Zaburi 17:13-15 NEN

Zaburi 17:13-15

17:13 Za 35:8; 55:23; 73:18; Hes 10:3Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe,

niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.

17:14 Za 49:17; Lk 16:8, 25; Isa 2:7; 57:17Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii,

kutokana na watu wa ulimwengu huu

ambao fungu lao liko katika maisha haya.

Na wapate adhabu ya kuwatosha.

Watoto wao na wapate zaidi ya hayo,

hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.

17:15 Za 3:5; Hes 12:2; Mt 5:8; 1Yn 3:2Na mimi katika haki nitauona uso wako,

niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.

Read More of Zaburi 17