Zaburi 115:12-18 NEN

Zaburi 115:12-18

115:12 1Nya 16:15; Mwa 12:2; Efe 1:3Bwana anatukumbuka na atatubariki:

ataibariki nyumba ya Israeli,

ataibariki nyumba ya Aroni,

115:13 Za 24:4; 112:1; Law 26:3; Mit 10:6; Kum 11:27atawabariki wale wanaomcha Bwana,

wadogo kwa wakubwa.

115:14 Kum 1:11Bwana na awawezeshe kuongezeka,

ninyi na watoto wenu.

115:15 Mdo 14:15; Ufu 10:6; Za 96:5; Mwa 1:1; 14:19Mbarikiwe na Bwana

Muumba wa mbingu na dunia.

115:16 Za 89:11; Mwa 1:28; 8:6-8Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana,

lakini dunia amempa mwanadamu.

115:17 Za 88:10-12Sio wafu wanaomsifu Bwana,

wale washukao mahali pa kimya,115:17 Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania.

115:18 Za 111:1; 113:2; 28:6; 33:2; 105:1; 145:2; Dan 2:20bali ni sisi tunaomtukuza Bwana,

sasa na hata milele.

Msifuni Bwana.115:18 Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah.

Read More of Zaburi 115