以赛亚书 61 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以赛亚书 61:1-11

大喜的讯息

1主耶和华的灵在我身上,因为耶和华膏立了我,

让我传福音给贫穷的人,

差遣我医治伤心的人,

宣告被掳的人得释放、

被囚的人得自由;

2宣告耶和华的恩年和我们上帝报仇的日子,

安慰一切悲哀的人;

3以华冠取代锡安哀伤者头上的灰尘,

以喜乐的膏油取代他们的哀伤,

以颂赞的外袍取代他们的灰心。

他们将被称为耶和华所栽种的公义橡树,

以彰显祂的荣耀。

4他们必重修古老的荒场,

修复久已毁坏之地,

重建历代荒废的城邑。

5异乡客要为你们牧放羊群,

外族人要为你们耕种田地、

照料葡萄园。

6你们要被称为耶和华的祭司,

我们上帝的臣仆。

你们必享用各国的财富,

夸耀自己拥有他们的荣华。

7你们曾经蒙受耻辱,

如今将得到双倍的福分;

你们曾经遭受屈辱,

如今将因得到产业而快乐。

你们将在自己的土地上得到双倍的福分,

享受永远的快乐。

8“因为我耶和华喜爱公正,

憎恶抢劫之罪。

我必凭信实赏赐我的子民,

与他们立永远的约。

9他们的后代必享誉列国,

子孙必名闻万邦,

看见的人都承认他们是蒙耶和华赐福之民。”

10我因耶和华而无比喜乐,

因我的上帝而心里快乐,

因为祂给我穿上救恩的衣服、

披上公义的袍子,

使我像戴上华冠的新郎,

又像戴上饰物的新娘。

11大地怎样使嫩苗长出,

园子怎样使种子发芽,

主耶和华必照样使公义与颂赞在万民中滋长。

Kiswahili Contemporary Version

Isaya 61:1-11

Mwaka Wa Upendeleo Wa Bwana

161:1 Isa 11:2; Mdo 4:26; Lk 4:18-19; Zek 9:12; 2Kor 3:17; Isa 50:4; Dan 9:24-26; Ay 5:16Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu,

kwa sababu Bwana amenitia mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

261:2 Isa 49:8; Mal 4:1-3; Mt 5:4; Isa 1:24; Lk 4:18-19; Ay 5:1; Lk 6:21kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote waombolezao,

361:3 Isa 60:20-21; 3:23; Ay 2:8; Rut 3:3; Ebr 1:9; Yer 31:13; Za 92:12-13; Mt 15:13na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando la Bwana,

ili kuonyesha utukufu wake.

461:4 Amo 9:14; Yn 15:8; Zek 1:16-17; Isa 44:26; Eze 36:33Watajenga upya magofu ya zamani

na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;

watafanya upya miji iliyoharibiwa,

iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.

561:5 Isa 14:1-2; Eze 36:33; Isa 56:6Wageni watayachunga makundi yenu,

wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,

na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.

661:6 Kut 19:6; Kum 33:19; 1Pet 2:5; Isa 60:1Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana,

mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.

Mtakula utajiri wa mataifa,

nanyi katika utajiri wao mtajisifu.

761:7 Kum 21:17; Zek 9:12; Isa 29:22; 41:11; 60:21; Za 126:5; Isa 25:9Badala ya aibu yao

watu wangu watapokea sehemu maradufu,

na badala ya fedheha

watafurahia katika urithi wao;

hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,

nayo furaha ya milele itakuwa yao.

861:8 Mwa 9:16; Isa 1:17; 55:3; 5:16; Za 11:7; Ebr 13:20; Isa 42:6“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki,

na ninachukia unyangʼanyi na uovu.

Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao

na kufanya agano la milele nao.

961:9 Isa 43:5; 48:19; Mwa 12:2; Kum 28:3-12Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,

na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.

Wale wote watakaowaona watatambua

kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.”

1061:10 Hab 3:18; Ay 27:6; Isa 49:18; Ufu 21:2; Za 2:11; Isa 7:13; Lk 1:47; Ufu 19:8Ninafurahia sana katika Bwana,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

1161:11 Za 85:11; Isa 45:8; Mwa 47:23; Isa 58:11Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota,

na bustani isababishavyo mbegu kuota,

ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa

zichipuke mbele ya mataifa yote.