,大卫的座位还是空的,扫罗就问儿子约拿单:“耶西的儿子为什么这两天都不来赴宴呢?” 28约拿单答道:“大卫恳求我让他回到伯利恒29因为他家要在城中献祭,他的哥哥要他去。他求我恩准他去见他的哥哥们。所以,他没有来参加王的宴席。”

30扫罗约拿单发怒,对他说:“你这邪逆妇人养的!难道我不知道你是站在耶西的儿子那边吗?你这样做不但自取其辱,也使你母亲蒙羞。 31只要耶西的儿子活在世上,你和你的王位就不得安稳。你派人把他抓到我这里,他非死不可。” 32约拿单问:“为什么要杀他?他做了什么?”

33扫罗气得把矛掷向约拿单,想要杀他。约拿单知道父亲决意要杀大卫34他怒气冲冲地离席,整天不肯进食,因为他看见父亲如此卑劣地对待大卫,心里非常难过。 35第二天早晨,约拿单按照和大卫的约定带着一个少年来到田野。 36约拿单对少年说:“你跑去把我射的箭拾回来。”少年就向前跑去,约拿单把箭射在他前面。 37少年跑到落箭之处的时候,约拿单就大声叫道:“箭不是在你前面吗? 38快快去,不要耽延。”少年连忙把箭拾起来,回到主人那里。 39他不知道主人的用意,只有约拿单大卫知道。 40约拿单把弓箭交给那少年,吩咐他带回城中。 41少年离开以后,大卫就从磐石南面出来,伏地拜了三拜。二人彼此亲吻,抱头痛哭,大卫更是泣不成声。 42约拿单说:“我们已凭耶和华的名起誓,有耶和华在你我和你我的子孙之间永远为我们的盟约作证,你就安心去吧。”大卫便起身离开,约拿单也回城去了。

Kiswahili Contemporary Version

1 Samweli 20:1-42

Daudi Na Yonathani

120:1 1Sam 24:9; 22:23; 23:15; 24:11; 25:29; Za 40:14; 54:3; 63:9; 70:2Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akamwendea Yonathani na kumuuliza, “Kwani nimefanya nini? Kosa langu ni nini? Nimemkosea baba yako kwa jinsi gani, hata kwamba anajaribu kuuondoa uhai wangu?”

220:2 Mwa 44:7; Yos 22:29Yonathani akajibu, “La hasha! Hutakufa! Tazama, baba yangu hafanyi kitu chochote, kikubwa au kidogo, bila kuniambia mimi. Kwa nini anifiche hili? Sivyo ilivyo!”

320:3 Kum 6:13Lakini Daudi akaapa na kusema, “Baba yako anajua kabisa kwamba nimepata kibali mbele yako, naye amesema moyoni mwake, ‘Yonathani sharti asilijue hili, la sivyo atahuzunika.’ Lakini kweli kama Bwana aishivyo na kama uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.”

4Yonathani akamwambia Daudi, “Chochote unachotaka nifanye, nitakufanyia.”

520:5 Hes 10:10; 25:11; 1Sam 9:12; 2Fal 4:23; 1Nya 23:31; 2Nya 2:4; Ezr 3:5; Neh 10:33; Za 81:3; Isa 1:13; Eze 45:17; 46:6; Za 55:13; Yn 8:59Basi Daudi akamwambia, “Angalia, kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo, nami inanipasa kula chakula pamoja na mfalme; lakini niache niende kujificha shambani mpaka kesho kutwa. 620:6 1Sam 17:58; 1:3; 16:4; 9:12Kama baba yako akiona ya kuwa sipo, mwambie, ‘Daudi aliniomba sana ruhusa kuwahi Bethlehemu, mji wake wa nyumbani, kwa sababu dhabihu ya mwaka inafanywa huko kwa ajili ya ukoo wake wote.’ 720:7 1Sam 10:27; 25:17; 18:11; Kum 1:23Kama akisema, ‘Ni vyema sana,’ basi mtumishi wako yu salama. Lakini kama akikasirika, unaweza kuwa na hakika kwamba anakusudia kunidhuru. 820:8 1Sam 18:3; 23:18; 2Sam 14:32; Yos 2:14; Rut 1:8Lakini kwa habari yako wewe, mtende wema mtumishi wako, kwa sababu mmeingia kwenye agano pamoja naye mbele za Bwana. Kama nina hatia, basi niue wewe mwenyewe! Kwa nini unikabidhi kwa baba yako?”

9Yonathani akasema, “La hasha! Kama ningekuwa na kidokezo kidogo kwamba baba yangu amekusudia kukudhuru wewe, je, nisingekuambia?”

10Daudi akamuuliza, “Je, nani atakayeniambia kama baba yako atakujibu kwa ukali?”

11Yonathani akamwambia, “Njoo, twende shambani.” Basi wakaenda huko pamoja.

1220:12 1Sam 19:3; Yos 22:22Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Ninakuahidi kwa jina la Bwana, Mungu wa Israeli, hakika nitamchunguza baba yangu wakati kama huu kesho kutwa! Kama ameweka utaratibu wa kufaa kukuhusu wewe, je, sitakutumia ujumbe na kukufahamisha? 1320:13 Rut 1:17; 1Sam 16:18; 18:12Lakini ikiwa baba yangu amenuia kukudhuru, Bwana na anishughulikie kwa ukali, iwapo sitakufahamisha na kukuaga uende salama. Bwana na awe pamoja nawe kama alivyokuwa pamoja na baba yangu. 14Lakini nitendee wema usiokoma kama ule wa Bwana siku zote za maisha yangu, ili nisije nikauawa, 1520:15 1Sam 24:21; 2Sam 9:7; Mwa 21:23wala usiuondoe wema wako kwa jamaa yangu, hata kama ni wakati ule Bwana atakapokuwa amekatilia mbali kila adui wa Daudi kutoka kwenye uso wa dunia.”

1620:16 1Sam 18:1-3; 25:22-23; Yos 22:23; 2Sam 4:7; 21:8Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi, akisema: “Bwana na awaangamize adui za Daudi.” 1720:17 Yos 9:18; 1Sam 18:3; 2Sam 1:26Naye Yonathani akamtaka Daudi athibitishe tena kiapo chake cha kumpenda, kwa sababu Yonathani alimpenda Daudi kama nafsi yake mwenyewe.

18Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni sikukuu ya Mwezi Mwandamo. Itajulikana kwamba haupo kwa kuwa kiti chako kitakuwa hakina mtu. 1920:19 1Sam 19:2Kesho kutwa, inapokaribia jioni, nenda mahali pale ulipojificha wakati tatizo hili lilipoanza na usubiri karibu na jiwe la Ezeli. 2020:20 2Fal 13:15Nitapiga mishale mitatu kando yake, kama kwamba nilikwenda kulenga shabaha. 2120:21 Kum 6:13; 10:20; Isa 65:16; Yer 4:2Kisha nitamtuma mvulana na kumwambia, ‘Nenda ukaitafute mishale.’ Kama nikimwambia, ‘Tazama mishale iko upande huu wako! Uilete hapa,’ basi uje, kwa sababu hakika kama Bwana aishivyo, wewe ni salama, hakuna hatari. 22Lakini kama nikimwambia huyo mvulana, ‘Angalia, mishale iko mbele yako,’ basi inakupasa uondoke, kwa sababu Bwana amekuruhusu uende zako. 2320:23 Mwa 31:50Kuhusu yale tuliyozungumza wewe na mimi: kumbuka, Bwana ndiye shahidi kati yako wewe na mimi milele.”

2420:24 Hes 10:10; Mit 27:12Basi Daudi akajificha shambani, na sikukuu ya Mwezi Mwandamo ilipowadia, mfalme akaketi ili ale. 2520:25 1Sam 14:50Akaketi mahali pake pa kawaida karibu na ukuta, kuelekeana na Yonathani, naye Abneri akaketi karibu na Mfalme Sauli, lakini kiti cha Daudi kilikuwa wazi. 2620:26 Law 15:5; 1Sam 16:5; Law 6:2; 7:21; Hes 19:16; 1Kor 15:33; 2Kor 6:17; Efe 2:1-3; 5:11Sauli hakusema chochote siku ile kwa kuwa alifikiri, “Kuna kitu cha lazima kimetokea kwa Daudi ambacho kimemfanya najisi asihudhurie karamuni, hakika yeye yu najisi.” 27Lakini siku iliyofuata, siku ya pili ya mwezi, kiti cha Daudi kilikuwa wazi tena. Kisha Sauli akamwambia mwanawe Yonathani, “Kwa nini mwana wa Yese hajaja chakulani jana wala leo?”

28Yonathani akamjibu, “Daudi alinisihi sana nimpe ruhusa aende Bethlehemu. 2920:29 Mwa 8:20Alisema, ‘Niruhusu niende, kwa sababu jamaa yetu wana dhabihu mjini, na ndugu yangu ameniagiza niwepo huko. Kama nimepata kibali mbele yako, niruhusu niende kuona ndugu zangu.’ Hii ndiyo sababu hakuja mezani pa mfalme.”

30Hasira ya Sauli ikawaka dhidi ya Yonathani na kumwambia, “Wewe mwana wa mwanamke mkaidi na mwasi! Je, sijui kuwa umekuwa upande wa mwana wa Yese kwa aibu yako mwenyewe na kwa aibu ya mama yako aliyekuzaa? 3120:31 1Sam 23:17; 24:20Maadamu mwana wa Yese angali anaishi katika dunia hii wewe wala ufalme wako hautasimama. Sasa tuma aitwe umlete kwangu, kwa kuwa ni lazima afe!”

3220:32 1Sam 19:4-5; Mt 23:27; Mwa 31:36; Lk 23:22; Za 25:3; 69:4; Mit 14:25; 24:11; Mt 27:23; Yn 7:31; 15:25Yonathani akamuuliza baba yake, “Kwa nini auawe? Kwani amefanya nini?” 3320:33 1Sam 18:11, 17Lakini Sauli akamtupia Yonathani mkuki wake kwa nguvu ili amuue. Hapo ndipo Yonathani alipotambua kwamba baba yake alikusudia kumuua Daudi.

34Yonathani akainuka kutoka mezani kwa hasira kali. Siku ile ya pili ya mwezi hakula chakula, kwa kuwa alikuwa amehuzunishwa na vitendo vya aibu ambavyo baba yake alikuwa anamtendea Daudi.

35Kesho yake asubuhi Yonathani alikwenda shambani kukutana na Daudi. Alikuwa amefuatana na mvulana mdogo, 36naye Yonathani akamwambia yule mvulana, “Kimbia ukatafute mishale nitakayorusha.” Mvulana alipokuwa akikimbia, akarusha mishale mbele yake. 37Yule mvulana alipofika mahali pale ambapo mshale wa Yonathani ulipokuwa umeanguka, Yonathani akamwita, “Je, mshale hauko mbele yako?” 38Yonathani akampigia kelele, “Harakisha, nenda haraka! Usisimame!” Mvulana akaokota mshale na kurudi kwa bwana wake. 39(Mvulana hakujua chochote juu ya hayo yote; Yonathani na Daudi tu ndio waliojua.) 40Basi Yonathani akampa yule mvulana silaha zake na kumwambia, “Nenda, zirudishe mjini.”

4120:41 Mwa 33:3; Rut 2:10; 1Sam 24:8; 25:23; 2Sam 1:2Baada ya mvulana kwenda, Daudi akainuka kutoka upande wa kusini wa lile jiwe, naye akasujudu uso wake mpaka nchi mara tatu mbele ya Yonathani. Kisha kila mmoja akambusu mwenzake, wakalia pamoja. Lakini Daudi akalia zaidi.

4220:42 1Sam 1:17; Mdo 15:33; Mwa 40:14; 2Sam 1:26; Mit 18:24; Isa 48:1; Mwa 31:50; 1Sam 18:3; 2Sam 9; 1Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa kuwa tumeapiana kiapo cha urafiki kati yetu kwa jina la Bwana, tukisema, ‘Bwana ndiye shahidi kati yako na mimi, na kati ya wazao wako na wazao wangu milele.’ ” Kisha Daudi akaondoka, naye Yonathani akarudi mjini.