Mithali 31:21-31 NEN

Mithali 31:21-31

31:21 Yos 2:18-19; Ebr 9:19-22Theluji ishukapo, hana hofu kwa ajili ya watu wa nyumbani mwake,

kwa maana wote wamevikwa nguo za kutia joto.

Hutengeneza mazulia ya urembo ya kufunika kitanda chake,

yeye huvaa kitani safi na urujuani.

31:23 Kut 3:16; Kum 16:18; Rut 4:1, 11; Mit 12:4Mume wake anaheshimiwa kwenye lango la mji,

aketipo miongoni mwa wazee wa nchi.

Hutengeneza mavazi ya kitani na kuyauza,

naye huwauzia wafanyabiashara mishipi.

31:25 1Tim 2:9, 10Amevikwa nguvu na heshima,

anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo.

Huzungumza kwa hekima

na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake.

31:27 Mit 14:1; 1Tim 5:14; 2Tim 3:15; Tit 2:4-5Huangalia mambo ya nyumbani mwake

wala hali chakula cha uvivu.

31:28 1Fal 2:19Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa,

mumewe pia humsifu, akisema:

“Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri,

lakini wewe umewapita wote.”

31:30 Za 112:1Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi,

bali mwanamke anayemcha Bwana atasifiwa.

Mpe thawabu anayostahili,

nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.

Read More of Mithali 31