使徒行传 20 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

使徒行传 20:1-38

保罗再访马其顿和希腊

1这场风波平息后,保罗召集众门徒勉励一番后,便辞别他们去了马其顿2他走遍那一带,用许多话鼓励当地的门徒。之后,他又去希腊3在那里逗留了三个月。保罗正要乘船去叙利亚时,听闻犹太人计划要害他,就决定经马其顿回去。 4同他到亚细亚去的人有庇哩亚毕罗斯的儿子所巴特帖撒罗尼迦亚里达古西公都,还有特庇该犹提摩太亚细亚推基古特罗非摩5他们先到特罗亚等候我们。 6除酵节过后,我们从腓立比启航,五天后在特罗亚和他们会合,大家同住了七天。

犹推古死而复活

7七日的第一日20:7 照犹太人的算法,太阳下山后为一日的开始,基督徒又以礼拜天为一周之始,所以七日的第一日很有可能是礼拜六晚上。,我们聚会掰饼,保罗因为次日要离开,就向他们讲道,直到半夜。 8我们聚会的楼上灯火通明。 9有个名叫犹推古的青年坐在窗台上听道。保罗讲了许久,犹推古不胜困倦睡着了,竟从三楼掉了下去。别人将他抱起来时,他已经死了。 10保罗下去伏在他身上,抱着他对众人说:“不要惊慌,他还活着!” 11保罗说完就回到楼上,与大家一同掰饼、吃了,又谈了很久,直到天亮才离去。 12大家把活过来的犹推古送回家,都大得安慰。

保罗告别以弗所的众长老

13我们照保罗的吩咐先乘船到亚朔预备在那里接他,他打算由陆路步行过去。 14他到了亚朔,我们接他上船,一同前往米推利尼15我们从米推利尼启航,第二天到了基阿附近,第三天到达撒摩,第四天在米利都停泊。 16保罗急于赶回耶路撒冷,希望在五旬节前赶到,所以决定越过以弗所,免得在亚细亚境内耽误太久。

17保罗米利都派人到以弗所请教会的长老前来与他相会。 18他们都来了,保罗说:“各位,自从我踏进亚细亚那天起,在你们当中为人如何,你们都很清楚。 19我含着眼泪谦卑地事奉主,又遭到犹太人的谋害,历尽艰辛。 20你们也知道,凡是对你们有益的事,我没有避而不宣,我总是在公开场合和各人家中教导你们。 21我劝犹太人和希腊人都要悔改,归向上帝,信靠主耶稣基督。 22现在,我在圣灵的催促下前往耶路撒冷,不知道在那里会发生什么事, 23只知道圣灵在各城指示我,前面必有监禁和苦难等着我。 24不过,只要能跑完我当跑的路程,完成主耶稣交托给我的使命——为上帝充满恩典的福音做见证,就是牺牲性命,我也在所不惜。

25“我一向在你们中间传扬上帝的国,如今我知道,以后你们再也见不到我的面了。 26所以今天我向你们声明,将来你们有谁灭亡,与我无关。 27因为上帝的整个计划,我没有向你们避而不宣。 28你们要为自己,也要为教会的群羊警醒,因为圣灵已经任命你们做群羊的监督,牧养上帝的教会。教会是祂用自己的血赎回来的。 29我知道,在我离开以后,一定会有凶恶的豺狼闯进你们中间,残害羊群。 30就是你们中间也会有人起来歪曲真理,引诱门徒跟随他们。 31所以你们一定要警醒,牢记这三年来我怎样昼夜不住地流着泪劝诫你们。

32“现在,我把你们交托给上帝和祂充满恩典的道,这道能造就你们,使你们与一切得以圣洁的人同得产业。 33我从未贪图别人的金银和衣服, 34你们都知道,我亲手做工养活自己和同工。 35我凡事以身作则,教导你们勤奋工作,帮助软弱的人,并牢记主耶稣的话,‘施比受更有福。’”

36保罗说完这番话,就和大家一同跪下祷告。 37众人都哭了,抱着保罗与他亲吻, 38最使他们伤心的就是他说“你们再也见不到我的面了”。随后,众人送他上了船。

Kiswahili Contemporary Version

Matendo 20:1-38

Paulo Apita Makedonia Na Uyunani

120:1 Mdo 11:26; 16:9Baada ya zile ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia. 2Alipita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo. Ndipo hatimaye akawasili Uyunani, 320:3 2Kor 11:26; 1The 2:15-16; Mdo 16:9ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya bahari kwenda Shamu, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yake, aliamua kurudi kupitia njia ya Makedonia. 420:4 Mdo 19:29; 17:19-29; 16:1; Efe 6:21; 2Tim 4:12; Mdo 21:29; 2Tim 4:20Paulo alikuwa amefuatana na Sopatro mwana wa Piro, Mberoya, Aristarko na Sekundo kutoka Thesalonike na Gayo, mtu wa Derbe, Timotheo pamoja na Tikiko na Trofimo kutoka sehemu ya Asia. 520:5 Mdo 16:10; 16:8Hawa watu walitutangulia wakaenda kutungojea Troa. 620:6 Mdo 16:2; 18:8Lakini sisi tukasafiri kwa njia ya bahari kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba.

Eutiko Afufuliwa Huko Troa

720:7 1Kor 16:2; Ufu 1:10Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka usiku wa manane. 820:8 Mdo 1:13Kwenye chumba cha ghorofani walimokuwa wamekutania kulikuwa na taa nyingi. 9Kijana mmoja jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akihubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa. 1020:10 1Fal 17:21; 2Fal 4:34; Mt 9:23; 24Paulo akashuka chini, akajitupa juu yake na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, uzima wake bado umo ndani yake.” 1120:11 Mdo 20:7; Mt 14:19Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea mpaka mapambazuko, akaondoka. 12Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.

Paulo Awaaga Wazee Wa Efeso

13Tukatangulia melini tukasafiri mpaka Aso ambako tungempakia Paulo. Alikuwa amepanga hivyo kwa maana alitaka kufika kwa miguu. 14Alipotukuta huko Aso, tulimpakia melini, tukasafiri wote mpaka Mitilene. 1520:15 2Tim 4:20Kutoka huko tuliendelea kwa njia ya bahari, na kesho yake tukafika mahali panapokabili Kio. Siku iliyofuata tukavuka kwenda Samo, na kesho yake tukawasili Mileto. 1620:16 Mdo 18:19; 19:21; 2:1; 1Kor 16:8Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko sehemu za Asia, kwa sababu alikuwa anatamani kama ikiwezekana kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.

1720:17 Mdo 11:30Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa waje wakutane naye. 1820:18 Mdo 18:19, 21; 19:1-4Walipofika akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua jinsi nilivyoishi katikati yenu muda wote tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia. 19Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi nikivumilia taabu na mapingamizi yaliyonipata kutokana na hila za Wayahudi. 2020:20 Za 40:10Mnajua kwamba sikusita kuhubiri jambo lolote ambalo lingekuwa la kuwafaa ninyi, lakini nilifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba. 2120:21 Mdo 18:5; 2:38; Efe 1:15; Kol 2:5Nimewashuhudia Wayahudi na Wayunani kwamba inawapasa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.

2220:22 Mdo 19:21“Nami sasa nimesukumwa na Roho, ninakwenda Yerusalemu wala sijui ni nini kitakachonipata huko. 2320:23 Mdo 21:4; 9:16Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja. 2420:24 Mdo 21:13; 2Kor 4:1; Gal 1:1; Tit 1:3Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Yesu aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.

2520:25 Mt 4:23; Mdo 20:38; Rum 15:23“Nami sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu ambaye nimemhubiria Ufalme wa Mungu katika kwenda kwangu huku na huko, atakayeniona uso tena. 2620:26 Mdo 18:6Kwa hiyo nawatangazia leo, sina hatia ya damu ya mtu awaye yote. 27Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu. 2820:28 1Pet 5:2Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe. 2920:29 Mt 7:15Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi. 3020:30 Mdo 11:26Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate. 3120:31 Mdo 19:10Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.

3220:32 Mdo 14:23; Mt 25:34; Ebr 9:15; Mdo 26:18“Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa. 3320:33 1Sam 12:3; 1The 2:5Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote. 3420:34 Mdo 18:3Ninyi wenyewe mnajua kwamba mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami. 3520:35 Rum 15:1; 1Kor 9:12; 2Kor 11:9, 12; 12:13; Efe 4:28; 1The 4:11; 2The 3:8Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’ ”

3620:36 Lk 22:41; Mdo 9:40Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba. 3720:37 Lk 15:20Wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kumbusu, 38Kilichowahuzunisha zaidi ni kwa sababu ya yale maneno aliyosema kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Wakaenda naye mpaka kwenye meli.