Zaburi 119:169-176 NEN

Zaburi 119:169-176

Kuomba Msaada

119:169 Ay 16:18; Za 119:9, 34Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako,

nipe ufahamu sawasawa na neno lako.

119:170 1Fal 8:30; 2Nya 6:24; Za 28:2; 140:6; 143:1; 3:7; 22:20; 59:1; 119:41Maombi yangu na yafike mbele zako,

niokoe sawasawa na ahadi yako.

119:171 Za 51:15; 63:3; 94:12; Isa 2:3; Mik 4:2Midomo yangu na ibubujike sifa,

kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.

119:172 Za 51:14; 119:7, 75Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako,

kwa kuwa amri zako zote ni za haki.

119:173 Za 37:24; 73:23; Isa 41:10; Lk 10:42; Yos 24:22; Mit 1:29Mkono wako uwe tayari kunisaidia,

kwa kuwa nimechagua mausia yako.

119:174 Za 119:16, 24, 166Ee Bwana, ninatamani wokovu wako,

na sheria yako ni furaha yangu.

119:175 Za 119:116, 159; Isa 55:3Nijalie kuishi ili nipate kukusifu,

na sheria zako zinitegemeze.

119:176 Za 119:10; 95:10; Yer 50:17; Eze 34:11; Lk 15:4Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea.

Mtafute mtumishi wako,

kwa kuwa sijasahau amri zako.

Read More of Zaburi 119