Luka 8:40-56, Luka 9:1-9 NEN

Luka 8:40-56

Msichana Afufuliwa, Na Mwanamke Aponywa

(Mathayo 9:18-26; Marko 5:21-43)

8:40 Mt 9:18-26; Mk 5:21-43Basi Yesu aliporudi, umati mkubwa wa watu ukampokea kwa furaha, kwani walikuwa wakimngojea. 8:41 Mk 5:22Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Yesu, akimwomba afike nyumbani kwake, 8:42 Lk 7:12kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, alikuwa anakufa.

Yesu alipokuwa akienda, umati wa watu ukamsonga sana. 8:43 Law 15:25-30Katika umati huo palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili. Tena alikuwa amegharimia yote aliyokuwa nayo kwa ajili ya matibabu, wala hakuna yeyote aliyeweza kumponya. 8:44 Mt 9:20Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Yesu na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma.

8:45 Lk 5:5Yesu akauliza, “Ni nani aliyenigusa?”

Watu wote walipokana, Petro akasema, “Bwana, huu umati wa watu unakusonga na kukusukuma kila upande.”

8:46 Mt 14:36; Mk 3:10; Lk 5:17; 6:19Lakini Yesu akasema, “Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka.”

Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Yesu. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara. 8:48 Mt 9:22; Mdo 15:33Basi Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani.”

8:49 Lk 8:41Yesu alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani kwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia, “Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu.”

Yesu aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo, “Usiogope. Amini tu, naye binti yako atapona.”

8:51 Mt 4:21Walipofika nyumbani kwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, pamoja na baba na mama wa yule binti. 8:52 Lk 23:27; Mt 9; 24; Yn 11:11-13Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Yesu akawaambia, “Acheni kulia. Huyu binti hajafa, ila amelala.”

Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa. 8:54 Lk 7:14Yesu akamshika yule binti mkono na kuita, “Binti, amka!” Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula. 8:56 Mt 8:4Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Yesu akawakataza wasimwambie mtu yeyote juu ya yale yaliyotukia.

Read More of Luka 8

Luka 9:1-9

Yesu Awatuma Wale Kumi Na Wawili

(Mathayo 10:5-15; Marko 6:7-13)

9:1 Mt 10:1; 4:23; Lk 5:17Yesu kisha akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa mamlaka na uwezo wa kutoa pepo wachafu wote na kuponya magonjwa yote, 9:2 Mt 3:2kisha akawatuma waende wakahubiri Ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa. 9:3 Lk 10:4; 22:35Akawaagiza akisema, “Msichukue chochote safarini: sio fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, hata msichukue kanzu ya ziada. 9:4 Mt 10:11; Mk 6:10Katika nyumba yoyote mwingiayo, kaeni humo hadi mtakapoondoka katika mji huo. 9:5 Lk 10:14Kama watu wasipowakaribisha, mnapoondoka katika mji wao, kungʼuteni mavumbi kutoka kwenye miguu yenu ili kuwa ushuhuda dhidi yao.” 9:6 Mk 6:12Hivyo wale wanafunzi wakaondoka wakaenda kutoka kijiji hadi kijiji, wakihubiri habari njema na kuponya wagonjwa kila mahali.

Herode Afadhaika

(Mathayo 14:1-12; Marko 6:14-29)

9:7 Mt 3:1; 14:1Basi Mfalme Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia habari za yote yaliyotendeka. Naye akafadhaika, kwa kuwa baadhi ya watu walikuwa wakisema Yohana Mbatizaji amefufuliwa kutoka kwa wafu. 9:8 Mt 11:14; Yn 1:21Wengine wakasema Eliya amewatokea, na wengine wakasema kwamba mmoja wa manabii wa kale amefufuka. 9:9 Lk 23:8Herode akasema, “Yohana nilimkata kichwa. Lakini ni nani huyu ambaye ninasikia mambo kama haya kumhusu?” Akatamani sana kumwona.

Read More of Luka 9