以斯帖记 4 – CCB & NEN

Chinese Contemporary Bible 2022 (Simplified)

以斯帖记 4:1-17

末底改求以斯帖帮忙

1末底改得知这事,就撕裂衣服,披上麻衣,头蒙灰尘,在城中行走,放声痛哭, 2一直走到宫门前才停住,因为穿麻衣的不可进宫门。 3王的命令和谕旨传到各省各地,犹太人极其悲伤,他们禁食、哭泣、哀号,许多人身披麻衣躺在灰中。

4以斯帖王后的宫女和太监把这事禀告她,她非常难过,便为末底改送去衣服,让他换下麻衣,他却不肯接受。 5于是,以斯帖把王派来服侍她的一个名叫哈他革的太监召来,叫他去见末底改,查明事情的原委。 6哈他革就到宫门前的广场见末底改7末底改便将自己的遭遇,以及哈曼为灭绝犹太人而许诺捐入国库的银子数目都告诉了他。 8末底改还把一份在书珊城颁布的要消灭犹太人的谕旨抄本交给哈他革,让他给以斯帖看并说明原委,嘱咐她去见王,为自己的同胞向王求情。 9哈他革回去把末底改的话告诉以斯帖10以斯帖便吩咐哈他革回复末底改说: 11“王的所有臣仆和各省人民都知道有一条法令,不论男女,未蒙宣召擅入内院去见王的必被处死,除非王向他伸出金杖,他才能活命。现在我已有三十天未蒙王召见了。”

12末底改听到以斯帖捎来的话后, 13便回复她说:“你别以为在宫里就比其他犹太人安全。 14如果你此时沉默不语,犹太人必从别处得解脱,蒙拯救,但你和你父亲一家必灭亡。谁知道你得了王后之位不是为了今日之时呢?”

15以斯帖派人回复末底改说: 16“你去召集书珊城所有的犹太人为我禁食,三天三夜不吃不喝,我和我的宫女也要这样禁食。然后,我要违例去见王,我若死就死吧!”

17于是,末底改便去照以斯帖的一切吩咐行事。

Kiswahili Contemporary Version

Esta 4:1-17

Mordekai Amshawishi Esta Kusaidia

14:1 Eze 27:30-31; Za 30:11Mordekai alipojua yote yaliyokwisha kufanyika, alirarua mavazi yake na kuvaa nguo za magunia na kujipaka majivu, akaenda mjini, akiomboleza kwa sauti na kwa uchungu. 2Alikwenda akasimama nje ya lango la mfalme, kwa sababu hakuna yeyote aliyeruhusiwa kuingia akiwa amevaa nguo za magunia. 3Katika kila jimbo ambapo amri na agizo la mfalme lilifika, kulikuwa na maombolezo makuu miongoni mwa Wayahudi pamoja na kufunga, kulia na kuomboleza. Watu wengi wakalala juu ya nguo za magunia na majivu.

4Wajakazi wa Esta na matowashi walipokuja na kumwambia kuhusu Mordekai, alipatwa na huzuni kuu. Alimtumia nguo avae badala ya nguo za magunia, lakini Mordekai hakuzikubali. 5Ndipo Esta akamwita Hathaki, mmojawapo wa matowashi wa mfalme ambaye alikuwa amewekwa kumhudumia Esta, akamwagiza kutafuta ni nini kilikuwa kikimtaabisha Mordekai na ni kwa nini.

6Basi Hathaki alitoka nje kumwendea Mordekai kwenye uwanja ulio wazi wa mji mbele ya lango la mfalme. 74:7 Es 7:4Mordekai akamwambia kila kitu ambacho kimempata, pamoja na hesabu kamili ya fedha ambazo Hamani aliahidi kulipa katika hazina ya mfalme kwa ajili ya maangamizi ya Wayahudi. 8Akampa nakala ya andiko la amri kwa ajili ya maangamizi yao, lililokuwa limechapishwa huko Shushani, kumwonyesha Esta na kumwelezea. Mordekai akamwambia towashi amshawishi Esta kwenda mbele ya mfalme kuomba rehema na kumsihi kwa ajili ya watu wake.

9Hathaki akarudi kwa Esta na kumwarifu alilolisema Mordekai. 10Kisha Esta akamwamuru Hathaki amweleze Mordekai, 114:11 Dan 2:9; Za 125:3“Maafisa wote wa mfalme na watu wa majimbo ya ufalme wanajua kuwa mwanaume au mwanamke yeyote ambaye ataingia kumwona mfalme katika ua wa ndani bila kuitwa, mfalme ana sheria moja tu: Atauawa. Njia pekee kinyume na hili ni mfalme kumnyooshea fimbo ya dhahabu ili aishi. Lakini siku thelathini zimepita tangu nilipoitwa kwenda kwa mfalme.”

12Wakati Mordekai aliarifiwa maneno ya Esta, 13Mordekai alirudisha jibu hili: “Usifikiri kwamba kwa sababu uko katika nyumba ya mfalme wewe pekee katika Wayahudi wote utapona. 144:14 Ay 34:29; Mhu 3:7; Amo 5:13Kwa kuwa kama utakaa kimya wakati huu, msaada na ukombozi kwa Wayahudi utatoka mahali pengine, lakini wewe na jamaa ya baba yako mtaangamia. Nani ajuaye kwamba hukuja kwenye nafasi ya mamlaka kwa ajili ya wakati kama huu?”

15Kisha Esta alituma jibu hili kwa Mordekai: 164:16 2Nya 20:3; Mwa 43:14“Nenda, kusanya pamoja Wayahudi wote walioko Shushani, nanyi mfunge kwa ajili yangu. Msile wala kunywa kwa siku tatu, usiku na mchana. Mimi na wajakazi wangu tutafunga kama mnavyofanya. Baada ya kufanyika hili, nitakwenda kwa mfalme, hata ingawa ni kinyume cha sheria. Ikiwa ni kuangamia na niangamie.”

17Kwa hiyo Mordekai alikwenda zake na kutekeleza maagizo yote ya Esta.