Zaburi 60:5-12 NEN

Zaburi 60:5-12

60:5 Ay 40:14; Kum 33:12; Za 108:6Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,

ili wale uwapendao wapate kuokolewa.

60:6 Mwa 12:6; 33:17; Za 89:35; Yos 13:27Mungu amenena kutoka patakatifu pake:

“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi

na kulipima Bonde la Sukothi.

60:7 Yos 13:31; Hes 34:19; Mwa 41:52; 49:10; Kum 33:17Gileadi ni yangu na Manase ni yangu;

Efraimu ni kofia yangu ya chuma,

nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.

60:8 2Sam 8:1Moabu ni sinia langu la kunawia,

juu ya Edomu natupa kiatu changu;

nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”

Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?

Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?

60:10 Yos 7:12; Za 44:9Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,

na hutoki tena na majeshi yetu?

60:11 Za 146:3; Mit 3:5Tuletee msaada dhidi ya adui,

kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.

60:12 1Nya 19:13; Ay 40:12; Za 44:5Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,

naye atawaponda adui zetu.

Read More of Zaburi 60