Mithali 2:12-22 NEN

Mithali 2:12-22

2:12 Mit 2:16; 3:13-18; 4:5Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu,

kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,

2:13 Mit 4:19; Yn 3:19; Efe 4:18wale waachao mapito yaliyonyooka

wakatembea katika njia za giza,

2:14 Mit 15:21; Yer 11:15wale wapendao kutenda mabaya

na kufurahia upotovu wa ubaya,

2:15 Za 125:5; Mit 21:8ambao mapito yao yamepotoka

na ambao ni wapotovu katika njia zao.

2:16 Mit 6:20-29; 7:5-27Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,

kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno

ya kushawishi kutenda ubaya,

2:17 Mal 2:14; Mwa 2:24aliyemwacha mwenzi wa ujana wake

na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.

2:18 Mit 5:5; 7:27; 9:18Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo

na mapito yake kwenye roho za waliokufa.

2:19 Mit 5:8; Mhu 7:26; Ebr 13:4Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi,

au kufikia mapito ya uzima.

2:20 Ebr 6:12Hivyo utatembea katika njia za watu wema

na kushikamana na mapito ya wenye haki.

2:21 Za 37:29Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi,

nao wasio na lawama watabakia ndani yake.

2:22 Ay 18:17; Za 37:38; Kum 29:28Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi,

nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.

Read More of Mithali 2