Zekaria 12:1-14, Zekaria 13:1-9, Zekaria 14:1-21 NEN

Zekaria 12:1-14

Maadui Wa Yerusalemu Kuangamizwa

12:1 Mwa 1:8; Za 102:25; 104:2; Yer 51:15; Ebr 1:10; Isa 57:16; Ebr 12:9Hili ni neno la Bwana kuhusu Israeli. Bwana, yeye azitandaye mbingu, awekaye misingi ya dunia na aiumbaye roho ya mwanadamu ndani yake, asema: 12:2 Za 78:5; 60:3; Isa 51:23; Zek 14:14“Nitakwenda kufanya Yerusalemu kuwa kikombe cha kuyumbisha mataifa yote yanayoizunguka. Yuda utazingirwa kwa vita na Yerusalemu pia. 12:3 Isa 28:16; 29:8; 66:18; Zek 14:2; Dan 2:34-35; Mt 21:44Katika siku hiyo, wakati mataifa yote ya dunia yatakapokusanyika dhidi yake, nitaufanya Yerusalemu kuwa jabali lisilosogezwa kwa mataifa yote. Wote watakaojaribu kulisogeza watajiumiza wenyewe. 12:4 Za 76:6; Zek 10:5Katika siku hiyo nitampiga kila farasi kwa hofu ya ghafula, naye ampandaye nitampiga kwa uwazimu,” asema Bwana. “Nitalielekeza jicho langu la ulinzi juu ya nyumba ya Yuda, nami nitawapofusha farasi wote wa mataifa. 12:5 Eze 30:24Kisha viongozi wa Yuda watasema mioyoni mwao, ‘Watu wa Yerusalemu wana nguvu kwa sababu Bwana Mwenye Nguvu Zote ni Mungu wao.’

12:6 Isa 10:17-18; Zek 11:1; 14:10; Oba 1:18“Katika siku hiyo nitawafanya viongozi wa Yuda kuwa kama kigae cha moto ndani ya lundo la kuni, kama mwenge uwakao kati ya miganda. Watateketeza kulia na kushoto mataifa yote yanayowazunguka, lakini Yerusalemu utabaki salama mahali pake.

12:7 Yer 30:18; Amo 9:11Bwana atayaokoa makao ya Yuda kwanza, ili heshima ya nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu isiwe kubwa zaidi kuliko ile ya Yuda. 12:8 Za 91:4; 82:6; Yoe 3:10, 16; Zek 9:15; Mik 7:8Katika siku hiyo, Bwana atawakinga wale waishio Yerusalemu, ili kwamba aliye dhaifu kupita wote miongoni mwao awe kama Daudi, nayo nyumba ya Daudi itakuwa kama Mungu, kama Malaika wa Bwana akiwatangulia. 12:9 Isa 29:7; Zek 1:21; 14:2-3; 1Kor 1:27-31Katika siku hiyo nitatoka kuangamiza mataifa yote yatakayoshambulia Yerusalemu.

Kumwombolezea Yule Aliyechomwa Mkuki

12:10 Eze 37:9; 39:29; Isa 44:3; Yoe 2:28-29; Za 22:16; Yn 19:34-37; Amu 11:34; Mwa 21:16; Yer 31:19; Yoe 2:28; Lk 2:35; Ufu 1:7“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema12:10 Au: Roho wa neema. na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. 12:11 Yer 50:4; 2Fal 23:29; Mdo 2:37; 2Nya 35:24Katika siku hiyo kilio kitakuwa kikubwa Yerusalemu, kama kilio cha Hadad-Rimoni katika tambarare ya Megido. 12:12 Mt 24:30; Ufu 1:7Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yake, nao wake zao peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi na wake zao, ukoo wa nyumba ya Nathani na wake zao, ukoo wa nyumba ya Lawi na wake zao, ukoo wa Shimei na wake zao, 12:14 Zek 7:3na koo zote zilizobaki na wake zao.

Read More of Zekaria 12

Zekaria 13:1-9

Kutakaswa Dhambi

13:1 Yer 17:13; Law 16:30; Za 51:2; Ebr 9:14; Isa 1:16-17; Yn 1:29; 1Kor 6:11; 1Pet 1:19; 1Yn 1:7“Katika siku hiyo, chemchemi itafunguliwa kwa nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu, kuwatakasa dhambi na unajisi.

13:2 Yer 43:12; 23:14-15; Eze 6:6; 36:25; Hos 2:17; Mik 5:13; 1Fal 22:22; Kut 23:13; 2Pet 2:1“Katika siku hiyo, nitayakatilia mbali majina ya sanamu kutoka nchi, nayo hayatakumbukwa tena,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. “Nitaondoa manabii wao pamoja na roho ya uchafu katika nchi. 13:3 Yer 28:16; 23:34; Kum 13:6-11; 18:20; Neh 6:14; Eze 14:9Ikiwa yupo yeyote atakayeendelea kutabiri, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Ni lazima ufe, kwa sababu umesema uongo kwa jina la Bwana.’ Atakapotabiri, wazazi wake mwenyewe watampasua tumbo.

13:4 Yer 6:15; Mt 3:5; 1Fal 18:7; Isa 20:2; Eze 12:24; Mik 3:6-7“Katika siku hiyo, kila nabii ataaibika kwa maono ya unabii wake. Hatavaa vazi la kinabii la nywele ili apate kudanganya watu. 13:5 Amo 7:14Atasema, ‘Mimi sio nabii. Mimi ni mkulima; ardhi imekuwa kazi yangu tangu ujana wangu.’ Ikiwa mtu atamuuliza, ‘Majeraha haya yaliyo mwilini mwako ni ya nini?’ Atajibu, ‘Ni majeraha niliyoyapata katika nyumba ya rafiki zangu.’

Mchungaji Apigwa, Nao Kondoo Watawanyika

13:7 Isa 34:5; 40:11; 53:4; Yer 47:6; Eze 37:24; 2Sam 17:2; Mk 4:27; Ebr 13:20; Yn 10:20; 1:29; Mk 14:27“Amka, ee upanga, dhidi ya mchungaji wangu,

dhidi ya mtu aliye karibu nami!”

asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

“Mpige mchungaji,

nao kondoo watatawanyika,

nami nitageuza mkono wangu

dhidi ya walio wadogo,

13:8 Eze 5:2-4, 12; Zek 14:2; Rum 11:5katika nchi yote,” asema Bwana,

“theluthi mbili watapigwa na kuangamia;

hata hivyo theluthi moja watabaki ndani yake.

13:9 Isa 4:4; 33:14; 30:16; 44:5; Mal 3:2; Za 12:6; 50:15; 86:7; Dan 11:35; 1Pet 1:6-7; Ay 6:29; Yer 6:27; 29:12; 30:22; Law 26:16; Eze 20:38; Isa 48:10; Za 66:10Hii theluthi moja nitaileta katika moto;

nitawasafisha kama fedha isafishwavyo

na kuwajaribu kama dhahabu.

Wataliitia Jina langu

nami nitawajibu;

nitasema, ‘Hawa ni watu wangu,’

nao watasema, ‘Bwana ni Mungu wetu.’ ”

Read More of Zekaria 13

Zekaria 14:1-21

Bwana Yuaja Kutawala

14:1 Isa 13:6; 23:18; Yoe 1:15; Mal 4:1Siku ya Bwana inakuja ambayo nyara zilizotekwa kwenu zitagawanywa miongoni mwenu.

14:2 Isa 2:3; Zek 12:3; 13:8; Eze 5:8; Mwa 34:29; Mao 5:11; Isa 13:6; Yoe 3:2Nitayakusanya mataifa yote huko Yerusalemu kupigana dhidi yake, mji utatekwa, nyumba zitavamiwa na kuporwa na wanawake watanajisiwa. Nusu ya mji watakwenda uhamishoni, lakini watakaobaki hawataondolewa kutoka mjini.

14:3 Zek 9:14-15; 8:9; Isa 8:9Kisha Bwana atatoka na kupigana dhidi ya watu wa yale mataifa, kama apiganavyo siku ya vita. 14:4 Eze 11:23; Hes 16:31; Mdo 1:11-12; Yoe 3:12Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini. 14:5 Isa 29:6; 66:15-16; Mt 16:27; 25:31; Yud 14; Mt 24:30; Yoe 3:11Nanyi mtakimbia kupitia katika bonde hilo la mlima wangu kwa kuwa litaenea hadi Aseli. Mtakimbia kama mlivyokimbia tetemeko la ardhi katika siku za Uzia mfalme wa Yuda. Kisha Bwana Mungu wangu atakuja na watakatifu wote pamoja naye.

14:6 Isa 13:10; Yer 4:23Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. 14:7 Yer 30:7; Ufu 21:23-25; 22:5; Isa 13:10; 30:26Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Bwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo.

14:8 Eze 47:1-12; Yn 7:38; Ufu 22:1-2; Isa 30:25; Yoe 2:20; Mwa 8:22Siku hiyo, maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu, nusu kwenda kwenye bahari ya mashariki,14:8 Yaani Bahari ya Chumvi au Bahari Mfu. na nusu kwenda kwenye bahari ya magharibi14:8 Yaani Bahari ya Mediterania. wakati wa kiangazi na wakati wa masika.

14:9 Za 22:28; 47:7; Oba 1:21; Kum 6:4; Isa 45:24; Ufu 15:1; Hab 2:14; Efe 4:5-6; Za 2:8Bwana atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo atakuwepo Bwana mmoja na jina lake litakuwa jina pekee.

14:10 1Fal 15:22; Yos 15:32; Isa 2:2; Yer 20:2; 30:18; Amo 9:11; Zek 12:6; 2Fal 14:13; Neh 3:1Nchi yote kuanzia Geba, kaskazini mwa Yuda, hadi Rimoni, kusini mwa Yerusalemu, itakuwa kama Araba.14:10 Araba maana yake Nchi tambarare. Lakini Yerusalemu utainuliwa juu na kubaki mahali pake, toka Lango la Benyamini hadi mahali pa Lango la Kwanza, mpaka kwenye Lango la Pembeni na kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye mashinikizo ya divai ya mfalme. 14:11 Zek 2:4; Za 48:8; Eze 34:25-28; Yer 31:40Utakaliwa na watu, kamwe hautaharibiwa tena, Yerusalemu utakaa salama.

14:12 Isa 11:4; Law 26:16; Kum 28:22; Ay 18:13Hii ndiyo tauni ambayo Bwana atapiga nayo mataifa yote ambayo yalipigana dhidi ya Yerusalemu: Nyama ya miili yao itaoza wangali wamesimama kwa miguu yao, macho yao yataoza kwenye matundu yake na ndimi zao zitaoza vinywani mwao. 14:13 Mwa 35:5; Amu 7:22; Zek 11:6; 1Sam 14:15Katika siku hiyo Bwana atawatia wanaume hofu kuu. Kila mwanaume atakamata mkono wa mwenzake nao watashambuliana. 14:14 Zek 12:2; Isa 23:18Yuda pia atapigana katika Yerusalemu. Utajiri wa mataifa yote yanayoizunguka Yerusalemu utakusanywa, wingi wa dhahabu, fedha na nguo. Tauni ya aina iyo hiyo itapiga farasi na nyumbu, ngamia na punda, nao wanyama wote walioko kwenye kambi za adui.

14:16 2Fal 19:31; Za 22:29; 86:9; Isa 19:21; 60:6-9; Oba 1:21; Kut 23:16; Isa 66:23; 1Tim 6:15; Law 23:34; Neh 8:14; Hos 12:9Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 14:17 2Nya 32:23; Yer 14:4; Amo 4:7; Isa 60:12Ikiwa taifa lolote la dunia hawatakwenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Bwana Mwenye Nguvu Zote, mvua haitanyesha kwao. 14:18 Mwa 27:29Ikiwa watu wa Misri nao hawatakwenda kushiriki, hawatapata mvua. Bwana ataleta juu yao tauni ile ambayo itawapiga mataifa yale ambayo hayatakwenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 14:19 Ezr 3:4Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayatakwenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.

14:20 Kut 39:30; Eze 46:20; Zek 9:15Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: Takatifu kwa Bwana, navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya Bwana vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. 14:21 Yer 31:40; Rum 14:6-7; 1Kor 10:31; Neh 8:10; 11:1; Eze 44:9; Kol 3:17; Isa 35:8; Ufu 21:27; Efe 2:19Kila chungu kilichoko Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya Bwana Mwenye Nguvu Zote.

Read More of Zekaria 14