Hesabu 9:15-23, Hesabu 10:1-36, Hesabu 11:1-3 NEN

Hesabu 9:15-23

Wingu La Moto Juu Ya Maskani

(Kutoka 40:34-38)

9:15 Kut 38:21; 26:30; 33:16; 13:21; 40:34Katika siku hiyo ambayo Maskani, Hema la Ushuhuda, iliposimamishwa, wingu liliifunika. Kuanzia jioni mpaka asubuhi wingu lililokuwa juu ya Maskani lilionekana kama moto. 9:16 Kut 40:38; Kum 1:33; Neh 9:12Hivyo ndivyo lilivyoendelea kuwa; wingu liliifunika wakati wa mchana, na usiku lilionekana kama moto. 9:17 Kut 40:36-38; 1Kor 10:1; Za 78:14; Isa 49:10; Yn 10:4; Hes 9:21; Kut 13:21, 22Wakati wowote wingu lilipoinuka kutoka juu ya Hema, nao Waisraeli waliondoka; mahali popote wingu liliposimama, Waisraeli walipiga kambi. 9:18 Kut 40:37Kwa amri ya Bwana Waisraeli waliondoka, na kwa amri yake walipiga kambi. Kwa muda wote wingu liliposimama juu ya Maskani, Waisraeli walibaki wamepiga kambi.

9:19 Law 8:35; Kut 40:37Wakati wingu lilipobaki juu ya Maskani kwa muda mrefu, Waisraeli walitii amri ya Bwana nao hawakuondoka. 9:20 Za 48:14; Mit 3:5-6Wakati mwingine wingu lilikuwa juu ya Maskani kwa siku chache tu; kwa amri ya Bwana wangelipiga kambi na kisha kwa amri yake wangeliondoka. 9:21 Mt 28:20Wakati mwingine wingu lilikuwepo kuanzia jioni mpaka asubuhi tu, na lilipoinuka asubuhi, nao waliondoka. Ikiwa ni mchana au usiku, wakati wowote wingu lilipoinuka, waliondoka. Ikiwa wingu lilikaa juu ya Maskani kwa siku mbili au mwezi au mwaka, Waisraeli wangebaki wamepiga kambi na hawakuondoka; lakini lilipoinuka, wangeondoka.

9:23 Za 73:24; 107:7; Isa 63:14Kwa amri ya Bwana walipiga kambi, na kwa amri ya Bwana waliondoka. Walitii amri ya Bwana, kufuatana na agizo lake kupitia Mose.

Read More of Hesabu 9

Hesabu 10:1-36

Tarumbeta Za Fedha

Bwana akamwambia Mose: 10:2 Hes 31:6; Neh 4:18; 12:35; Za 47:5; 98:6; 105:3; Yer 4:5; 19; 6:1; Hos 5:8; 8:1; Yoe 2:1“Tengeneza tarumbeta mbili za fedha ya kufua, uzitumie kwa kuita jumuiya pamoja na wakati wa kuvunja makambi ili kuondoka. Tarumbeta zote mbili zikipigwa, jumuiya yote itakusanyika mbele yako katika ingilio la Hema la Kukutania. 10:4 Kut 18:21; Hes 7:2Kama tarumbeta moja tu ikipigwa, viongozi, yaani wakuu wa koo za Israeli, ndio watakaokusanyika mbele yako. Wakati mlio wa kujulisha hatari ukipigwa, makabila yaliyo na makambi upande wa mashariki yataondoka. Ukisikika mlio wa pili wa jinsi hiyo, walioko kwenye makambi ya kusini wataondoka. Mlio huo wa kujulisha hatari utakuwa ishara ya kuondoka. 10:7 Yer 4:5; 6:1; Eze 33:3; Yoe 2:1; 1Kor 14:8Ili kukusanya kusanyiko, piga tarumbeta zote, lakini siyo kwa mlio wa kujulisha hatari.

10:8 Mwa 9:12; Hes 15:14; 35:29; Yos 6:4; 2Nya 13:12“Wana wa Aroni, makuhani, ndio watakaopiga hizo tarumbeta. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yenu na kwa vizazi vijavyo. 10:9 Kut 3:9; Amu 2:18; 6:9; 1Sam 10:18; 2Fal 13:4; Za 106:42; Law 23:24; 2Nya 13:12; Mwa 8:1Wakati mtakapopigana vita katika nchi yenu wenyewe dhidi ya adui anayewaonea, piga tarumbeta kwa mlio wa kujulisha hatari. Ndipo utakumbukwa na Bwana Mungu wenu na kuokolewa kutoka kwa adui zenu. 10:10 Hes 28:11; 1Sam 20:5, 24; 2Fal 4:23; 2Nya 8:13; Za 81:3; Isa 1:13; Eze 45:17; 46:6; Amo 8:5; Law 23:24; 1:3; 3:1; 11:44; Hes 6:14Pia nyakati za furaha yenu, yaani sikukuu zenu zilizoamriwa na sikukuu za Mwezi Mwandamo, mtapiga tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zenu za amani, nazo zitakuwa ukumbusho kwa ajili yenu mbele za Mungu wenu. Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.”

Waisraeli Waondoka Sinai

10:11 Kut 38:21; 40:17; Hes 9:17Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili wa mwaka wa pili, wingu liliinuka kutoka juu ya maskani ya Ushuhuda. 10:12 Mwa 14:6; Kum 1:1; 33:2; Kut 40:36; Hes 12:16; Hab 3:3Ndipo Waisraeli wakaondoka kutoka Jangwa la Sinai wakasafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine mpaka wingu lilipotua katika Jangwa la Parani. 10:13 Kum 1:6; Hes 2:34Waliondoka kwa mara ya kwanza kwa agizo la Bwana kupitia kwa Mose.

10:14 Hes 1:52; 2:3-9; 1:7Vikosi vya kambi ya Yuda vilitangulia kwanza chini ya alama yao. Nashoni mwana wa Aminadabu alikuwa kiongozi wao. 10:15 Law 24:11; Hes 1:8Nethaneli mwana wa Suari alikuwa kiongozi wa kabila la Isakari, 10:16 Hes 2:7; 1:9naye Eliabu mwana wa Heloni alikuwa kiongozi wa kabila la Zabuloni. 10:17 Hes 4:21-32Ndipo Maskani iliposhushwa, nao wana wa Gershoni na wana wa Merari ambao waliibeba wakaondoka.

10:18 Hes 2:16; 2:10-16; 1:5Vikosi vya kambi ya Reubeni vilifuata, chini ya alama yao. Elisuri mwana wa Shedeuri alikuwa kiongozi wao. Shelumieli mwana wa Surishadai aliongoza kikosi cha kabila la Simeoni, 10:20 Hes 1:14naye Eliasafu mwana wa Deueli aliongoza kikosi cha kabila la Gadi. 10:21 Hes 2:17; 4:20Kisha Wakohathi wakaondoka, wakichukua vitu vitakatifu. Maskani ilikuwa isimamishwe kabla wao hawajafika.

10:22 Hes 2:24; 1:10Vikosi vya kambi ya Efraimu vilifuata, chini ya alama yao. Elishama mwana wa Amihudi alikuwa kiongozi wao. Gamalieli mwana wa Pedasuri aliongoza kikosi cha kabila la Manase, 10:24 Hes 1:11naye Abidani mwana wa Gideoni alikuwa kiongozi wa kikosi cha kabila la Benyamini.

10:25 Hes 2:31; 1:12; Yos 6:9Mwishowe, kama kikosi cha nyuma cha ulinzi wa vikosi vyote, vikosi vya kambi ya Dani viliondoka chini ya alama yao. Ahiezeri mwana wa Amishadai alikuwa kiongozi wao. Pagieli mwana wa Okrani aliongoza kikosi cha kabila la Asheri, naye Ahira mwana wa Enani aliongoza kikosi cha kabila la Naftali. 10:28 Za 80:1; Wim 6:10Huu ndio ulikuwa utaratibu wa kuondoka wa vikosi vya Waisraeli walipokuwa wanaondoka.

10:29 Amu 4:11; Kut 2:18; 3:1; Mwa 12:7; 15:14Basi Mose akamwambia Hobabu mwana wa Reueli, Mmidiani, mkwewe Mose, “Tunaondoka kwenda mahali ambapo Bwana amesema ‘Nitawapa ninyi mahali hapo.’ Twende pamoja nasi tutakutendea mema, kwa maana Bwana ameahidi mambo mema kwa Israeli.”

10:30 Mt 21:29; Kut 18:27Akajibu, “Hapana, sitakwenda; nitarudi kwenye nchi yangu mwenyewe na watu wangu mwenyewe.”

10:31 Ay 29:15Lakini Mose akasema, “Tafadhali usituache. Wewe unajua mahali ambapo yatupasa kupiga kambi jangwani, nawe unaweza kuwa macho yetu. 10:32 Kut 12:48; Kum 10:18; Za 22:27-31; 67:5-7Ikiwa utafuatana nasi, tutashirikiana nawe mema yoyote tutakayopewa na Bwana.”

10:33 Kum 1:33; 10:8; 31:9; Yos 3:3; Amu 20:27; 2Sam 15:24; Yer 31:2Hivyo waliondoka kutoka mlima wa Bwana, nao wakasafiri kwa siku tatu. Sanduku la Agano la Bwana liliwatangulia kwa zile siku tatu ili kuwatafutia mahali pa kupumzika. 10:34 Hes 9:15-23; Kut 13:21; Neh 9:12, 19Wingu la Bwana lilikuwa juu yao wakati wa mchana walipoondoka kambini.

10:35 2Nya 6:41; Za 17:13; 44:26; 94:2; 132:8; Amu 5:31; 2Sam 2:1; Za 68:1; 92:9; Kum 5:9; 7:10; Isa 17:12-14; 59:18Wakati wowote Sanduku lilipoondoka, Mose alisema,

“Ee Bwana, inuka!

Watesi wako na watawanyike;

adui zako na wakimbie mbele zako.”

10:36 Isa 52:8; 63:17; Mwa 15:5; 26:4; Kum 1:10; 10:22; Neh 9:23Wakati wowote Sanduku liliposimama, alisema,

“Ee Bwana, rudi,

kwa maelfu ya Waisraeli wasiohesabika.”

Read More of Hesabu 10

Hesabu 11:1-3

Moto Kutoka Kwa Bwana

11:1 Law 10:2; Kut 4:14; 14:11; 16:7; Mao 3:39; Hes 12:2; 21:28; Kum 1:34; Za 78:63; Isa 26:11; Kut 15:23, 24; 16:2, 3, 7; Kum 9:22; 2Fal 1:12Basi watu wakalalamika kwa habari ya taabu zao masikioni mwa Bwana, naye alipowasikia, hasira yake ikawaka. Ndipo moto kutoka kwa Bwana ukawaka miongoni mwao na kuteketeza baadhi ya viunga vya kambi. 11:2 Kum 9:19; 1Sam 2:25; 12:23; Za 106:23; Mwa 20:7; Hes 21:7; Yn 2:1Watu walipomlilia Mose, akamwomba Bwana, nao moto ukazimika. 11:3 Kum 9:20-22; Hes 16:35; Ay 1:16; Isa 10:17Hivyo mahali pale pakaitwa Tabera,11:3 Tabera maana yake Kunaungua. kwa sababu moto kutoka kwa Bwana uliwaka miongoni mwao.

Read More of Hesabu 11