Yeremia 23:9-40, Yeremia 24:1-10, Yeremia 25:1-14 NEN

Yeremia 23:9-40

Manabii Wasemao Uongo

23:9 Hab 3:16; Yer 20:8-9; 4:19; Ay 4:14Kuhusu manabii:

Moyo wangu umevunjika ndani yangu;

mifupa yangu yote inatetemeka.

Nimekuwa kama mtu aliyelewa,

kama mtu aliyelemewa na divai,

kwa sababu ya Bwana

na maneno yake matakatifu.

23:10 Za 107:34; Yer 9:2, 10; 4:26; Hos 4:2-3; Kum 28:23-24; Yer 12:11Nchi imejaa wazinzi;

kwa sababu ya laana, nchi imekauka

na malisho yaliyoko nyikani yamekauka.

Mwenendo wa manabii ni mbaya

na mamlaka yao si ya haki.

23:11 Yer 6:13; Sef 3:4; 2Fal 21:4; Yer 8:10; 7:10“Nabii na kuhani wote si wacha Mungu;

hata hekaluni mwangu ninaona uovu wao,”

asema Bwana.

23:12 Ay 3:23; Za 35:6; Mit 4:19; Yer 11:23; Kum 32:35; Yer 13:16“Kwa hiyo mapito yao yatakuwa utelezi,

watafukuziwa mbali gizani

na huko wataanguka.

Nitaleta maafa juu yao

katika mwaka wa kuadhibiwa kwao,”

asema Bwana.

23:13 1Fal 18:18-22; Isa 9:16; 3:12; Eze 13:10“Miongoni mwa manabii wa Samaria

nililiona jambo la kuchukiza:

Walitabiri kwa Baali

na kuwapotosha Israeli watu wangu.

23:14 Yer 5:30; Hos 6:10; Yer 29:23; Eze 13:22; Mt 11:24; Isa 1:9-10; Amo 4:11; Isa 5:18Nako miongoni mwa manabii wa Yerusalemu

nimeona jambo baya sana:

Wanafanya uzinzi

na kuenenda katika uongo.

Wanatia nguvu mikono ya watenda mabaya,

kwa ajili hiyo hakuna yeyote

anayeachana na uovu wake.

Wote wako kama Sodoma kwangu;

watu na Yerusalemu wako kama Gomora.”

23:15 Yer 8:14; 9:15; 8:10Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo kuhusu manabii:

“Nitawafanya wale chakula kichungu

na kunywa maji yaliyotiwa sumu,

kwa sababu kutokana na manabii wa Yerusalemu

kutokumcha Mungu kumeenea katika nchi yote.”

23:16 Yer 27:9-14; Mt 7:15; Mit 19:27; Eze 13:3; Yer 14:14; 9:20Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Msisikilize wanachowatabiria manabii,

wanawajaza matumaini ya uongo.

Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,

hayatoki katika kinywa cha Bwana.

23:17 Yer 13:10; 8:11; Amo 9:10; Mik 3:11; 1Fal 22:8; Yer 4:10; 5:12Huendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,

Bwana asema: Mtakuwa na amani.’

Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,

wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’

23:18 1Fal 22:19; Rum 11:34Lakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Bwana

ili kuona au kusikia neno lake?

Ni nani aliyesikiliza

na kusikia neno lake?

23:19 Isa 30:30; Yer 30:23; 25:32; Zek 7:14Tazama, dhoruba ya Bwana

itapasuka kwa ghadhabu,

kisulisuli kitazunguka na kuanguka

vichwani vya waovu.

23:20 2Fal 23:26-27; Yer 30:24; 4:28Hasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.

Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.

23:21 Yer 14:14; 27:15Mimi sikuwatuma manabii hawa,

lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.

Mimi sikusema nao,

lakini wametabiri.

23:22 2Fal 17:13; Kum 33:10; 2Fal 17:13; Yer 25:5; Amo 3:7Lakini kama wangesimama barazani mwangu,

wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,

nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya

na kutoka matendo yao maovu.”

23:23 Za 139:1-10; 1Fal 20:23-28“Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”

Bwana asema,

“wala si Mungu aliyeko pia mbali?

23:24 Ay 11:20; 1Fal 8:27; Ebr 4:13; Mwa 3:8; Ay 22:12-14; Mhu 12:14; Isa 28:15; 1Kor 4:5Je, mtu yeyote aweza kujificha

mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”

Bwana asema.

“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”

Bwana asema.

23:25 Yer 14:14; 27:10; 29:8; Kum 13:1“Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ 23:26 Isa 30:10; 1Tim 4:1-2; Eze 13:2; Yer 14:14Mambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? 23:27 Kum 13:13; Yer 29:8; Amu 3:7; 8:33-34; Mdo 13:8; Yer 2:23Wanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali. 23:28 1Sam 3:17Mwache nabii aliye na ndoto aseme ndoto yake, lakini yule aliye na neno langu na aliseme kwa uaminifu. Kwa maana jani kavu lina uhusiano gani na ngano?” asema Bwana. 23:29 Za 39:3; 1Kor 3:13; 1Pet 4:10; Yer 5:14; Ebr 4:12“Je, neno langu si kama moto,” asema Bwana, “na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?

23:30 Za 34:16; Kum 18:20; Yer 21:13; 14:15“Kwa hiyo, niko kinyume na manabii wanaoibiana maneno kana kwamba ni yangu,” asema Bwana. “Naam, mimi niko kinyume na manabii wanaotikisa ndimi zao wenyewe na kusema, ‘Bwana asema.’ 23:32 Mao 2:14; Sef 3:4; Yer 7:8; 50:6; Ay 13:4; Eze 13:3; 22:28; Yer 14:14Kweli, niko kinyume na hao wanaotabiri ndoto za uongo,” asema Bwana. “Wanazisimulia na kuwapotosha watu wangu kwa uongo wao bila kujali, lakini sikuwatuma wala sikuwaamuru. Hawawafaidi watu hawa hata kidogo,” asema Bwana.

Maneno Ya Uongo Na Manabii Wa Uongo

23:33 2Fal 21:14; Yer 17:15; Mal 1:1“Wakati watu hawa, au nabii, au kuhani watakapokuuliza, ‘Mzigo wa Bwana ni nini?’ wewe utawaambia, ‘Ninyi ndio mzigo. Nami nitawavua kama vazi, asema Bwana.’ 23:34 Mao 2:14; Zek 13:3Nabii, kuhani, au mtu yeyote akisema, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ nitamwadhibu huyo na nyumba yake. 23:35 Yer 33:3; 42:4Hivyo mnaambiana kila mmoja na mwenzake, au kwa mtu wa nyumba yao: ‘Bwana amejibu nini?’ au ‘Bwana amesema nini?’ 23:36 Gal 1:7-8; 2Pet 3:16; Yos 3:10Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa Bwana,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu. Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘Bwana amekujibu nini?’ au ‘Je, Bwana amesema nini?’ Ingawa unadai, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ hili ndilo Bwana asemalo: Ulitumia maneno, ‘Huu ndio mzigo wa Bwana,’ hata ingawa nilikuambia kuwa kamwe usiseme, ‘Huu ni mzigo wa Bwana.’ 23:39 Yer 7:15Kwa hiyo, hakika nitakusahau na kukutupa mbali na uso wangu pamoja na mji niliowapa ninyi na baba zenu. 23:40 Yer 20:11; Eze 5:14-15Nitaleta juu yako fedheha ya kudumu: yaani aibu ya kudumu ambayo haitasahaulika.”

Read More of Yeremia 23

Yeremia 24:1-10

Vikapu Viwili Vya Tini

24:1 2Fal 24:16; 2Nya 36:9; Kut 23:19; Kum 26:2; Amo 8:1-2Baada ya Yekonia24:1 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, Bwana akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Bwana. 24:2 Wim 2:13; Isa 5:4Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza. Kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbovu mno zisizofaa kuliwa.

24:3 Yer 1:11; Amo 8:1-2Kisha Bwana akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?”

Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu ni mbovu mno zisizofaa kuliwa.”

Kisha neno la Bwana likanijia: 24:5 Yer 29:4, 20“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo. 24:6 Kum 30:3; Eze 11:17; Yer 42:10; 30:9; Amo 9:14-15Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa, 24:7 Law 26:12; Ebr 8:10; Yer 32:40; 2Nya 6:37; Eze 11:19; Isa 11:9; 51:18; Zek 2:11nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.

24:8 Yer 29:17; 39:6-9; 44:26; 46:14; 32:4-5; 44:30“ ‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbovu mno zisizofaa kuliwa,’ asema Bwana, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, wawe wamebaki katika nchi hii, au wanaishi Misri. 24:9 Yer 25:18; 34:17; Kum 28:25; 2Fal 22:19; Yer 29:18; Dan 9:7; Yer 15:4Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia. 24:10 Isa 51:19; Ufu 6:8; Yer 27:8; 9:16; 15:2; Kum 28:21Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao hadi wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’ ”

Read More of Yeremia 24

Yeremia 25:1-14

Miaka Sabini Ya Kuwa Mateka

25:1 2Fal 24:2; Yer 46:2Neno likamjia Yeremia kuhusu watu wote wa Yuda, katika mwaka wa nne wa utawala wa Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kwanza wa utawala wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. 25:2 Yer 18:11Hivyo nabii Yeremia akawaambia watu wote wa Yuda na wale wote waishio Yerusalemu: 25:3 1Nya 3:14; Yer 11:7; 26:5; 7:26; Isa 65:12Kwa miaka ishirini na mitatu, kuanzia mwaka wa kumi na tatu wa utawala wa Yosia mwana wa Amoni mfalme wa Yuda, hadi siku hii ya leo, neno la Bwana limekuwa likinijia, nami nimesema nanyi mara kwa mara, lakini hamkusikiliza.

25:4 Yer 6:17; 29:19; 7:25-26Ingawa Bwana amewatuma watumishi wake wote hao manabii kwenu mara kwa mara, hamkusikiliza wala hamkujali. Walisema, “Geukeni sasa, kila mmoja wenu kutoka njia yake mbaya na matendo yake maovu, ndipo mtaweza kukaa katika nchi ambayo Bwana aliwapa ninyi na baba zenu milele. 25:6 Kut 20:3; Kum 8:19Msiifuate miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu. Msinikasirishe kwa vitu ambavyo mmevitengeneza kwa mikono yenu.”

25:7 Kum 32:21; 2Fal 17:20; Yer 7:19“Lakini ninyi hamkunisikiliza mimi, tena mkanikasirisha kwa vitu mlivyovitengeneza kwa mikono yenu, nanyi mmejiletea madhara juu yenu wenyewe,” asema Bwana.

Kwa hiyo Bwana Mwenye Nguvu Zote asema hivi: “Kwa sababu hamkuyasikiliza maneno yangu, 25:9 Isa 13:3-5; 14:31; 41:2; 2Nya 29:8; Yer 18:16; Hes 21:2; Eze 12:20nitayaita mataifa yote ya kaskazini na mtumishi wangu Nebukadneza mfalme wa Babeli,” asema Bwana. “Nitawaleta waishambulie nchi hii na wakazi wake wote, na dhidi ya mataifa yote yanayowazunguka. Nitawaangamiza kabisa na kuwafanya kitu cha kuchukiwa na kudharauliwa, na kuwa magofu daima. 25:10 Isa 24:8; Eze 26:13; Yer 7:34; Mhu 12:3-4; Mao 5:15; Ufu 18:22-23; 15:5Nitawaondolea sauti ya shangwe na furaha, sauti ya bibi na bwana arusi, sauti ya mawe ya kusagia, na mwanga wa taa. 25:11 Law 26:31-32; Yer 12:11-12; 28:14; 4:26-27; 2Nya 36:21Nchi hii yote itakuwa ukiwa na isiyofaa kitu, nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.”

25:12 Yer 27:7; 29:10; Isa 13:19-22; 14:22-23; Mwa 10:10; Za 137:8“Lakini miaka sabini itakapotimia, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na taifa lake na nchi ya Wakaldayo kwa ajili ya hatia yao,” asema Bwana. “Nitaifanya kuwa ukiwa milele. 25:13 Isa 30:8Nitaleta juu ya nchi hiyo mambo yote niliyosema dhidi yake, yote yaliyoandikwa katika kitabu hiki, na kutolewa unabii na Yeremia dhidi ya mataifa yote. 25:14 Isa 14:6; Yer 50:19; 51:27-28; Ay 21:19; Yer 27:7Wao wenyewe watakuwa watumwa wa mataifa mengi na wafalme wakuu. Nitawalipizia sawasawa na matendo yao na kazi ya mikono yao.”

Read More of Yeremia 25