Zaburi 71:9-18 NEN

Zaburi 71:9-18

71:9 Za 51:11; 92:14; Kum 4:31; 31:6Usinitupe wakati wa uzee,

wala usiniache nguvu zangu zinapopungua.

71:10 Za 3:7; 10:8; 59:3; 31:13; Mt 1:10; 12:14Kwa maana adui zangu wananisengenya,

wale wanaonivizia kuniua wafanya hila.

71:11 Isa 40:27; 54:7; Mt 27:46; Za 7:2; 9:10; Mao 5:20Wanasema, “Mungu amemwacha,

mkimbilieni mkamkamate,

kwani hakuna wa kumwokoa.”

71:12 Za 38:21, 22; 22:19Ee Mungu, usiwe mbali nami,

njoo haraka kunisaidia, Ee Mungu wangu.

71:13 Ay 8:22; Za 15:3; 70:2; Yer 18:19Washtaki wangu na waangamie kwa aibu,

wale wanaotaka kunidhuru

na wafunikwe kwa dharau na fedheha.

71:14 Za 25:3; 42:5; 130:7; 131:3Lakini mimi, nitatumaini siku zote,

nitakusifu zaidi na zaidi.

71:15 Za 71:8; 66:6; 51:14Kinywa changu kitasimulia haki yako,

wokovu wako mchana kutwa,

ingawa sifahamu kipimo chake.

71:16 Za 77:12; 106:2; 118:15; 9:1; 145:4Ee Bwana Mwenyezi, nitakuja

na kutangaza matendo yako makuu,

nitatangaza haki yako, yako peke yako.

71:17 Yer 7:13; Ay 5:9; Za 26:7; 86:10; 96:3; Kum 4:5Ee Mungu, umenifundisha tangu ujana wangu,

hadi leo ninatangaza matendo yako ya ajabu.

71:18 Isa 46:4; Kut 9:16; Ay 8:8; Yoe 1:3; Za 78:4; 145:4; 22:30, 31Ee Mungu, usiniache,

hata niwapo mzee wa mvi,

mpaka nitangaze uwezo wako kwa kizazi kijacho,

nguvu zako kwa wote watakaokuja baadaye.

Read More of Zaburi 71