Ayubu 35:1-16, Ayubu 36:1-33, Ayubu 37:1-24 NEN

Ayubu 35:1-16

Elihu Analaumu Mtu Kujiona Kuwa Mwenye Haki

Ndipo Elihu akasema:

35:2 Ay 33:32; 2:9; 32:2“Je, unadhani hili ni haki?

Wewe unasema, ‘Nina haki mbele za Mungu.’

35:3 Ay 21:15; 34:9Bado unamuuliza, ‘Ni faida gani nimepata,

na imenifaidi nini kwa kutokutenda dhambi?’

“Ningependa nikujibu wewe

pamoja na marafiki zako walio pamoja nawe.

35:5 Kum 10:14; Mwa 15:5; Ay 22:12; Za 19:1-4Tazama juu mbinguni ukaone;

yaangalie mawingu yaliyo juu sana juu yako.

35:6 Ay 7:20; Mit 8:36Je, ukitenda dhambi, inamdhuruje Mungu?

Kama dhambi zako zikiwa nyingi,

hilo linamfanyia nini Mungu?

35:7 Rum 11:35; Mit 9:12; 1Kor 4:7; Lk 17:10Kama wewe ni mwadilifu, unampa nini,

au yeye anapokea nini mkononi kwako?

35:8 Eze 18:24; 18:5-9; Zek 7:9-10Uovu wako unamdhuru tu mtu mwingine kama wewe,

nayo haki yako inawafaa wanadamu tu.

35:9 Kut 2:23; Ay 5:15; 12:19; Lk 18:3-7“Wanadamu hulia kwa kulemewa na mateso;

huomba msaada kutoka mkono wenye nguvu.

35:10 Ay 4:17; Isa 51:13; Za 77:6; Mdo 16:25; 1Pet 4:19Lakini hakuna asemaye, ‘Yuko wapi Mungu Muumba wangu,

yeye anifanyaye niimbe usiku,

35:11 Za 94:12; Lk 12:24; Ay 32:8yeye atufundishaye sisi zaidi kuliko wanyama wa dunia,

na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?’

35:12 1Sam 8:18; Mit 1:1Yeye hajibu wakati watu waliapo

kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

35:13 Kum 1:45; 1Sam 8:18; Ay 15:31; Mit 15:8Naam, Mungu hasikilizi maombi yao ya ubatili;

Mwenyezi hayazingatii.

35:14 Ay 9:11; Yer 11:11Si zaidi sana kwamba hatakusikiliza

wewe usemapo humwoni,

tena ya kwamba shauri lako liko mbele zake

na wewe lazima umngojee,

pia zaidi, kwamba hasira yake kamwe haiadhibu

wala haangalii uovu hata kidogo?

35:16 Ay 34:35-37; 1Kor 4:20Hivyo Ayubu hufumbua kinywa chake kwa maneno yasiyo na maana;

anaongea maneno mengi bila maarifa.”

Read More of Ayubu 35

Ayubu 36:1-33

Elihu Atukuza Wema Wa Mungu

Elihu akaendelea kusema:

“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha

kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.

36:3 Ay 4:17; 8:3Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali,

nami nitamhesabia haki Muumba wangu.

36:4 Ay 6:28; 13:6; 37:5, 16, 23; 32:17Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo;

mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.

36:5 Za 31:22; 69:33; Hes 23:19; Rum 11:29“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu;

ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.

36:6 Ay 8:22; 4:10Hawaachi waovu waendelee kuishi,

bali huwapa walioteswa haki yao.

36:7 Za 34:15; 113:8; Mt 6:18; Isa 22:23Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki;

huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme

na kuwatukuza milele.

36:8 2Sam 3:34; 2Fal 23:33Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo,

wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,

36:9 Ay 15:25huwaonyesha yale waliyoyatenda,

kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.

36:10 Ay 33:16; 2Fal 17:13; Ay 5:17Huwafanya wao kusikia maonyo,

na huwaagiza kutubu uovu wao.

36:11 Kut 28:1; Hag 1:12; Isa 1; 19Kama wakitii na kumtumikia,

wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio,

na miaka yao katika utoshelevu.

36:12 Law 26:38; Ay 15:22; 4:21; Efe 4:18Lakini wasiposikiliza,

wataangamia kwa upanga,

nao watakufa pasipo maarifa.

36:13 Ay 15:12; Rum 2:5; Ay 5:2; 4:17; Amo 4:11“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki;

hata anapowafunga, hawamwombi msaada.

36:14 Kum 23:17Wanakufa wangali vijana,

miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.

36:15 Ay 5:15; 2Kor 12:10; Ay 33:16; 34:33Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao,

na kuzungumza nao katika dhiki zao.

36:16 Hos 2:14; Za 23:5; 78:19“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki,

ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi,

hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.

36:17 Ay 20:29; 22:11Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu;

hukumu na haki vimekukamata.

36:18 Kut 23:8; Amo 5:12; Ay 34:33Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri;

usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.

36:19 Za 49:6; Yer 9:23Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi

vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?

36:20 Ay 34:20-25Usiutamani usiku uje,

ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.

36:21 Ay 34:33; Za 66:18; Ebr 11:25Jihadhari usigeukie uovu,

ambao unaupenda zaidi kuliko mateso.

36:22 Isa 40:13; Rum 11:34“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake.

Ni nani aliye mwalimu kama yeye?

36:23 Ay 34:10, 13; Rum 11:33; Mwa 18:25; Kum 32:4Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake,

au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?

36:24 1Nya 16:24; Za 35:27; 59:16; Ufu 15:3Kumbuka kuzitukuza kazi zake,

ambazo watu wamezisifu katika wimbo.

36:25 Rum 1:20Wanadamu wote wameiona;

watu wanaikazia macho kwa mbali.

36:26 1Kor 13:12; Mwa 21:33; Ebr 1:12Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu,

kupita ufahamu wetu!

Hesabu ya miaka yake haitafutiki.

36:27 2Sam 1:21; Za 147:8“Yeye huvuta juu matone ya maji,

ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;

36:28 Ay 22:11; Mt 5:45mawingu huangusha chini maji yake,

nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.

36:29 Mit 8:28; Isa 40:22Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu,

jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.

36:30 Kut 19:16; Yer 10:13; Hab 3:11; Isa 51:10; Za 18:12, 14; 97:4Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka,

naye huvifunika vilindi vya bahari.

36:31 1Fal 17:1; Amo 4:7-8; Isa 30:23; Mdo 14:17Hivi ndivyo atawalavyo mataifa,

na kuwapa chakula kwa wingi.

36:32 Ay 28:24; Za 18:14Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi,

na kuuagiza kulenga shabaha yake.

Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja;

hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.36:33 Au: hutangaza kuja kwake.

Read More of Ayubu 36

Ayubu 37:1-24

37:1 Za 38:10; Isa 15:5; Yer 4:19; Hab 3:16“Kwa hili moyo wangu unatetemeka,

nao unaruka kutoka mahali pake.

37:2 Za 18:13; 29:3-9Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake,

sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake.

37:3 2Sam 22:13; Za 18:14; Ay 36:32; Mt 24:27; Lk 17:24Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote

na kuupeleka hata miisho ya dunia.

37:4 1Sam 2:10; Kut 20:19Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake;

Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari.

Wakati sauti yake ingurumapo tena,

huuachilia umeme wake wa radi.

37:5 Ay 11:7-9Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu;

yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.

37:6 Kum 28:12; Ay 38:22; Mwa 7:4; Ay 36:27Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’

nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’

37:7 Ay 12:14; Za 111:2; 109:27; 104:19-23Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake,

yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.

37:8 Ay 28:26; 38:40; Za 104:22Wanyama hujificha;

hubakia kwenye mapango yao.

37:9 Za 50:3; 147:17Dhoruba hutoka katika chumba chake,

baridi hutoka katika upepo uendao kasi.

37:10 Ay 38:29-30; Za 147:17Pumzi ya Mungu hutoa barafu,

eneo kubwa la maji huganda.

37:11 Ay 26:8; 36:30; 28:26Huyasheheneza mawingu kwa maji,

naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.

37:12 Za 147:16; 148:8; Ay 37:3Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake,

juu ya uso wa dunia yote,

kufanya lolote ayaamuruyo.

37:13 Kut 9:22-23; 1Sam 12:17; Kut 9:18; 1Fal 18:45Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu,

au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.

37:14 Ay 32:10; 5:9“Ayubu, sikiliza hili;

nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu.

37:15 Ay 36:30, 32Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu,

na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?

37:16 Ay 36:29; 5:9; 36:4Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia,

hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?

37:17 Mdo 27:13Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako

wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini,

37:18 Mwa 1:1, 8; Ay 22:14; Kum 28:23; Za 104:2je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga,

zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa?

37:19 Rum 8:26; Ay 13:18; 9:3“Tuambieni yatupasayo kumwambia;

hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu.

Je, aambiwe kwamba nataka kuongea?

Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa?

37:21 Amu 5:31; Mdo 22:1; 26:13Basi hakuna awezaye kulitazama jua,

jinsi linavyongʼaa angani,

upepo ukishafagia mawingu.

37:22 Za 19:5; Kut 24:17Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu;

Mungu huja katika utukufu wa kutisha.

37:23 Ay 5:9; Rum 11:33; Ay 8:3; Yer 25:5; Mao 3:33Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza;

katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.

37:24 Mik 6:8; Mt 10:28; 11:25; Efe 5:15Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni,

kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”

Read More of Ayubu 37