列王纪下 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

列王纪下 4:1-44

以利沙帮助穷寡妇

1有一个先知的妻子哀求以利沙说:“你仆人——我丈夫怎样敬畏耶和华,你是知道的。如今他去世了,债主来要把我的两个孩子带去做奴隶。” 2以利沙问她:“我该怎样帮你呢?告诉我,你家里有什么?”妇人答道:“婢女家什么也没有,只有一瓶油。” 3以利沙说:“你去向所有邻居借空器皿,要尽量多借一些。 4然后回家关上门,你和你儿子在屋里把那瓶油倒在所有借来的器皿中,装满的放在一边。” 5于是,妇人辞别以利沙,回去后把自己和儿子关在屋里,儿子递给她器皿,她就倒油。 6器皿都装满了,她对儿子说:“再拿个器皿给我。”儿子说:“已经没有了。”这时,油止住了。 7妇人将经过告诉上帝的仆人,上帝的仆人对她说:“你去把油卖了还债,你们母子可以用剩下的钱度日。”

以利沙和书念妇人

8一天,以利沙路过书念,那里一位富有的妇人挽留他吃饭。此后以利沙每次路过那里,总到她家里吃饭。 9那妇人对丈夫说:“我看常路过我们这里的这位是上帝圣洁的仆人。 10不如我们在房顶上给他盖一间小屋,里面放床、桌子、椅子和灯。这样,他来我们家时,可以在那里休息。”

11一天,以利沙又到了那里,便在那间小屋里休息。 12以利沙吩咐仆人基哈西去请书念的妇人。他就请来妇人,妇人站在以利沙面前。 13以利沙吩咐基哈西说:“你对她说,‘你为我们费了不少心,我们该为你做些什么呢?要不要我们在王或元帅面前为你说些好话呢?’”她答道:“我在本族中安居无事。” 14以利沙基哈西:“我们能为她做什么呢?”基哈西说:“她没有儿子,丈夫也已经老了。” 15以利沙说:“你再去请她来。”她来了,站在门口。 16以利沙对她说:“明年这时候,你必抱一个儿子。”她说:“上帝的仆人,我主啊,不要骗婢女。” 17那妇人果然怀了孕,在第二年的那时候生了一个儿子,应验了以利沙对她说的话。

18孩子渐渐长大。一天,他到收割的人那里找他父亲。 19突然,他对他父亲喊道:“我的头啊!我的头啊!”他父亲见状立刻吩咐仆人抱他到他母亲那里。 20仆人把他抱起来,送到他母亲那里。孩子坐在母亲的膝上,到中午就死了。 21他母亲上楼把他放在上帝仆人的床上,关上门出来。 22她叫来丈夫,对他说:“请你预备一个仆人和一头驴,我好赶快去见上帝的仆人,然后返回来。” 23她丈夫说:“今天不是朔日4:23 “朔日”即每月初一。,也不是安息日,你为什么要去见他?”妇人说:“放心吧。” 24她骑上驴,对仆人说:“快走吧!我不吩咐你,就不要慢下来。”

25她就去迦密山见上帝的仆人。上帝的仆人远远望见她,就对仆人基哈西说:“你看,书念的妇人来了! 26你跑去迎接她,问问她和她的丈夫与孩子都好吗。”

妇人对以利沙的仆人说:“一切都好。”

27可是,她上山见到上帝的仆人后,就抱住他的脚。基哈西想要推开她,但上帝的仆人说:“由她吧!因为她心里非常痛苦。耶和华没有告诉我发生了什么事。” 28妇人说:“我何尝向我主求过儿子呢?我不是对你说不要骗我吗?” 29以利沙吩咐基哈西:“你要束上腰带,拿着我的杖去她家。路上不论遇见谁,都不要问候他。有人问候你,也不要作答。去把我的杖放在孩子脸上。” 30孩子的母亲说:“我凭永活的耶和华和你的性命起誓,你若不同去,我决不离开你。”于是,以利沙跟她同去。 31基哈西先赶到,把杖放在孩子脸上,可是孩子一点动静也没有。他就回去找以利沙,路上碰见他,便说:“孩子还没醒过来。”

32以利沙进了屋子,看见孩子死了,躺在床上, 33就关上门,向耶和华祈祷。 34祷告后,他上床伏在孩子身上,口对口,眼对眼,手对手,孩子的身体渐渐变暖了。 35然后,以利沙起来在房内来回走了一趟,又上床伏在孩子身上。孩子打了七个喷嚏,便睁开了眼睛。 36以利沙基哈西请那妇人来。他便请来妇人,以利沙对妇人说:“把你儿子抱走吧。” 37妇人进来,在以利沙脚前下拜,然后抱起儿子出去了。

用面粉解毒

38以利沙回到吉甲,那里正遭遇饥荒。一群先知坐在他面前,他吩咐仆人把一口大锅放在火上给他们煮汤。 39有个先知到田间摘野菜,看见一棵野瓜藤,便摘了一兜野瓜回来,切碎了放进锅里,却不知道那是什么瓜。 40汤煮好后倒出来给众人喝,他们刚喝了一点,就叫道:“上帝的仆人啊,锅里有剧毒!”他们都不敢喝了。 41以利沙说:“拿点面粉来。”他把面粉撒在锅里,说:“倒出来给众人喝吧。”于是,锅里没有毒了。

用二十个饼喂饱百人

42巴力·沙利沙来了一个人,他带了二十个用初熟大麦做的饼和一些麦穗送给上帝的仆人。上帝的仆人说:“分给众人吃吧。” 43仆人说:“这怎么够一百人吃呢?”以利沙说:“你只管分给众人吃。因为耶和华说,‘众人都能吃饱,并且还会剩下。’” 44于是,仆人将食物摆在众人面前,他们都吃饱了,果然还有剩余,正如耶和华所言。

Kiswahili Contemporary Version

2 Wafalme 4:1-44

Mafuta Ya Mjane

14:1 Law 25:39-43; Neh 5:3-5Mke wa mmoja wa wana wa manabii akamlilia Elisha, akamwambia, “Mtumishi wako, mume wangu, amekufa, nawe unajua alikuwa anamcha Bwana. Lakini sasa yule anayemdai anakuja kuchukua wanangu wawili kama watumwa wake.”

24:2 1Fal 17:12Elisha akamjibu, “Nitawezaje kukusaidia? Niambie, una nini ndani ya nyumba yako?”

Akasema, “Mtumishi wako hana kitu chochote kabisa, isipokuwa mafuta kidogo.”

3Elisha akasema, “Zunguka kwa majirani zako wote ukaombe vyombo vitupu. Usiombe vichache. 4Kisha ingia ndani na ujifungie mlango, wewe na wanao. Mimina mafuta kwenye vyombo vyote, na kila kimoja kinapojaa, kiweke kando.”

5Yule mjane akaondoka na kujifungia ndani, yeye na wanawe. Wao wakamletea vyombo, naye akaendelea kumimina mafuta. 6Vyombo vyote vilipojaa, akamwambia mwanawe, “Niletee chombo kingine.”

Lakini mwanawe akajibu, “Hakuna chombo kingine kilichobaki.” Basi mafuta yakakoma kutiririka.

74:7 1Fal 12:22Yule mwanamke akaenda akamwambia yule mtu wa Mungu, naye mtu wa Mungu akasema, “Nenda ukayauze hayo mafuta ulipe madeni yako. Wewe na wanao mnaweza kuishi kwa kile kinachosalia.”

Mwana Wa Mshunami Afufuliwa

84:8 Yos 19:18Siku moja Elisha akaenda Shunemu. Huko kulikuwa na mwanamke mmoja mwenye cheo, ambaye alimsisitiza Elisha aje kula chakula. Kwa hiyo kila mara alipitia pale, akaingia humo ili ale. 9Akamwambia mumewe, “Ninajua kwamba huyu mtu ambaye anakuja kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. 104:10 Mt 10:41; Rum 12:13Tutengeneze chumba kidogo juu darini na tuweke ndani yake kitanda na meza, kiti na taa kwa ajili yake. Kisha anaweza kukaa humo kila mara akija kwetu.”

11Siku moja Elisha alipofika, akapanda chumbani kwake na kulala humo. 124:12 2Fal 8:1Akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Mwite huyo Mshunami.” Hivyo akamwita, naye akaja akasimama mbele yake. 13Elisha akamwambia mtumishi wake, “Mwambie huyu mwanamke, ‘Umetaabika sana kwa ajili yetu. Sasa utendewe nini? Je, tunaweza kuzungumza na mfalme au jemadari wa jeshi kwa niaba yako?’ ”

Akajibu, “Mimi ninaishi kwangu miongoni mwa watu wangu.”

14Elisha akamwambia mtumishi wake, “Je, ni nini kinachoweza kufanyika kwa ajili yake?”

Gehazi akasema, “Hakika, hana mwana, na mume wake ni mzee.”

15Ndipo Elisha akasema, “Mwite huyo mwanamke.” Kwa hiyo akamwita, naye akaja akasimama mlangoni. 164:16 Mwa 18:10Elisha akamwambia, “Mwaka ujao, wakati kama huu utabeba mwana mikononi mwako.”

Yule mama akapinga, akasema, “La hasha, bwana wangu, usimpotoshe mtumishi wako, ee mtu wa Mungu!”

17Lakini yule mwanamke akapata mimba, na mwaka uliofuata wakati kama ule ule akamzaa mwana, kama vile Elisha alivyokuwa amemwambia.

184:18 Rut 2:3Mtoto akakua, naye siku moja akamwendea baba yake, ambaye alikuwa pamoja na wavunaji. 19Akamwambia baba yake, “Kichwa changu! Kichwa changu!”

Baba yake akamwambia mtumishi, “Mchukue umpeleke kwa mama yake.” 20Baada ya mtumishi kumbeba na kumpeleka kwa mama yake, mtoto akaketi mapajani mwa mama yake mpaka adhuhuri, kisha akafa. 214:21 2Fal 4:32Mama akampandisha na kumlaza juu ya kitanda cha yule mtu wa Mungu, kisha akafunga mlango, akatoka nje.

22Akamwita mume wake na kusema, “Tafadhali mtume mmoja miongoni mwa mtumishi pamoja na punda ili niweze kwenda kwa mtu wa Mungu haraka na kurudi.”

234:23 Hes 10:10; 1Nya 23:31Mume wake akamuuliza, “Kwa nini uende kwake leo? Leo si mwandamo wa mwezi, wala si Sabato.”

Mwanamke akasema, “Yote ni sawa.”

24Akatandika punda na kumwambia mtumishi wake, “Mwongoze huyo punda. Usinipunguzie mwendo mpaka nikuambie.” 254:25 1Fal 18:20Kwa hiyo akaenda na kumfikia huyo mtu wa Mungu katika Mlima Karmeli.

Alipomwona kwa mbali, huyo mtu wa Mungu akamwambia mtumishi wake Gehazi, “Tazama, yule Mshunami! 26Kimbia ukamlaki, umuulize, ‘Je, wewe hujambo? Mume wako hajambo? Mtoto wako ni mzima?’ ”

Akasema, “Kila kitu ni sawasawa.”

274:27 1Sam 1:15Alipomfikia huyo mtu wa Mungu pale mlimani, akashika miguu yake. Gehazi akaja ili amwondoe, lakini yule mtu wa Mungu akasema, “Mwache! Yuko katika uchungu mkubwa, lakini Bwana amenificha jambo hili na hajaniambia kwa nini.”

28Yule mwanamke akasema, “Je, bwana wangu, mimi nilikuomba mwana? Je, sikukuambia, ‘Usiamshe matumaini yangu’?”

294:29 1Fal 18:46; Kut 4:2Elisha akamwambia Gehazi, “Jikaze viuno, chukua fimbo yangu mkononi mwako na ukimbie. Ikiwa utakutana na mtu yeyote, usimsalimie, na mtu yeyote akikusalimu, usimjibu. Ilaze fimbo yangu juu ya uso wa mtoto.”

30Lakini mama mtoto akasema, “Hakika kama Bwana aishivyo na wewe uishivyo, sitakuacha.” Kwa hiyo Elisha akainuka, akafuatana naye.

31Gehazi akatangulia mbele na kuilaza fimbo juu ya uso wa mtoto, lakini hapakuwa na sauti wala itikio. Hivyo Gehazi akarudi kukutana na Elisha, na kumwambia, “Mtoto hajaamka.”

32Elisha alipofika kwenye ile nyumba, mtoto alikuwa amelala juu ya kitanda chake angali amekufa. 334:33 1Fal 17:20; Mt 6:6Akaingia ndani, akajifungia yeye na yule mtoto, akamwomba Bwana. 344:34 1Fal 17:21; Mdo 20:10Kisha akapanda kitandani, akalala juu ya yule mtoto, mdomo wake juu ya mdomo wa mtoto, macho yake juu ya macho ya mtoto, mikono yake juu ya mikono ya mtoto. Naye alipojinyoosha juu yake, mwili wa mtoto ukapata joto. 354:35 Yos 6:15; 2Fal 8:5Elisha akajiondoa juu yake na kuanza kutembeatembea ndani ya chumba, kisha akarudi tena kitandani na kujinyoosha tena juu ya mtoto mara nyingine. Mtoto akapiga chafya mara saba, akafungua macho yake.

364:36 Ebr 11:35Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite huyo Mshunami.” Naye akafanya hivyo. Yule Mshunami alipokuja, Elisha akasema, “Mchukue mwanao.” 37Akaingia ndani, akaanguka miguuni pa Elisha na kusujudu hadi nchi. Kisha akamchukua mwanawe na kutoka nje.

Mauti Ndani Ya Chungu

384:38 2Fal 2:1; 8:1Elisha akarudi Gilgali, nako huko kulikuwa na njaa katika eneo lile. Wakati wana wa kundi la manabii walipokuwa wanakutana naye, akamwambia mtumishi wake, “Teleka chungu kikubwa jikoni uwapikie manabii.”

39Mmoja wao akatoka kwenda mashambani kuchuma mboga na akapata mtango mwitu. Akachuma matango na kujaza nguo yake aliyoikunja ili kubebea. Aliporudi, akayakatakata na kuyatumbukiza ndani ya chungu, ingawa hakuna aliyejua ni nini. 40Mchuzi ukagawiwa watu, lakini walipoanza kula, wakalia, “Ee mtu wa Mungu, kuna mauti ndani ya chungu.” Nao hawakuweza kula.

414:41 Kut 15:25; 2Fal 2:21Elisha akasema, “Leteni unga.” Akauweka ndani ya chungu na kusema, “Wagawie watu ili wale.” Wala hapakuwa na kitu chochote chenye madhara ndani ya chungu.

Watu Mia Wanalishwa

424:42 1Sam 9:4; Mt 14:17Akaja mtu kutoka Baal-Shalisha, akimletea mtu wa Mungu mikate ishirini ya shayiri iliyookwa kutokana na nafaka ya kwanza, pamoja na masuke ya nafaka mpya. Elisha akasema, “Wape watu ili wale.”

434:43 Lk 9:13; Yn 6:12Mtumishi wake akamuuliza, “Nitawezaje kuandaa hii mbele ya watu mia?”

Lakini Elisha akajibu, “Wape watu ili wale. Kwa maana hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Watakula na kusaza.’ ” 44Basi akaiandaa mbele yao ile mikate, wakala na baadhi yake wakasaza, sawasawa na neno la Bwana.