Zaburi 119:97-104 NEN

Zaburi 119:97-104

Kuipenda Sheria Ya Bwana

119:97 Za 1:2; 119:15, 47Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

119:98 2Tim 3:17; Kum 4:6, 8; 19:7; Isa 48:17Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

119:99 2Tim 3:15; Za 119:15Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.

119:100 Ay 12:12; 32:7; Za 119:56; Kum 6:17Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,

kwa kuwa ninayatii mausia yako.

119:101 Mit 1:15; 2Kor 7:1; Za 119:57Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya,

ili niweze kutii neno lako.

119:102 Kum 17:20; 4:5Sijaziacha sheria zako,

kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.

119:103 Mit 24:13, 14; 8:11; Za 19:10Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu,

matamu kuliko asali katika kinywa changu!

119:104 Za 111:10; 119:7Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,

kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.

Read More of Zaburi 119