创世记 44 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

创世记 44:1-34

约瑟试验弟兄

1约瑟吩咐管家说:“给他们的口袋装满粮食,他们能带多少就装多少,把各人的钱放回他们的口袋中, 2再把我的银杯和买粮的钱一起放在最小的兄弟的口袋中。”管家遵命而行。

3清早,他们就牵着驴被送走了。 4他们出城不久,约瑟对管家说:“你快去追他们,追上了就对他们说,‘你们为什么以恶报善? 5为什么偷我主人用来喝酒和占卜的银杯?你们这是作恶!’”

6于是,管家追上他们,按约瑟的话问他们。 7他们回答说:“我主为什么这样说?我们绝不会做这种事。 8你看,我们把上次在口袋里发现的钱都从迦南带回来还你了,又怎么会偷你主人家的金银呢? 9你若在仆人中任何人身上搜到银杯,他就要死!我们也要做我主的奴仆。”

10管家说:“好,就照你们的话做吧!银杯从谁那里搜出来,谁就做我的奴仆,其他人都没有罪。” 11于是,他们急忙把各自的口袋卸到地上打开。 12管家就从最年长的开始搜查,结果在最年幼的便雅悯口袋里搜出了银杯。 13他们伤心地撕裂衣服,把东西放回驴背上,返回城里。

14犹大和他兄弟们回到约瑟家时,约瑟还在那里,他们就俯伏在他面前。 15约瑟对他们说:“你们做的是什么事?难道你们不知道像我这样的人是懂得占卜的吗?” 16犹大说:“我们能对我主说什么呢?我们还有什么话可说呢?我们如何洗脱罪名呢?上帝既然查出你仆人们的罪,我们跟那个手上被发现有银杯的一起做我主的奴仆吧!” 17约瑟回答说:“不!我决不会这样做。从谁那里搜出了银杯,谁就做我的奴仆,其他人平安地回去见你们的父亲吧。”

犹大求情

18犹大近前来对他说:“我主啊,你就像法老一样,求你容仆人说一句话,不要向仆人发怒。 19我主曾经问仆人们是否有父亲和弟兄, 20我们对我主说,‘我们有年迈的老父,他在晚年得了一个儿子,这孩子的哥哥已经死了,他母亲只剩下他这一个儿子,他父亲很疼爱他。’ 21你吩咐仆人们把弟弟带来给你亲眼看看, 22我们对我主说,‘这孩子不能离开他父亲,他若离开,他父亲一定会死。’ 23可是,你说如果仆人们不把最小的弟弟带来,就不得再见你的面。 24我们回到你仆人——我们的父亲那里,把我主的话告诉了他。

25“后来,他又吩咐仆人们回来买些粮, 26我们告诉他,我们不能来,只有我们最小的弟弟同来,我们才能来。否则,我们不能见你的面。 27你仆人——我的父亲就对我们说,‘你们知道,我妻子给我生了两个儿子。 28其中一个离我而去,我想他一定被野兽撕碎了,我再没有见过他。 29要是你们把这个也带走,遇上什么意外的话,你们会使我这白发苍苍的老人凄凄惨惨地下阴间。’

30“我们父亲的命与这孩子的命紧密相连,倘若我没有把这孩子带回到你仆人——我的父亲身边, 31他一看这孩子不在,一定会死。仆人们会使自己白发苍苍的父亲凄凄惨惨地下阴间。 32仆人曾经向父亲担保这孩子的安全,说我若不把这孩子带回他身边,情愿一生担罪。 33现在请准许仆人代替这孩子做我主的奴仆,让他跟他哥哥们回去吧。 34这孩子若不和我一同回去,我如何见我父亲呢?我不愿看到灾难临到我父亲。”

Kiswahili Contemporary Version

Mwanzo 44:1-34

Kikombe Cha Fedha Ndani Ya Gunia

1Kisha Yosefu akampa yule msimamizi wa nyumbani mwake maagizo haya: “Jaza magunia ya watu hawa kiasi cha chakula ambacho wanaweza kuchukua, na uweke fedha ya kila mtu kwenye mdomo wa gunia lake. 244:2 Mwa 44:8Kisha weka kikombe changu kile cha fedha kwenye mdomo wa gunia la yule mdogo wa wote pamoja na fedha zake ambazo angenunulia nafaka yake.” Naye akafanya kama Yosefu alivyosema.

344:3 Amu 19:9Kulipopambazuka, hao watu wakaruhusiwa kuondoka pamoja na punda zao. 4Kabla hawajafika mbali kutoka mjini, Yosefu akamwambia mtumishi wake, “Wafuatilie wale watu mara moja, utakapowakuta, waambie, ‘Kwa nini mmelipiza wema kwa ubaya? 544:5 Mwa 30:27Je, kikombe hiki sicho anachonywea bwana wangu na pia hukitumia kwa kutabiri mambo yajayo? Hili ni jambo ovu mlilolitenda.’ ”

6Alipowafikia, akarudia maneno haya kwao. 744:7 Mwa 18:5Lakini wakamwambia mtumishi, “Kwa nini bwana wangu anasema maneno kama haya? Liwe mbali na watumishi wako wasije wakafanya jambo kama hilo! 844:8 Mwa 42:25Hata hivyo tulikurudishia zile fedha kutoka nchi ya Kanaani ambazo tulizikuta kwenye midomo ya magunia yetu. Hivyo kwa nini tuibe fedha au dhahabu kutoka nyumbani kwa bwana wako? 944:9 Mwa 31:32Ikiwa yeyote miongoni mwa watumishi wako atapatikana nacho, auawe, na sisi wengine tutakuwa watumwa wa bwana wangu.”

10Akajibu, “Vema sana; na iwe kama msemavyo. Yeyote atakayekutwa nacho atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine mtakuwa hamna lawama.”

11Kila mmoja wao akafanya haraka kushusha gunia lake chini na kulifungua. 12Ndipo msimamizi akaendelea kutafuta, akianzia kwa mkubwa wa wote na akaishia kwa mdogo wa wote. Basi kikombe kikapatikana katika gunia la Benyamini. 1344:13 Mwa 37:29Kwa jambo hili, wakararua nguo zao. Ndipo wote wakapakiza mizigo yao juu ya punda zao na kurudi mjini.

1444:14 Mwa 33:3Yosefu alikuwa bado yuko nyumbani mwake wakati Yuda na kaka zake walipoingia, wote wakajitupa chini mbele yake. 1544:15 Za 26:6Yosefu akawaambia, “Ni jambo gani hili mlilolifanya? Hamjui kuwa mtu kama mimi anaweza kufahamu mambo kwa njia ya kutabiri?”

1644:16 Mwa 37:8; Za 26:6Yuda akajibu, “Tutaweza kusema nini kwa bwana wangu? Tutaweza kuzungumza nini? Tutawezaje kuthibitisha kwamba hatuna hatia? Mungu amefunua hatia ya watumishi wako. Sasa sisi tu watumwa wa bwana wangu, sisi wenyewe pamoja na yule aliyepatikana na kikombe.”

17Lakini Yosefu alisema, “Liwe mbali nami kufanya jambo kama hili! Mtu yule tu aliyekutwa na kikombe ndiye atakayekuwa mtumwa wangu. Ninyi wengine, rudini kwa baba yenu kwa amani.”

1844:18 Mwa 18:30Ndipo Yuda akamwendea na kumwambia: “Tafadhali bwana wangu, mruhusu mtumishi wako aseme neno kwa bwana wangu. Usimkasirikie mtumishi wako, ingawa wewe ni sawa na Farao mwenyewe. 19Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, ‘Mnaye baba au ndugu?’ 2044:20 Mwa 37:3; 42:13Nasi tukakujibu, ‘Tunaye baba yetu ambaye ni mzee; pia yupo mwanawe mdogo aliyezaliwa katika uzee wake. Ndugu yake amekufa, na huyu mdogo ndiye mwana pekee kwa mama yake aliyebaki, naye baba yake anampenda.’ 

2144:21 Mwa 42:15“Ndipo ulipowaambia watumishi wako, ‘Mleteni kwangu ili niweze kumwona kwa macho yangu mwenyewe.’ 22Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Kijana hawezi kumwacha baba yake; akimwacha, baba yake atakufa.’ 2344:23 Mwa 43:5Lakini ukawaambia watumishi wako, ‘Ndugu yenu mdogo asiposhuka pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.’ 2444:24 Mwa 43:28Tuliporudi nyumbani kwa mtumwa wako baba yangu, tulimwambia lile bwana wangu alilokuwa amesema.

2544:25 Mwa 42:2“Ndipo baba yetu aliposema, ‘Rudini Misri mkanunue chakula kingine.’ 2644:26 Mwa 43:5Lakini tukamwambia, ‘Hatuwezi kushuka Misri mpaka ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi ndipo tutakapokwenda. Hatutaweza kuuona uso wa yule mtu mpaka ndugu yetu mdogo awe pamoja nasi.’

2744:27 Mwa 46:19“Mtumwa wako baba yangu alituambia, ‘Mnajua mke wangu alinizalia wana wawili. 2844:28 Mwa 37:33Mmojawapo alipotea, nami nikasema, “Hakika ameraruliwa vipande vipande.” Nami sijamwona tangu wakati huo. 2944:29 Mwa 42:38Ikiwa mtaniondolea huyu tena na akapatwa na madhara, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini nikiwa mwenye huzuni.’

3044:30 1Sam 18:1“Hivyo sasa, kama kijana hatakuwa pamoja nasi nitakaporudi kwa mtumishi wako baba yangu, na kama baba yangu, ambaye maisha yake yamefungamanishwa na uhai wa kijana huyu, 31akiona kijana hayupo nasi, atakufa. Watumishi wako watashusha kichwa chenye mvi cha baba yetu kaburini kwa huzuni. 32Mtumwa wako alimhakikishia baba yangu usalama wa kijana. Nikamwambia, ‘Kama sikumrudisha kwako nitakuwa mwenye lawama mbele yako, baba yangu, maisha yangu yote!’

33“Sasa basi, tafadhali mruhusu mtumishi abaki hapa kama mtumwa wa bwana wangu badala ya kijana, naye kijana umruhusu arudi na ndugu zake. 34Ninawezaje kurudi kwa baba yangu kama kijana hatakuwa pamoja nami? La hasha! Usiniache nikaone huzuni ile itakayompata baba yangu.”