历代志上 12 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

历代志上 12:1-40

投奔大卫的人

1大卫洗革拉躲避基士的儿子扫罗的时候,有些勇士来投奔他,帮助他作战。 2他们是弓箭手,左右手都能甩石射箭,来自便雅悯支派,与扫罗同族。 3他们的首领是亚希以谢,其次是约阿施,都是基比亚示玛的儿子,还有亚斯玛威的儿子耶薛毗力,以及比拉迦亚拿突耶户4统领三十位勇士的杰出战士基遍以实买雅,他在三十人中是勇士,另有耶利米雅哈悉约哈难基得拉约撒拔5伊利乌赛耶利摩比亚利雅示玛利雅哈律弗示法提雅6可拉以利加拿耶西亚亚萨列约以谢雅朔班7基多耶罗罕的儿子犹拉西巴第雅

8有些迦得支派的人到旷野的堡垒投奔大卫,他们是能征惯战的勇士,善用盾和矛,貌似雄狮,快如山鹿。 9他们为首的是以薛,其次是俄巴底雅,第三是以利押10第四是弥施玛拿,第五是耶利米11第六是亚太,第七是以利业12第八是约哈难,第九是以利萨巴13第十是耶利米,第十一是末巴奈14这些迦得人都是将领,级别最低的统领一百人,最高的统领一千人。 15一月,约旦河水涨过两岸的时候,他们渡到河对岸,把住在平原的人打得东奔西逃。

16便雅悯支派和犹大支派中也有人到堡垒投奔大卫17大卫出去迎接他们,说:“如果你们是好心来帮助我的,我就与你们结盟,但如果你们把我这无罪之人出卖给敌人,愿我们祖先的上帝鉴察、惩罚你们。” 18当时,上帝的灵感动那三十位勇士的首领亚玛撒,他就说:

大卫啊,我们是你的人!

耶西的儿子啊,我们拥护你!

愿你无比昌盛!

愿帮助你的人也都昌盛!

因为你的上帝帮助你。”

大卫便收留他们,派他们统领他的队伍。

19从前,大卫非利士人一同去攻打扫罗的时候,有些玛拿西人来投奔大卫。但大卫及其部下没有帮助非利士人作战,因为非利士人的首领商议后,害怕大卫拿着非利士人的头颅去归顺他的主人扫罗,便让他们走了。 20大卫洗革拉的时候,玛拿西支派的千夫长押拿约撒拔耶叠米迦勒约撒拔以利户洗勒太都来投奔他。 21他们都是作战英勇的将领,帮助大卫抗击匪徒。 22那时天天有人来投效大卫,以致形成一支大军,好像上帝的军队。

23有些武装好的军兵也到希伯仑投奔大卫,要把扫罗的国权交给大卫,正如耶和华的应许。以下是这些人的数目: 24犹大支派来了手持盾牌和长矛的六千八百名战士; 25西缅支派来了七千一百名英勇的战士; 26利未支派来了四千六百人; 27亚伦家族中的首领耶何耶大和他的三千七百个随从; 28年轻、英勇的撒督和他家族的二十二个将领; 29扫罗的亲族、便雅悯支派中有三千人,大部分便雅悯人仍然效忠扫罗家; 30来自以法莲支派、在本族中有名望的两万零八百个英勇的战士; 31来自玛拿西半个支派、被点名选出来拥立大卫做王的一万八千人; 32来自以萨迦支派、洞悉时事且深明以色列当行之道、统领族人的二百位族长; 33来自西布伦支派、能征善战、拥有各种兵器、训练有素、忠心耿耿的五万人; 34来自拿弗他利支派的一千名将领和三万七千名手持盾牌和长矛的随从; 35来自支派的两万八千六百名能征善战的人; 36来自亚设支派的四万名能征善战的精兵; 37来自约旦河东边的吕便支派、迦得支派和玛拿西半个支派的十二万拥有各种兵器的人。

38以上这些人都是训练有素的勇士,他们诚心诚意到希伯仑拥立大卫以色列王,其余的以色列人也都齐心要立大卫做王。 39他们在那里与大卫一起吃喝了三天,因为他们的亲族为他们预备了食物。 40他们周围的人,远至以萨迦西布伦拿弗他利各支派的人,都用驴、骆驼、骡子和牛驮来面饼、无花果饼、葡萄干、酒和油,又牵来许多牛和羊,以色列充满了欢乐。

Kiswahili Contemporary Version

1 Nyakati 12:1-40

Mashujaa Waungana Na Daudi

112:1 Yos 15:31; 1Sam 27:2-6Hawa ndio watu waliomjia Daudi huko Siklagi, wakati alikuwa amefukuzwa mbele ya Sauli mwana wa Kishi (walikuwa miongoni mwa mashujaa waliomsaidia Daudi vitani, 212:2 Amu 3:15; 20:16; 2Sam 3:19walikuwa na pinde na walikuwa na uwezo wa kupiga mishale au kutupa mawe kwa kombeo wakitumia mkono wa kushoto au wa kulia; hawa walikuwa ndugu zake Sauli kutoka kabila la Benyamini):

312:3 Yos 21:18; 1Nya 11:28Mkuu wao alikuwa Ahiezeri, na wa pili Yoashi, wote wana wa Shemaa Mgibeathi; pia Yezieli na Peleti wana wa Azmawethi; Beraka, Yehu Mwanathothi, 412:4 Yos 15:36; 10:2; 18:21, 25; 1Fal 9:2; Isa 28:21na Ishmaya Mgibeoni, shujaa miongoni mwa wale Thelathini, ambaye alikuwa kiongozi wa wale Thelathini; Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi, Mgederathi, 5Eluzai, Yeremothi, Bealia, Shemaria, Shefatia, Mharufi; 6Elikana, Ishia, Azareli, Yoezeri na Yashobeamu, wana wa Kora; 712:7 Yos 15:58Yoela na Zebadia, wana wa Yerohamu, kutoka Gedori.

812:8 Mwa 30:11; 2Sam 2:18; 17:10; 23:14, 29; 23:20; 1Nya 2:17; Mit 28:1Baadhi ya Wagadi wakajitenga na kujiunga na Daudi katika ngome yake huko jangwani. Walikuwa mashujaa hodari, waliokuwa tayari kwa vita na wenye uwezo wa kutumia ngao na mkuki. Nyuso zao zilikuwa nyuso za simba na walikuwa na wepesi kama paa milimani.

9Ezeri alikuwa mkuu wao,

Obadia alikuwa wa pili katika uongozi, Eliabu wa tatu,

10Mishmana wa nne, Yeremia wa tano,

11Atai wa sita, Elieli wa saba,

12Yohanani wa nane, Elzabadi wa tisa,

13Yeremia wa kumi, na Makbanai wa kumi na moja.

1412:14 Law 26:8; Kum 32:30Hawa Wagadi walikuwa majemadari. Aliyekuwa wa mwisho kuliko wote aliweza kuongoza askari 100, na aliyekuwa na uweza zaidi ya wote aliongoza 1,000. 1512:15 Yos 3:15; Yer 12:5; 49:19Wao ndio walivuka Mto Yordani katika mwezi wa kwanza ukiwa umefurika hadi kwenye kingo zake zote na kusababisha watu wote waliokuwa wanaishi kwenye mabonde kukimbilia mashariki na wengine magharibi.

1612:16 2Sam 3:19Wabenyamini wengine na baadhi ya watu kutoka Yuda pia walikuja kwa Daudi katika ngome yake. 1712:17 Zek 3:2; Yud 9Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mimi mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.”

1812:18 Amu 6:34; 2Nya 15:1; 2Sam 17:25; 1Sam 25:5-6; 1Nya 2:17Kisha Roho akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema:

“Sisi tu watu wako, ee Daudi!

Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese!

Ushindi, naam, ushindi uwe kwako,

pia ushindi kwa wale walio upande wako,

kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.”

Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi.

1912:19 1Sam 29:2-4Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi wakati alikwenda pamoja na Wafilisti, kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu, baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) 2012:20 1Sam 27:6Daudi alipokwenda Siklagi, hawa ndio watu wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu 1,000 katika kabila la Manase. 21Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. 22Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, mpaka akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

Wengine Waungana Na Daudi Huko Hebroni

2312:23 2Sam 2:3-4; 1Nya 10:14; 1Sam 16:1; 1Nya 11:10Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Bwana alivyokuwa amesema:

24watu wa Yuda, wanaochukua ngao na mikuki walikuwa 6,800 wote wakiwa tayari kwa vita.

25Watu wa Simeoni, mashujaa waliokuwa tayari kwa vita walikuwa 7,100.

26Watu wa Lawi walikuwa 4,600, 27pamoja na Yehoyada, kiongozi wa jamaa ya Aroni, aliyekuwa pamoja na watu 3,700, 2812:28 2Sam 8:17; 1Nya 27:17; 1Fal 1:8; 2:25; 1Nya 6:8; Eze 44:15na Sadoki, kijana shujaa na hodari, aliyekuwa pamoja na maafisa ishirini na wawili kutoka jamaa yake.

2912:29 2Sam 3:19; 2:8-9Watu wa Benyamini, ndugu zake Sauli, walikuwa 3,000; wengi wao walikuwa wameendelea kuwa waaminifu kwa Sauli mpaka wakati huo.

30Watu wa Efraimu, mashujaa hodari 20,800, watu waliokuwa maarufu katika koo zao.

31Watu wa nusu ya kabila la Manase, waliotajwa kwa majina ili waje kumweka Daudi kuwa mfalme, watu 18,000.

3212:32 Es 1:13Watu wa Isakari, waliofahamu majira na kujua kile ambacho Israeli inapasa kufanya, walikuwa viongozi 200, pamoja na jamaa zao wote chini ya uongozi wao.

33Watu wa Zabuloni, askari wenye uzoefu mkubwa walioandaliwa tayari kwa vita wakiwa na silaha za kila aina, ili kumsaidia Daudi kwa uaminifu thabiti, walikuwa 50,000.

34Watu wa Naftali, maafisa 1,000, pamoja na watu 37,000 waliochukua ngao na mikuki.

35Watu wa Dani 28,600 waliokuwa tayari kwa vita.

36Watu wa Asheri, askari 40,000 wenye uzoefu mkubwa waliondaliwa kwa ajili ya vita.

37Na pia watu kutoka mashariki ya Yordani, watu wa Reubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, wakiwa na kila aina ya silaha, watu 120,000.

3812:38 2Sam 5:1-3Wote hawa walikuwa watu wapiganaji waliojitolea kutumika katika safu zao. Walikuja Hebroni wakiwa wameamua kikamilifu kumfanya Daudi mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wengine wote walikuwa pia na nia hiyo moja ya kumfanya Daudi kuwa mfalme. 3912:39 2Sam 3:20; Isa 25:6-8Watu hawa wakakaa huko na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa sababu jamaa zao zilikuwa zimewapatia mahitaji yao. 4012:40 2Sam 16:1; 17:29; 1Sam 25:18; 1Nya 29:22Pia, majirani zao hata wale walio mbali hadi Isakari, Zabuloni na Naftali, walikuja wakiwaletea vyakula walivyovibeba kwa punda, ngamia, nyumbu na maksai. Kulikuwepo na wingi wa unga, maandazi ya tini, maandazi ya zabibu kavu, divai, mafuta, ngʼombe na kondoo, kwa maana kulikuwa na furaha katika Israeli.