Zaburi 45:10-17 NEN

Zaburi 45:10-17

45:10 Yer 5:1; Rut 1:11; 1:16; Kum 21:13Sikiliza, ewe binti, fikiri na utege sikio:

Sahau watu wako na nyumba ya baba yako.

45:11 Mao 2:15; Efe 5:33; Isa 54:5; Za 95:6; Es 1:11Mfalme ameshangazwa na uzuri wako;

mheshimu, kwa kuwa yeye ni bwana wako.

45:12 Yos 19:29; 1Fal 9:16; 2Nya 9:24Binti wa Tiro atakuletea zawadi,

watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako.

45:13 Isa 61:10; Kut 39:3; Ufu 19:7, 8Utukufu wote una binti mfalme katika chumba chake;

vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu.

45:14 Amu 5:30; Es 2:15; Wim 1:3Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa,

mabikira wenzake wanamfuata

na wanaletwa kwako.

45:15 Es 8:17Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha,

na kuingia katika jumba la mfalme.

45:16 1Sam 2:8; Za 68:27; 113:8; 1Pet 2:9; Ufu 1:6Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu,

mtawafanya wakuu katika nchi yote.

45:17 Isa 11:10; Mal 1:11; Kut 3:15; Ufu 22:5; Za 33:11; 138:4; 119:90; 135:13Nitadumisha kumbukumbu lako katika vizazi vyote,

kwa hiyo mataifa watakusifu milele na milele.

Read More of Zaburi 45