Mithali 26:13-22 NEN

Mithali 26:13-22

26:13 Mit 6:6-11; 24:30-34; 22:13Mvivu husema, “Yuko simba barabarani,

simba mkali anazunguka mitaa!”

26:14 Mit 6:9Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake,

ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.

26:15 Mit 19:24Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,

naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.

Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe,

kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.

Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio,

ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.

Kama mtu mwendawazimu

atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha,

26:19 Efe 5:4ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema,

“Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”

26:20 Mit 22:10Bila kuni moto huzimika;

pasipo uchongezi ugomvi humalizika.

26:21 Mit 14:17Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto,

ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.

26:22 Mit 18:8; Eze 22:9Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu;

huingia sehemu za ndani sana za mtu.

Read More of Mithali 26