Ayubu 19:1-29
Hotuba Ya Sita Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Najua Mkombozi Wangu Yu Hai
Ndipo Ayubu akajibu:
19:2 1Sam 1:6; Za 6:2, 3; Ay 6:9; 13:25“Je, mtaendelea kunitesa mpaka lini,
na kuniponda kwa maneno yenu?
19:3 Mwa 31:7; Ay 20:3Mara kumi hizi mmenishutumu;
bila aibu mnanishambulia.
19:4 Ay 6:24; Za 19:12; Eze 18:4Kama ni kweli nimepotoka,
kosa langu ninabaki kuhusika nalo mwenyewe.
19:5 Za 38:16; 55:12; Mik 7:8Kama kweli mngejitukuza wenyewe juu yangu,
na kutumia unyonge wangu dhidi yangu,
19:6 Ay 6:29; 18:8; 10:3basi jueni kuwa Mungu amenitendea yaliyo mabaya,
naye amekokota wavu wake kunizunguka.
19:7 Ay 9:24; 30:20; Za 22:2; Hab 1:2-4“Ingawa ninalia, ‘Nimetendewa mabaya!’ sipati jibu;
ingawa ninaomba msaada, hakuna haki.
19:8 Mao 3:7; Hos 2:6; Mhu 6:4; Yer 14:19Yeye ameizuia njia yangu hivyo siwezi kupita;
ameyafunika mapito yangu na giza.
19:9 Ay 12:17; Za 89:39-44; Mao 5:16Amenivua heshima yangu,
na kuniondolea taji kichwani pangu.
19:10 Ay 12:14; 7:6; 14:7Amenibomoa kila upande hadi nimeisha;
amelingʼoa tegemeo langu kama mti.
19:11 Ay 16:9; 13:14Hasira yake imewaka juu yangu;
amenihesabu kuwa miongoni mwa adui zake.
19:12 Ay 16:13; 16:10; 3:23Majeshi yake yananisogelea kwa nguvu;
yamenizingira,
yamepiga kambi kulizunguka hema langu.
19:13 Ay 16:10-13; 30:12; Mt 26:56; 2Tim 4:16“Amewatenga ndugu zangu mbali nami;
wale tunaojuana nao wamefarakana nami kabisa.
19:14 Ay 19:19; 2Sam 15:12; Ay 12:4; 16:20; Za 88:18; Yer 20:10; 38:22Watu wa jamaa yangu wamekwenda mbali;
rafiki zangu wamenisahau.
19:15 Mwa 14:14; Mhu 2:7Wageni wangu na watumishi wangu wa kike wananiona kama mgeni;
wananitazama kama mgeni.
Namwita mtumishi wangu, wala haitiki,
ingawa namwomba kwa kinywa changu mwenyewe.
19:17 Za 38:5Pumzi ya kinywa changu ni kinyaa kwa mke wangu;
nimekuwa chukizo mno kwa ndugu zangu mwenyewe.
19:18 2Fal 2:23; Ay 13:25Hata watoto wadogo hunidhihaki;
ninapojitokeza, hunifanyia mzaha.
19:19 Za 38:11; 55:12-13; Ay 3:10Rafiki zangu wa moyoni wote wananichukia kabisa;
wale niwapendao wamekuwa kinyume nami.
19:20 Ay 2:5Mimi nimebaki mifupa na ngozi tu;
nimeponea nikiwa karibu kufa.
19:21 Ay 6:14; Amu 2:15; Ay 4:5; 10:3; Mao 3:1“Nihurumieni, rafiki zangu, kuweni na huruma,
kwa kuwa mkono wa Mungu umenipiga.
19:22 Ay 13:25; 16:11; Mit 30:14; Isa 53:4Kwa nini mnanifuatia kama Mungu afanyavyo?
Hamtosheki kamwe na mwili wangu?
19:23 Kut 17:16; Isa 30:8“Laiti maneno yangu yangewekwa kwenye kumbukumbu,
laiti kwamba yangeandikwa kwenye kitabu,
19:24 Yer 17:1; Ay 16:18kwamba yangechorwa kwenye risasi kwa kifaa cha chuma,
au kuyachonga juu ya mwamba milele!
19:25 Law 25:25; Mit 23:11; 1Sam 14:39; Ay 16:19Ninajua kwamba Mkombozi19:25 Au: Mtetezi. wangu yu hai,
naye kwamba mwishoni atasimama juu ya nchi.
19:26 Hes 12:8; 1Yn 3:2Nami baada ya ngozi yangu kuharibiwa,
bado nikiwa na mwili huu nitamwona Mungu;
19:27 Lk 2:30; Za 42:1; 63:1; 54:2mimi nitamwona kwa macho yangu mwenyewe:
mimi, wala si mwingine.
Tazama jinsi moyo wangu unavyomtamani sana!
“Kama mkisema, ‘Tazama tutakavyomwinda,
maadamu mzizi wa tatizo uko ndani yake,’
19:29 Ay 15:22; Za 58:11; Mhu 12:14ninyi wenyewe uogopeni upanga,
kwa kuwa ghadhabu italeta adhabu kwa upanga,
nanyi ndipo mtakapojua kwamba kuna hukumu.”
Ayubu 20:1-29
Sofari Anasema: Uovu Hupokea Malipo Ya Haki
20:1 Ay 2:11Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:
20:2 Za 42:5; Mao 1:20“Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu,
kwa sababu nimehangaika sana.
20:3 Ay 19:3Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima,
nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu.
20:4 Kum 4:32; Ay 32:7“Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani,
tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
20:5 Ay 8:12; Za 73:19; 37:35macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi,
nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
20:6 Ay 33:17; Isa 16:6; Mwa 11:4; Isa 14:13-14; Oba 1:3-4Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni
na kichwa chake hugusa mawingu,
20:7 Ay 4:20; 7:8; 14:20ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe.
Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
20:8 Za 90:5; 73:20; Mhu 6:12; 12:7; Ay 18:11-18; Isa 17:14; 29:7Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena,
amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
20:9 Ay 7:8Jicho lililomwona halitamwona tena;
mahali pake hapatamwona tena.
20:10 Ay 5:4; 20:15, 18, 20; 3:15Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini,
nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.
20:11 Ay 13:26; 21:24; 17:16Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake,
zitalala naye mavumbini.
20:12 Ay 15:16; Za 10:7; 140:3“Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake
naye huuficha chini ya ulimi wake,
20:13 Hes 11:18-20ingawa hawezi kukubali kuuachia uende,
lakini huuweka kinywani mwake.
20:14 Za 104:26; Ay 10:18; Mwa 1:21; Ay 41:1, 8, 10, 2520:14 Mit 20:17; Yer 2:19; 4:18; Ufu 10:9; Hes 21:6Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake,
nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
20:15 Ay 20:10; Law 18:25Atatema mali alizozimeza;
Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
20:16 Kum 32:24, 34Atanyonya sumu za majoka;
meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
20:17 Kum 32:13-14; Ay 29:6; Yer 17:6Hatafurahia vijito,
mito inayotiririsha asali na siagi.
20:18 Ay 20:10; 5:5; Za 109:11Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila;
hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
20:19 Kum 15:11; Amo 8:4Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu;
amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
20:20 Mhu 5:12-14“Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana;
hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
20:21 Ay 7:8Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale;
kufanikiwa kwake hakutadumu.
20:22 Amu 2:15; Lk 2:16-20; Ay 20:29; 21:17, 30; 31:2-3Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata;
taabu itamjia kwa nguvu zote.
20:23 Za 78:30-31Atakapokuwa amelijaza tumbo lake,
Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake,
na kumnyeshea mapigo juu yake.
20:24 Yer 46:21; Amo 5:19; Isa 24:18Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma,
mshale wa shaba utamchoma.
20:25 Ay 18:11; 16:13; Za 88:15-16Atauchomoa katika mgongo wake,
ncha ingʼaayo kutoka ini lake.
Vitisho vitakuja juu yake;
20:26 Ay 5:14; 1:16; 15:34; 26:6; 28:22; 31:12; Za 21:9giza nene linavizia hazina zake.
Moto usiopepewa na mtu utamteketeza,
na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
20:27 Kum 31:28; Isa 26:21Mbingu zitaweka wazi hatia yake,
nayo nchi itainuka kinyume chake.
20:28 Kum 28:31; Mt 7:26-27; Hes 14:28-32; Efe 5:6Mafuriko yataichukua nyumba yake,
maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
20:29 Yer 13:25; Kum 29:20, 28; Ufu 21:8; Mt 24:51Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu,
urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”
Ayubu 21:1-34
Hotuba Ya Saba Ya Ayubu
Ayubu Anajibu: Waovu Mara Nyingi Huenda Bila Kuadhibiwa
Ndipo Ayubu akajibu:
21:2 Ay 13:17; 21:34“Yasikilizeni maneno yangu kwa makini;
hii na iwe faraja mnayonipa mimi.
21:3 Ay 6:14; 11:3; 16:10Nivumilieni ninapozungumza,
nami nikishazungumza, endeleeni kunidhihaki.
21:4 Za 22:1-3; Ay 6:3, 11; 1Sam 1:16“Je, kwani malalamiko yangu yanaelekezwa kwa mwanadamu?
Kwa nini nisikose subira?
21:5 Amu 18:19; Ay 40:4Niangalieni mkastaajabu;
mkaweke mkono juu ya vinywa vyenu.
21:6 Mwa 45:3; Ay 4:14Ninapowaza juu ya hili, ninaogopa,
nao mwili wangu unatetemeka.
21:7 Mhu 7:15; Mal 3:15; Yer 12:1-3Kwa nini waovu wanaendelea kuishi,
wakifikia umri wa uzee na kuendelea kuwa na nguvu?
21:8 Za 17:14; Mal 3:15Huwaona watoto wao wakithibitika
wakiwa wamewazunguka,
wazao wao mbele za macho yao.
21:9 Ay 5:24; Za 73:5Nyumba zao zi salama wala hakuna hofu;
fimbo ya Mungu haiko juu yao.
21:10 Kut 23:26Madume yao ya ngʼombe huvyaza bila kushindwa kamwe;
ngʼombe wao huzaa wala hawaharibu mimba.
21:11 Za 78:52; 107:41Huwatoa watoto wao nje kama kundi;
wadogo wao huchezacheza.
21:12 1Nya 15:16; Mt 15:17Huimba nyimbo kwa matari na kwa kinubi,
nao huifurahia sauti ya filimbi.
21:13 Ay 24:19; Za 49:14; Isa 14:15; Ay 3:13Huitumia miaka yao katika mafanikio
nao hushuka kaburini kwa amani.
21:14 Ay 4:17; Kum 32:15; Isa 30:11; 1Sam 11:15Lakini humwambia Mungu, ‘Tuache sisi!’
Hatuna haja ya kufahamu njia zako.
21:15 Yer 9:6; Mal 3:14Mwenyezi ni nani hata tumtumikie?
Tutapata faida gani kumwomba?
21:16 Ay 22:18; Za 1:1; 26:5; 36:1Lakini kufanikiwa kwao hakupo mikononi mwao wenyewe,
hivyo najitenga mbali na shauri la waovu.
21:17 Ay 18:5; 18:12; 20:22, 28“Lakini ni mara ngapi taa ya waovu huzimwa?
Ni mara ngapi maafa huwajia,
yale yawapatayo ambayo Mungu
huwapangia katika hasira yake?
21:18 Ay 13:15; Mwa 19:15; Ay 7:10; Mit 10:25; Mwa 7:23Ni mara ngapi huwa kama majani makavu mbele ya upepo,
kama makapi yachukuliwayo na dhoruba?
21:19 Kut 20:5; Yn 9:2Imesemekana, ‘Mungu huiweka akiba adhabu ya mtu
kwa ajili ya wanawe.’
Mungu na amlipe mtu mwenyewe,
ili apate kulijua!
21:20 Ay 6:4; Isa 51:17; Yer 25:15; Ufu 14:10Macho yake mwenyewe na yaone maangamizi yake;
yeye na ainywe ghadhabu ya Mwenyezi.
21:21 Ay 14:22; 14:5; 14:21; Mhu 9:5-6Kwani anajali nini kuhusu jamaa anayoiacha nyuma,
miezi yake aliyopangiwa ifikapo mwisho?
21:22 Za 94:12; 86:8; Rum 11:34“Je, yuko mtu yeyote awezaye kumfundisha Mungu maarifa,
iwapo yeye ndiye ahukumuye hata walio juu ya wote?
21:23 Mwa 15:15; Ay 13:26; 3:13Mtu mmoja hufa akiwa na nguvu zake kamili,
akiwa salama na mwenye raha kamili,
21:24 Mit 3:8mwili wake ukiwa umenawiri,
nayo mifupa yake ikiwa imejaa mafuta ndani yake.
21:25 Ay 10:1Mtu mwingine hufa katika uchungu wa nafsi,
akiwa hajafurahia kamwe jambo lolote zuri.
21:26 Mhu 9:2-3; Isa 14:11Hao wote hulala mavumbini,
nao mabuu huwafunika wote.
“Ninayajua kikamilifu yale mnayoyafikiri,
mipango ambayo kwayo mngenitendea mabaya.
21:28 Ay 1:3; 12:21; 29:25; 31:37; 8:22Mwasema, ‘Iko wapi sasa nyumba ya huyo mtu mkuu,
mahema ambayo watu waovu walikaa?’
Je, hamkuwahi kuwauliza hao wanaosafiri?
Je, hamkutafakari taarifa zao:
21:30 Ay 31:3; Mit 16:4; Isa 5:30; Rum 5:2kwamba mtu mwovu huepushwa kutoka siku ya maafa,
kwamba huokolewa kutoka siku ya ghadhabu?
21:31 Ay 34:11; Za 62:12; Mit 24:11-12; Isa 59:18Ni nani hulaumu matendo yake mbele ya uso wake?
Ni nani ampatilizaye kwa yale aliyoyatenda?
21:32 Isa 14:18Hupelekwa kaburini,
nao ulinzi ukawekwa kwenye kaburi lake.
21:33 Ay 3:17-19; 17:16; 24:24Udongo ulio bondeni ni mtamu kwake;
watu wote watamfuata,
nao umati wa watu usiohesabika umemtangulia.
“Hivyo ninyi mnawezaje kunifariji kwa upuzi wenu?
Hakuna kilichosalia cha majibu yenu isipokuwa uongo!”