Mathayo 27:45-66 NEN

Mathayo 27:45-66

Kifo Cha Yesu

(Marko 15:33-41; Luka 23:44-49; Yohana 19:28-30)

27:45 Amo 8:9Tangu saa sita hadi saa tisa giza liliifunika nchi yote. 27:46 Za 22:1Ilipofika saa tisa, Yesu akapaza sauti akalia, “Eloi, Eloi, lama sabakthani?” (maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”)

Baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale waliposikia hayo, wakasema, “Anamwita Eliya.”

27:48 Mt 27:34; Za 69:21Ghafula mmoja wao akaenda mbio na kuleta sifongo, akaichovya kwenye siki, akaiweka kwenye mwanzi na akampa Yesu ili anywe. Wengine wakasema, “Basi mwacheni. Hebu tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”

27:50 Yn 19:30Yesu alipolia tena kwa sauti kuu, akaitoa roho yake.

27:51 Kut 26:31-33; Ebr 10:19Wakati huo huo pazia la Hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini. Dunia ikatetemeka na miamba ikapasuka. Makaburi yakafunguka na miili ya watakatifu waliokuwa wamekufa ikafufuliwa. 27:53 Mt 4:5Wakatoka makaburini, na baada ya Yesu kufufuka, waliingia kwenye Mji Mtakatifu na kuwatokea watu wengi.

27:54 Mt 4:3; 17:5Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa, wakasema, “Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”

27:55 Lk 8:2-3Walikuwako wanawake huko wakiangalia kwa mbali. Hawa walikuwa wamemfuata Yesu tangu Galilaya ili kushughulikia mahitaji yake. 27:56 Lk 24:10; Yn 19:25Miongoni mwao walikuwepo Maria Magdalene, na Maria mama yao Yakobo na Yosefu, na mama yao wana wa Zebedayo.

Maziko Ya Yesu

(Marko 15:42-47; Luka 23:50-56; Yohana 19:38-42)

27:57 Kut 34:25; Mk 15:42; Lk 23:50; Yn 19:38Ilipofika jioni, alifika mtu mmoja tajiri kutoka Arimathaya aitwaye Yosefu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu. Akamwendea Pilato ili kumwomba mwili wa Yesu. Pilato akaamuru apewe. Yosefu akauchukua mwili wa Yesu, akaufunga katika kitambaa cha kitani safi, 27:60 Mk 16:4; Mdo 13:29na kuuweka katika kaburi lake mwenyewe jipya, alilokuwa amelichonga kwenye mwamba. Kisha akavingirisha jiwe kubwa katika ingilio la kaburi, akaenda zake. Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikuwepo mahali pale, wakiwa wameketi mkabala na kaburi.

Walinzi Pale Kaburini

Kesho yake, yaani siku iliyofuata ile ya Maandalizi ya Sabato, viongozi wa makuhani na Mafarisayo wakamwendea Pilato 27:63 Mt 16:21na kusema, “Bwana, tumekumbuka kwamba yule mdanganyifu wakati alikuwa bado hai alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 27:64 Mt 28:13Kwa hiyo uamuru kaburi lilindwe kwa uthabiti mpaka baada ya siku tatu. La sivyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kuuiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuliwa kutoka kwa wafu. Udanganyifu huu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”

27:65 Mt 28:11Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari walinzi. Nendeni, liwekeeni ulinzi kadri mwezavyo.” 27:66 Dan 6:7; Mt 28:2; 28:11Kwa hiyo wakaenda na walinzi ili kulilinda kaburi kwa uthabiti, wakatia muhuri kwenye lile jiwe na kuweka ulinzi.

Read More of Mathayo 27