Yohana 1:29-51 NEN

Yohana 1:29-51

Yesu Mwana-Kondoo Wa Mungu

1:29 Mwa 22:8; Ufu 5:6Siku iliyofuata, Yohana alimwona Yesu akimjia akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu! 1:30 Yn 15:27Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu.’ 1:31 Mal 3:1; Mt 3:6; Lk 1:17, 76, 77; 3:3, 4Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”

1:32 Mt 3:16; Mk 1:10Kisha Yohana akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake. 1:33 Mk 1:4; Mt 3:11Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho Mtakatifu.’ 1:34 Mt 4:3Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”

Wanafunzi Wa Kwanza Wa Yesu

1:35 Mt 3:1Siku iliyofuata, Yohana alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili. 1:36 Yn 1:29Alipomwona Yesu akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!”

Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yohana akisema haya, wakamfuata Yesu. 1:38 Mt 23:7Yesu akageuka, akawaona wakimfuata akawauliza, “Mnataka nini?”

Wakamwambia, “Rabi,” (maana yake Mwalimu), “Unaishi wapi?”

Yesu akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!”

Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.

1:40 Mt 4:18-22Andrea nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yohana aliyokuwa amesema, naye ndiye alimfuata Yesu. 1:41 Yn 4:25Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masiya” (yaani, Kristo). 1:42 Mwa 32:28; Mt 16:18Naye akamleta kwa Yesu.

Yesu akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro1:42 Petro kwa Kiyunani au Kefa kwa Kiaramu; maana yake ni Kipande cha mwamba.).

Yesu Awaita Filipo Na Nathanaeli

1:43 Mt 10:3; Yn 14:8-9; Mt 4:9Siku iliyofuata Yesu aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”

1:44 Yn 12:21Basi Filipo alikuwa mwenyeji wa Bethsaida, mji alikotoka Andrea na Petro. 1:45 Yn 21:2; Lk 24:27; Mt 2:23; Lk 3:23Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Mose aliandika habari zake katika Sheria na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani, Yesu wa Nazareti, mwana wa Yosefu.”

1:46 Yn 7:41-42, 52Nathanaeli akauliza, “Nazareti! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nazareti?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”

1:47 Za 32:2; Rum 9:4-6Yesu alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.”

Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?”

Yesu akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”

1:49 Mt 23:7; 4:3; 2; 2; 27:42Nathanaeli akamwambia, “Rabi, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”

Yesu akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu zaidi kuliko hilo.” 1:51 Mt 3:16; 8:20; Mwa 28:12Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

Read More of Yohana 1