Walawi 1:1-17, Walawi 2:1-16, Walawi 3:1-17 NEN

Walawi 1:1-17

Sadaka Ya Kuteketezwa

1:1 Kut 3:4; 19:3; 25:22; 40:2; Hes 7:89; 12:4-5Bwana akamwita Mose na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia, 1:2 Law 22:18-21; 7:16, 38; 23:38; 27:9; Hes 15:3“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe au la kondoo na mbuzi.

1:3 Kum 15:21; 12:5-6, 11; Mwa 8:20; Law 6:25; 17:9; 22:19-20, 27; Ezr 8:35; Mal 1:8; Kut 12:5; Ebr 9:14; 1Pet 1:19; Hes 6:16; Isa 58:5“ ‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ngʼombe, atamtoa ngʼombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Bwana. 1:4 Kut 29:10, 15, 36; Law 4:29; 6:25; Eze 45:15; Mwa 32:20, 30; 2Nya 29:23-24; Kut 29:26; 32:30; Isa 56:7; Rum 12:1; Hes 15:25; Flp 4:18; Ebr 10:11Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake. 1:5 Kut 29:11, 20; Law 3:2, 8; 8:2; 10:6; 21:1; Hes 15:8; Kum 13:8; Za 50:9; 69:31; Ebr 12:24; 1Pet 1:2Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Aroni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania. 1:6 Law 7:8; Kut 29:17Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande. 1:7 Mwa 22:9; Law 3:5; 6:12Wana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto. 1:8 Kut 29:13; Law 8:20; 9:13Kisha wana wa Aroni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 1:9 Kut 29:17, 18; Law 2:2; 3:5; 17:6; 6:22; 9:14; 23:8, 25, 36; Hes 28:6, 19; 18:17; 28:11-13; Mwa 8:21; Efe 2:5Ataziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

1:10 Mwa 22:7; Kut 12:5; Law 3:12; 4:23, 28; 5:6; Hes 15:11“ ‘Kama sadaka ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa mnyama dume asiye na dosari. 1:11 Kut 29:11, 20Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za Bwana, nao wana wa Aroni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu. Atamkata vipande vipande, naye kuhani atavipanga, pamoja na kichwa na mafuta ya mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. 1:13 Kut 29:17; Law 6:22; Kum 12:27Ataosha sehemu za ndani na miguu kwa maji, naye kuhani atavileta vyote na kuvichoma juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

1:14 Mwa 15:9; Lk 2:24; Law 5:7; Lk 2:24“ ‘Kama sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwa Bwana ni ndege, atamtoa hua au kinda la njiwa. 1:15 Law 5:8-9Kuhani atamleta kwenye madhabahu, naye atamvunja shingo na kumnyofoa kichwa na kumchoma juu ya madhabahu. Damu yake itachuruzishwa ubavuni mwa madhabahu. 1:16 Law 4:12; 6:10; Hes 4:13Ataondoa kifuko cha chakula pamoja na uchafu wake na kuvitupa upande wa mashariki wa madhabahu, mahali pale penye majivu. 1:17 Mwa 15:10; Law 5:8Atampasua na kumweka wazi katika mabawa yake, lakini asimwachanishe kabisa, kisha kuhani ataichoma juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

Read More of Walawi 1

Walawi 2:1-16

Sadaka Ya Nafaka

2:1 Kut 29:2, 41; Law 6:14-18; 5:11; 7:12; 24:7; Hes 15:4; 28:5; Neh 13:9; Isa 43:23“ ‘Mtu yeyote aletapo sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake itakuwa ya unga laini. Atamimina mafuta juu yake, aweke uvumba juu yake, 2:2 Law 1:9; 5:11, 12; 6:15; 24:7; Isa 1:13; 53:12; 65:3; 66:3; Hes 5:26; 18:8; Za 16:5; 73:26; Mdo 10:4naye atapeleka kwa makuhani wana wa Aroni. Kuhani atachukua konzi moja iliyojaa unga laini na mafuta pamoja na uvumba wote, na kuuteketeza kama sehemu ya kumbukumbu juu ya madhabahu, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 2:3 Law 6:16; 10:12-13; Kut 30:36; Hes 18:9Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe, ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

2:4 Law 7:9, 12; 8:26; 26:26; Kut 29:2“ ‘Kama utaleta sadaka ya nafaka iliyookwa jikoni, itakuwa ya unga laini: maandazi yaliyotengenezwa bila kutiwa chachu, yaliyochanganywa na mafuta, au mikate myembamba iliyotengenezwa bila kutiwa chachu, na iliyopakwa mafuta. 2:5 Law 6:21; 7:9; Eze 4:3Iwapo sadaka yako ya nafaka imeandaliwa kwenye kikaango, itakuwa ni ya unga laini uliochanganywa na mafuta, bila chachu. Ukande na kumimina mafuta juu yake; hii ni sadaka ya nafaka. 2:7 Law 7:9Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa kwenye sufuria, itatengenezwa kwa unga laini na mafuta. Ilete hiyo sadaka ya nafaka iliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana; mkabidhi kuhani ambaye ataipeleka madhabahuni. 2:9 Mwa 8:21; Kut 29:18; Rum 12:1Naye atatoa ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu kuwa sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana. 2:10 Ezr 2:63; Kut 29:18, 37Sadaka ya nafaka iliyobaki ni ya Aroni na wanawe; ni sehemu ya sadaka iliyo takatifu sana ya sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

2:11 Kut 34:25; 23:18; Law 6:16; Mt 16:12; Mk 8:15; 1Kor 5:8; Gal 5:8-9“ ‘Kila sadaka ya nafaka unayoleta kwa Bwana ni lazima ifanywe bila kutiwa chachu, kwa kuwa huna ruhusa kuchoma chachu yoyote au asali katika sadaka itolewayo kwa Bwana kwa moto. 2:12 Kut 34:22; 22:29; Law 23:10-11; Kum 26:10Unaweza kuzileta kwa Bwana kama sadaka ya malimbuko, lakini haziwezi kutolewa juu ya madhabahu kama harufu nzuri ya kupendeza. 2:13 Mk 9:49; Hes 18:19; 2Nya 13:5; Eze 43:24; Kol 4:6Koleza sadaka zako zote za nafaka kwa chumvi. Usiache kuweka chumvi ya Agano la Mungu wako katika sadaka zako za nafaka; weka chumvi kwenye sadaka zako zote.

2:14 Kut 34:22; Hes 15:20; Kum 16:13; 26:2; Rut 3:2; Kut 23:19; Mit 3:9; 2Fal 4:42“ ‘Kama ukileta malimbuko ya sadaka ya nafaka kwa Bwana, utatoa masuke yaliyopondwa ya nafaka mpya iliyookwa kwa moto. Weka mafuta na uvumba juu yake; ni sadaka ya nafaka. 2:16 Hes 4:16; Yer 14:12Kuhani atateketeza ile sehemu ya kumbukumbu kutoka kwenye hiyo sadaka ya nafaka iliyopondwa kwa mafuta, pamoja na uvumba wote, kama sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

Read More of Walawi 2

Walawi 3:1-17

Sadaka Ya Amani

3:1 Kut 32:6; 12:5; Law 7:11-34; 17:5“ ‘Kama sadaka ya mtu ni sadaka ya amani, naye akatoa ngʼombe kutoka kundi, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Bwana. 3:2 Kut 29:15, 20; 40:2; 24:6; Hes 8:10; 18:17; Law 1:5; 17:6; Isa 53:4; Ebr 9:28; 1Pet 2:24; 3:18Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani wana wa Aroni watanyunyiza damu yake pande zote za madhabahu. 3:3 Kut 29:13; 12:9; 3:4; 29:13; Law 4:9Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yote ya mnyama yafunikayo sehemu za ndani, ama yanayoungana na hizo sehemu za ndani, figo zote pamoja na mafuta yote yanayozizunguka karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. 3:5 Law 1:7-9; 7:29-34; Kut 29:13, 38-42; Hes 28:3-10; 1Sam 2:15-16Kisha wana wa Aroni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni zinazowaka, kama sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.

3:6 Law 22:21; Hes 15:3, 8; 2Kor 5:21; Tit 2:11-12; Ebr 7:26-27“ ‘Kama akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kama sadaka ya amani kwa Bwana, atamtoa dume au jike asiye na dosari. 3:7 Law 17:3, 8-9; Hes 15:5; 28:5-8; 1Fal 8:62Kama akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Bwana. 3:8 Law 1:5Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. 3:9 Isa 34:6; Yer 46:10; Eze 39:19; Sef 1:7Kutoka kwenye hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Bwana kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo, figo mbili pamoja na mafuta yanayozizunguka yaliyo karibu na kiuno na yale yanayofunika ini, ambayo atayatoa pamoja na figo. 3:11 Law 21:6, 17; 9:18; Hes 28:2; Eze 44:7Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.

3:12 Law 1:10; 4:3“ ‘Kama sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Bwana. 3:13 Kut 24:6; Law 1:5Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Aroni watanyunyiza damu yake kwenye madhabahu pande zote. Kutokana na ile sadaka anayotoa, atatoa sadaka hii kwa Bwana kwa moto: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo, 3:15 Law 7:4; 3:16; 7:31; 1:9; Mwa 4:4; 1Sam 2:16; Law 7:23; 2Nya 7:7figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno na yanayofunika ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo. Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu kama chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Bwana.

3:17 Kut 12:14, 20; 27:21; Mwa 9:12; Law 7:25-26; 17:10-16; Kum 12:16; Mdo 15:20“ ‘Hii ni kanuni ya kudumu kwa vizazi vijavyo, popote muishipo: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ”

Read More of Walawi 3