Mathayo 26:47-68 NEN

Mathayo 26:47-68

Yesu Akamatwa

(Marko 14:43-50; Luka 22:47-53; Yohana 18:3-12)

26:47 Mt 10:4Alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale Kumi na Wawili, akafika. Alikuwa amefuatana na umati mkubwa wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani na wazee wa watu. Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni.” 26:49 Mt 23:7Mara Yuda akamjia Yesu na kumsalimu, “Salamu, Rabi!” Akambusu.

26:50 Mt 20:13; 22:12Yesu akamwambia, “Rafiki, fanya kile ulichokuja kufanya hapa.”

Kisha wale watu wakasogea mbele, wakamkamata Yesu. 26:51 Lk 22:36-38; Yn 18:10Ghafula mmoja wa wale waliokuwa na Yesu alipoona hivyo, akaushika upanga wake, akauchomoa na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.

26:52 Kut 21:12; Ufu 13:10Ndipo Yesu akamwambia, “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote watumiao upanga watakufa kwa upanga. 26:53 2Fal 6:17; Mt 4:11Je, unadhani siwezi kumwomba Baba yangu naye mara moja akaniletea zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika? 26:54 Mt 1:22; 26:24Lakini je, yale Maandiko yanayotabiri kwamba ni lazima itendeke hivi yatatimiaje?”

26:55 Lk 21:27; Yn 18:20Wakati huo, Yesu akawaambia ule umati wa watu, “Je, mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyangʼanyi? Siku kwa siku niliketi Hekaluni nikifundisha, mbona hamkunikamata? 26:56 Mt 26:31Lakini haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia.” Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha na kukimbia.

Yesu Mbele Ya Kuhani Mkuu

(Marko 14:53-65; Luka 22:54-71; Yohana 18:13-24)

26:57 Mk 14:53; Lk 22:54; Yn 18:12; 13:14Wale waliokuwa wamemkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, kuhani mkuu, mahali ambapo walimu wa sheria pamoja na wazee walikuwa wamekusanyika. 26:58 Mk 14:66; 15:16; Lk 22:55; 11:21Lakini Petro akamfuata kwa mbali hadi uani kwa kuhani mkuu. Akaingia ndani, akaketi pamoja na walinzi ili aone litakalotukia.

26:59 Mt 5:22Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu ili wapate kumuua. 26:60 Za 27:12; Mdo 6:13; Kum 19:15Lakini hawakupata jambo lolote, ingawa mashahidi wengi wa uongo walijitokeza.

Hatimaye wakajitokeza mashahidi wawili wa uongo 26:61 Yn 2:19na kusema, “Huyu mtu alisema, ‘Ninaweza kulivunja Hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.’ ”

26:62 Mk 14:60Kisha kuhani mkuu akasimama na kumwambia Yesu, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?” 26:63 Mt 27:12-14; Mk 14:61; Dan 7:13Lakini Yesu akakaa kimya.

Ndipo kuhani mkuu akamwambia, “Nakuapisha mbele za Mungu aliye hai. Tuambie kama wewe ndiwe Kristo,26:63 Kristo maana yake ni Masiya, yaani Aliyetiwa mafuta. Mwana wa Mungu.”

26:64 Dan 7:13; Mt 16:27; 24:30; Lk 21:27Yesu akajibu, “Wewe umenena. Lakini ninawaambia nyote: Siku za baadaye, mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”

26:65 Mk 14:63Ndipo kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi? Tazama, sasa ninyi mmesikia hayo makufuru. 26:66 Law 24:16; Yn 19:7Uamuzi wenu ni gani?”

Wakajibu, “Anastahili kufa.”

26:67 Mt 16:21; 27:30Kisha wakamtemea mate usoni na wengine wakampiga ngumi. Wengine wakampiga makofi 26:68 Lk 22:63-65na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo! Ni nani aliyekupiga?”

Read More of Mathayo 26