Zekaria 1:1-21, Zekaria 2:1-13, Zekaria 3:1-10, Zekaria 4:1-14 NEN

Zekaria 1:1-21

Wito Wa Kumrudia Bwana

1:1 Ezr 4:24; 6:15; Mt 23:35; Lk 11:51; Neh 12:4Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema:

1:2 2Nya 36:16Bwana aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. 1:3 Yak 4:8; Mal 3:7; Ay 22:2; Yer 25:5; Mik 7:19; Lk 15:20Kwa hiyo waambie watu: Hivi ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Nirudieni mimi,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitawarudia ninyi,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. 1:4 2Nya 7:14; 24:19; 36:15; Zek 7:7; 2Fal 17:13; Za 78:8; 106:6; Yer 6:17; 17:23; 23:22; Eze 20:18; 33:4; Isa 1:16-17; Yer 3:12; Eze 33:11; Hos 14:1; Mit 3:8-9; Mdo 3:19Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hivi ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemavyo: ‘Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.’ Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema Bwana. Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? 1:6 Isa 44:26; Kum 28:2; Dan 9:12; Hos 5:9; Yer 12:14-17; 39:16; 23:20; 44:17; Mao 2:17; Isa 55:1; Mao 1:18Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?”

“Kisha walitubu na kusema, ‘Bwana Mwenye Nguvu Zote ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ ”

Maono Ya Kwanza: Mtu Katikati Ya Miti Ya Mihadasi

Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido.

1:8 Ufu 6:4; Zek 6:2-7; Yos 5:13Wakati wa usiku nilipata maono, mbele yangu alikuwepo mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia na weupe.

1:9 Zek 4:1-5; 5:5; Dan 7:16Nikauliza, “Hivi ni vitu gani bwana wangu?”

Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, “Nitakuonyesha kuwa ni nini.”

1:10 Zek 6:5-8; Za 91:11; Ebr 1:14Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, “Ni wale ambao Bwana amewatuma waende duniani kote.”

1:11 Isa 14:7; Mwa 16:7; Za 102:20Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa Bwana, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, “Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani.”

1:12 Za 6:3; 40:11; Yer 40:5; 2Nya 36:21; Dan 9:2; Za 103:13; Ufu 6:10; Zek 7:5Kisha malaika wa Bwana akasema, “Bwana Mwenye Nguvu Zote, utazuia mpaka lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?” 1:13 Isa 35:4; Ay 15:11; Zek 4:1; Isa 40:1-2; Yer 29:10Kwa hiyo Bwana akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.

1:14 Isa 26:11; Yoe 2:18; Zek 8:2Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, “Tangaza neno hili: Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, 1:15 Yer 48:11; 2Nya 28:9; Za 69:26; 123:3-4; Amo 1:11; Isa 47:6lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.’

1:16 Zek 2:1-2; 8:3; Ay 38:5; Isa 12:1“Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Bwana: ‘Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa Yerusalemu,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

1:17 Isa 14:1; 40:1; 54:8-10; 61:4; Ezr 9:9; Za 51:18; Isa 51:3; Zek 3:2“Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi na Bwana atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ”

Maono Ya Pili: Pembe Nne Na Mafundi Wanne

Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! 1:19 Amo 6:13; Ezr 4:1; Hab 3:14Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?”

Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.”

Kisha Bwana akanionyesha mafundi wanne. 1:21 1Fal 22:11; Za 75:4, 10; Isa 54:16-17; Zek 12:9Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?”

Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”

Read More of Zekaria 1

Zekaria 2:1-13

Maono Ya Tatu: Mtu Mwenye Kamba Ya Kupimia

Kisha nikatazama juu: pale mbele yangu alikuwepo mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake! 2:2 Eze 40:3; Zek 1:16; Ufu 21:15Nikamuuliza, “Unakwenda wapi?”

Akanijibu, “Kupima Yerusalemu, kupata urefu na upana wake.”

Kisha malaika aliyekuwa akizungumza nami akaondoka, malaika mwingine akaja kukutana naye 2:4 Eze 38:11; Isa 49:20; Yer 30:19; 33:22; Zek 14:11; Eze 36:10na kumwambia: “Kimbia, umwambie yule kijana, ‘Yerusalemu utakuwa mji usio na kuta kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo. 2:5 Isa 10:17; 11:10; 24:23; 26:1; Eze 38:14; 42:20; Za 46:5; 85:9; 125:2; Ufu 21:23; Isa 4:5Mimi mwenyewe nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka,’ asema Bwana, ‘nami nitakuwa utukufu wake ndani yake.’

2:6 Za 44:11; Eze 17:21; 37:9; Mt 24:31; Mk 13:27; Kum 28:64“Njooni! Njooni! Kimbieni mtoke katika nchi ya kaskazini,” asema Bwana, “Kwa kuwa nimewatawanya kwenye pande nne za mbingu,” asema Bwana.

2:7 Isa 42:7; 48:20; Yer 3:18“Njoo, ee Sayuni! Kimbia, wewe ukaaye ndani ya Binti Babeli!” 2:8 Kum 32:10; 2The 1:6Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Baada ya yeye kuniheshimu na kunituma mimi dhidi ya mataifa yaliyokuteka nyara, kwa kuwa yeyote awagusaye ninyi, anaigusa mboni ya jicho lake, 2:9 Isa 14:2; 48:16; Yer 12:14; Hab 2:8; Zek 4:9; 6:15hakika nitauinua mkono wangu dhidi yao ili watumwa wao wawateke nyara. Ndipo mtakapojua ya kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma.

2:10 Sef 3:14; Isa 23:12; Kut 25:8; Hes 23:21; Law 26:12; Zek 8:3; 9:9; Ufu 21:3; 2Kor 6:16“Piga kelele na ufurahie, ee Binti Sayuni, kwa maana ninakuja, nami nitaishi miongoni mwenu,” asema Bwana. 2:11 Yer 23:7; Mik 4:2; Zek 8:8, 20-22; Isa 2:2-3; Kut 12:49; Eze 33:33“Mataifa mengi yataunganishwa na Bwana siku hiyo, nao watakuwa watu wangu. Nitaishi miongoni mwenu nanyi mtajua kwamba Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma kwenu. 2:12 Kut 34:9; Za 33:12; Yer 10:16; 40:5; Kum 12:5; Isa 14:1; Kum 32:9Bwana atairithi Yuda kama fungu lake katika nchi takatifu na atachagua tena Yerusalemu. 2:13 Kut 14:14; Isa 41:1; Kum 26:15; Za 46:10; Hab 2:20; Rum 3:19Tulieni mbele za Bwana, enyi watu wote, kwa sababu ameinuka kutoka makao yake matakatifu.”

Read More of Zekaria 2

Zekaria 3:1-10

Maono Ya Nne: Mavazi Safi Kwa Ajili Ya Kuhani Mkuu

3:1 Ezr 2:2; Zek 6:11; 2Sam 24:1; 2Nya 18:21; Za 109:6; Mt 4:10; Ay 1:6; Ufu 12:10Kisha akanionyesha Yoshua,3:1 Yoshua kwa Kiebrania ni Yeshua, maana yake ni Yehova ni wokovu. kuhani mkuu, akiwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, naye Shetani amesimama upande wake wa kuume ili amshtaki. 3:2 Yud 9, 23; Isa 14:1; 7:4; Za 109:31; Mt 4:10; Lk 22:31; Rum 16:20; 8:33; 11:5Bwana akamwambia Shetani, “Bwana akukemee Shetani! Bwana, ambaye ameichagua Yerusalemu, akukemee! Je, mtu huyu siyo kijinga kinachowaka kilichonyakuliwa kwenye moto?”

3:3 Isa 64:6Wakati huu, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu alipokuwa amesimama mbele ya malaika. 3:4 2Sam 12:13; Eze 36:25; Mik 7:18; Mwa 41:42; Za 132:9; Ufu 19:8; Isa 52:1Malaika akawaambia wale waliokuwa wamesimama mbele yake, “Mvueni hizo nguo zake chafu.”

Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeiondoa dhambi yako, nami nitakuvika mavazi ya kitajiri.”

3:5 Kut 29:6Kisha nikasema, “Mvike kilemba kilicho safi kichwani mwake.” Kwa hiyo wakamvika kilemba safi kichwani na kumvika yale mavazi mengine, wakati malaika wa Bwana akiwa amesimama karibu.

Malaika wa Bwana akamwamuru Yoshua: 3:7 Law 8:35; Kum 17:8-113:7 Eze 44:15-16; 2Nya 23:6; Yer 15:19; Zek 6:15“Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote: ‘Ikiwa utakwenda katika njia zangu na kushika masharti yangu, basi utaitawala nyumba yangu na kuwa na amri juu ya nyua zangu, nami nitakupa nafasi miongoni mwa hawa wasimamao hapa.

3:8 Kum 28:46; Eze 12:11; Isa 4:2; 49:3“ ‘Sikiliza, ee Yoshua kuhani mkuu, pamoja na wenzako walioketi mbele yako, ambao ni watu walio ishara ya mambo yatakayokuja: Ninakwenda kumleta mtumishi wangu, Tawi. Tazama, jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua! Kuna macho saba juu ya jiwe lile moja, nami nitachora maandishi juu yake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nami nitaiondoa dhambi ya nchi hii kwa siku moja.

3:10 Ay 11:18; Hes 16:14; 1Fal 4:25; Mik 4:4“ ‘Katika siku hiyo kila mmoja wenu atamwalika jirani yake akae chini ya mzabibu wake na mtini wake,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

Read More of Zekaria 3

Zekaria 4:1-14

Maono Ya Tano: Kinara Cha Taa Cha Dhahabu Na Mizeituni Miwili

4:1 Dan 8:18; Yer 31:26Kisha malaika aliyezungumza nami akarudi na kuniamsha, kama mtu aamshwavyo kutoka usingizi wake. 4:2 Yer 1:13; Kut 25:31; Ufu 1:12; 4:5Akaniuliza, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Ninaona kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake na taa zake saba juu yake, tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwenye taa zote zilizo juu yake. 4:3 Ufu 11:4; Za 1:3Pia kuna mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume wa bakuli na mwingine upande wa kushoto.”

Nikamuuliza malaika aliyezungumza nami, “Hivi ni vitu gani, bwana wangu?”

4:5 Zek 1:9Akanijibu, “Hujui kuwa hivi ni vitu gani?”

Nikajibu, “Hapana, bwana wangu.”

4:6 1Nya 3:19; Ezr 5:2; 1Sam 2:9; 13:22; 1Fal 19:12; Neh 9:20; Dan 2:34; Isa 11:2-4Kisha akaniambia, “Hili ni neno la Bwana kwa Zerubabeli: ‘Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.

4:7 Za 26:12; 118:22; Yer 51:25; 1Nya 15:28; Isa 40:3-4; Mt 21:21; Ezr 3:11“Wewe ni kitu gani, ee mlima mkubwa sana? Mbele ya Zerubabeli wewe utakuwa ardhi tambarare. Kisha ataweka jiwe la juu kabisa la mwisho na watu wakipiga kelele wakisema, ‘Mungu libariki! Mungu libariki!’ ”

Kisha neno la Bwana likanijia: 4:9 Ezr 3:11; 6:15; Zek 2:9; 6:12; 1Kor 2:4“Mikono ya Zerubabeli iliweka msingi wa Hekalu hili, mikono yake pia italimalizia. Kisha mtajua ya kuwa Bwana Mwenye Nguvu Zote amenituma mimi kwenu.

4:10 Hag 2:23; Ezr 5:1; Neh 12:1; Ay 38:5; 2Nya 16:9; Ufu 5:6“Ni nani anayeidharau siku ya mambo madogo? Watu watashangilia watakapoona timazi mkononi mwa Zerubabeli.

“(Hizi saba ni macho ya Bwana ambayo huzunguka duniani kote.)”

4:11 Ufu 11:4Kisha nikamuuliza yule malaika, “Hii mizeituni miwili iliyoko upande wa kuume na wa kushoto wa kinara cha taa ni nini?”

Tena nikamuuliza, “Haya matawi mawili ya mizeituni karibu na hiyo mirija miwili ya dhahabu inayomimina mafuta ya dhahabu ni nini?”

Akajibu, “Hujui kuwa haya ni nini?”

Nikamjibu, “Hapana, bwana wangu.”

4:14 Kut 29:7; 40:15; Za 45:7; Isa 20:3; Dan 9:24-26Kwa hiyo akasema, “Hawa ni wawili ambao wamepakwa mafuta ili kumtumikia Bwana wa dunia yote.”

Read More of Zekaria 4