Yeremia 21:1-14, Yeremia 22:1-30, Yeremia 23:1-8 NEN

Yeremia 21:1-14

Mungu Anakataa Ombi La Sedekia

21:1 2Fal 24:18; 1Nya 9:12; 2Fal 25:18; Yer 37:3; 52:1Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Bwana wakati Mfalme Sedekia alipowatuma Pashuri mwana wa Malkiya, na kuhani Sefania mwana wa Maaseya kwake, kusema: 21:2 Mwa 25:22; Yer 32:5; Za 44:1-4; Yer 32:17; Kut 9:28; 2Fal 22:18; Mwa 10:10“Tuulizie sasa kwa Bwana, kwa sababu Nebukadneza mfalme wa Babeli anatushambulia. Labda Bwana atatenda maajabu kwa ajili yetu kama nyakati zilizopita, ili Nebukadneza atuondokee.”

Lakini Yeremia akawajibu, “Mwambieni Sedekia, 21:4 Yer 32:5; 37:8-10; Isa 13:4‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: Ninakaribia kuwageuzia silaha za vita zilizo mikononi mwenu, ambazo mnatumia kupigana na mfalme wa Babeli na Wakaldayo ambao wako nje ya ukuta wakiwazunguka kwa jeshi. Nami nitawakusanya ndani ya mji huu. 21:5 2Fal 22:13; Yer 6:12; Kut 6:6; 3:20; Yos 10:14; Eze 5:8Mimi mwenyewe nitapigana dhidi yenu kwa mkono wangu ulionyooshwa na mkono wa nguvu, kwa hasira na ghadhabu kali na ukali mwingi. 21:6 Yer 14:12; 7:20Nitawaangamiza waishio katika mji huu, watu na wanyama, nao watauawa kwa tauni ya kutisha. 21:7 Eze 12:14; 2Nya 36:10; Eze 29:19; Hab 1:6; Yer 39:5; 2Fal 25:7; Yer 52:9; 27:6Baada ya hayo, nitamtia Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na watu wa mji huu ambao walinusurika tauni, upanga na njaa, mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na kwa adui zao wale wanaotafuta uhai wao. Atawaua kwa upanga; hatakuwa na rehema juu yao au huruma wala kuwasikitikia,’ asema Bwana.

“Zaidi ya hayo, waambie watu hawa, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Tazama, naweka mbele yenu njia ya uzima, na njia ya mauti. 21:9 Yer 14:12; Eze 5:12; Yer 39:18; 45:5; 27:11; 40:9; 39:18Yeyote atakayekaa katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa au tauni. Lakini yeyote atakayetoka na kujisalimisha kwa Wakaldayo ambao wameuzunguka mji huu kwa jeshi, atanusurika, naye ataishi. 21:10 Yer 20:4; Amo 9:4; Yer 22:3; Isa 1:31; 42:25Nimekusudia kuufanyia mji huu jambo baya, wala si jema. Utatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteketeza kwa moto, asema Bwana.’

21:11 Yer 13:18“Zaidi ya hayo, ambia nyumba ya mfalme ya Yuda, ‘Sikia neno la Bwana, 21:12 Kut 22:22; Yer 22:3; Isa 1:31; 42:25Ewe nyumba ya Daudi, hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Hukumuni kwa haki kila asubuhi,

mwokoeni mikononi mwa mdhalimu

yeye aliyetekwa nyara,

la sivyo ghadhabu yangu italipuka

na kuwaka kama moto

kwa sababu ya uovu mlioufanya:

itawaka na hakuna wa kuizima.

21:13 Nah 2:13; Eze 5:8; 2Sam 5:6-7; Oba 1:3-4; Yer 49:4; 23:30; 50:31; 51:25Niko kinyume nawe, ee Yerusalemu,

wewe uishiye juu ya bonde hili

kwenye uwanda wa juu wa miamba,

asema Bwana,

wewe usemaye, “Ni nani awezaye kuja kinyume chetu?

Nani ataingia mahali pa kimbilio letu?”

21:14 Mit 1:31; Isa 3:10-11; 2Nya 36:19; 2Fal 19:23; Mao 2:3; Eze 20:47; Yer 17:10Nitawaadhibu kama istahilivyo matendo yenu,

asema Bwana.

Nitawasha moto katika misitu yenu

ambao utateketeza kila kitu kinachowazunguka.’ ”

Read More of Yeremia 21

Yeremia 22:1-30

Hukumu Dhidi Ya Wafalme Waovu

Hili ndilo asemalo Bwana: “Shuka kwenye jumba la kifalme la mfalme wa Yuda, utangaze ujumbe huu huko: 22:2 Lk 1:32; Amo 7:16‘Sikia neno la Bwana, ee mfalme wa Yuda, wewe uketiye kwenye kiti cha enzi cha Daudi: wewe, maafisa wako na watu wako mnaopitia malango haya. 22:3 Law 25:17; Hos 12:6; Yer 21:12; Za 72:4; Isa 1:17; Amo 5:24; Eze 33:14; Mik 6:8Hili ndilo Bwana asemalo: Tenda haki na adili. Mwokoe mkononi mwa mdhalimu yeye aliyetekwa nyara. Usimtendee mabaya wala ukatili mgeni, yatima au mjane, wala usimwage damu isiyo na hatia mahali hapa. 22:4 Yer 17:25Kwa kuwa ukiwa mwangalifu kushika maagizo haya, ndipo wafalme watakaokalia kiti cha enzi cha Daudi watakapoingia kupitia malango ya jumba hili la kifalme, wakiwa wamepanda magari na farasi, huku wakifuatana na maafisa wao na watu wao. 22:5 Yer 17:25; Mwa 22:16; Ebr 6:13Lakini kama hutayatii maagizo haya, asema Bwana, ninaapa kwa nafsi yangu kwamba jumba hili litakuwa gofu.’ ”

22:6 Mik 3:12; Mwa 31:21; Wim 4:1; Isa 33:9; 1Fal 7:2Kwa kuwa hili ndilo Bwana asemalo kuhusu jumba la kifalme la mfalme wa Yuda:

“Ingawa uko kama Gileadi kwangu,

kama kilele cha Lebanoni,

hakika nitakufanya uwe kama jangwa,

kama miji ambayo haijakaliwa na watu.

22:7 Yer 6:4; Isa 10:34; Za 74:5; Isa 21:14; Yer 4:7; Zek 11:1; 2Nya 36:16Nitawatuma waharabu dhidi yako,

kila mtu akiwa na silaha zake,

nao watazikata boriti zako nzuri za mierezi

na kuzitupa motoni.

22:8 Kum 29:24-26; 1Fal 9:8-9; Yer 16:10-11“Watu kutoka mataifa mengi watapitia karibu na mji huu na kuulizana, ‘Kwa nini Bwana amefanya jambo la namna hii juu ya mji huu mkubwa?’ 22:9 2Fal 22:17; Yer 16:11; Eze 39:23; 1Fal 9:9Nalo jibu litakuwa: ‘Kwa sababu wameliacha agano la Bwana, Mungu wao, na wameabudu na kuitumikia miungu mingine.’ ”

22:10 Mhu 4:2; Eze 24; 16; Yer 24:9; 29:18; 42:18Usimlilie yeye aliyekufa, wala usimwombolezee;

badala yake, afadhali umlilie kwa uchungu

yule aliyepelekwa uhamishoni,

kwa sababu kamwe hatairudia

wala kuiona tena nchi yake alikozaliwa.

22:11 2Fal 23:30-31; 1Nya 3:15Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Shalumu22:11 Shalumu ndiye pia anaitwa Yehoahazi. mwana wa Yosia, aliyeingia mahali pa baba yake kuwa mfalme wa Yuda, lakini ameondoka mahali hapa: “Yeye kamwe hatarudi tena. 22:12 2Fal 23:34Atafia huko mahali walipompeleka kuwa mateka; hataiona tena nchi hii.”

22:13 Mik 3:10; Hab 2:9; Law 19:13; Yak 5:4; Isa 5:8“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma,

vyumba vyake vya juu kwa udhalimu,

akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo,

bila kuwalipa kwa utumishi wao.

22:14 Isa 5:8-9; 2Sam 7:2; Eze 23:14Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme,

na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’

Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa,

huweka kuta za mbao za mierezi,

na kuipamba kwa rangi nyekundu.

22:15 2Fal 23:25; Za 22:21; Kum 9:7; Yer 3:13; Sef 3:2; Isa 3:10; Za 128:2“Je, inakufanya kuwa mfalme

huko kuongeza idadi ya mierezi?

Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji?

Alifanya yaliyo sawa na haki,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

22:16 Za 72:1-4, 12-13; Yn 8:19; Tit 1:16; Yak 1:22; Za 82:3; Mit 24:23Aliwatetea maskini na wahitaji,

hivyo yeye akafanikiwa katika yote.

Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?”

asema Bwana.

22:17 Eze 19:6; 2Fal 24:4; Isa 56:11; Eze 18:12; Mik 2:2; Kum 28:33“Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu

katika mapato ya udhalimu,

kwa kumwaga damu isiyo na hatia,

kwa uonevu na ukatili.”

Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda:

“Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’

Hawatamwombolezea wakisema:

‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’

22:19 2Fal 24:6; Yer 36:30Atazikwa maziko ya punda:

ataburutwa na kutupwa

nje ya malango ya Yerusalemu.”

22:20 Hes 27:12; Isa 57:13; Za 68:15; Yer 30:14; Eze 16:33-34; Hos 8:9“Panda Lebanoni ukapige kelele,

sauti yako na isikike huko Bashani,

piga kelele toka Abarimu,

kwa kuwa wote waliojiunga nawe wameangamizwa.

22:21 Yer 3:25; 3:13; Sef 3:2; Za 25:7; Zek 7:7; Kum 9:7; Isa 54:4; Yer 7:23-28Nilikuonya wakati ulipojisikia kwamba uko salama,

lakini ulisema, ‘Mimi sitasikiliza!’

Hii imekuwa kawaida yako tangu ujana wako;

hujanitii mimi.

22:22 Yer 7:19; 10:21; Ay 27:21Upepo utawaondoa wachungaji wako wote,

na wale ulioungana nao wataenda uhamishoni.

Kisha utaaibika na kufedheheka

kwa sababu ya uovu wako wote.

Wewe uishiye Lebanoni,

wewe uliyetulia kwenye majengo ya mierezi,

tazama jinsi utakavyoomboleza

maumivu makali yatakapokupata,

maumivu kama yale ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa!

22:24 2Fal 24:6-8; Yer 37:1; Hag 2:23; Mwa 38:18“Hakika kama niishivyo,” asema Bwana, “hata kama wewe, Yekonia22:24 Yekonia au Konia ni jina jingine la Yehoyakini. mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, ungekuwa pete yangu ya muhuri katika mkono wangu wa kuume, bado ningekungʼoa hapo. 22:25 2Fal 24:16; 2Nya 36:10; Yer 34:20Nitakutia mikononi mwa wale wanaotafuta uhai wako, wale unaowaogopa, yaani Nebukadneza mfalme wa Babeli na kwa Wakaldayo. 22:26 1Sam 25:29; Isa 22:17; Eze 19:9-14; 1Fal 2:19; 2Fal 24:8; 2Nya 36:10Nitakutupa mbali wewe na mama aliyekuzaa mwende katika nchi nyingine, ambayo hakuna hata mmoja wenu aliyezaliwa huko, nanyi mtafia huko. Kamwe hamtarudi katika nchi mliyotamani kuirudia.”

22:28 Za 31:12; Hos 8:8; Yer 17:4; 48:38; 2Fal 24:6; Yer 19:10Je, huyu mtu Yekonia ni chungu kilichodharauliwa,

chungu kilichovunjika,

chombo kisichotakiwa na mtu yeyote?

Kwa nini yeye na watoto wake watupwe nje kwa nguvu,

na kutupwa kwenye nchi wasioijua?

22:29 Yer 6:19Ee nchi, nchi, nchi,

sikia neno la Bwana!

22:30 1Nya 3:16-18; Mt 1:12; Yer 10:21; 38:23; 52:10; Ay 18:19; Za 94:20Hili ndilo Bwana asemalo:

“Mwandike huyu mtu kama asiye na mtoto,

mtu ambaye hatafanikiwa maisha yake yote,

kwa maana hakuna mtoto wake atakayefanikiwa,

wala kukaa kwenye kiti cha enzi cha Daudi

wala kuendelea kutawala katika Yuda.”

Read More of Yeremia 22

Yeremia 23:1-8

Tawi La Haki

23:1 Eze 34:1-10; Zek 11:5-7, 15-17; Isa 56:11; Eze 34:31; Yer 10:21; 12:10; 25:36“Ole wao wachungaji wanaoharibu na kutawanya kondoo wa malisho yangu!” asema Bwana. 23:2 Kut 32:34; Yer 21:12; Eze 34:8-10; Yn 10:8; Yer 10:21; 13:20Kwa hiyo hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, analowaambia wachungaji wanaowachunga watu wangu: “Kwa sababu mmelitawanya kundi langu na kuwafukuzia mbali, wala hamkuwatunza, basi mimi nitawaadhibu kwa ajili ya uovu mliofanya,” asema Bwana. 23:3 Isa 11:10-12; Eze 34:11-16; Yer 32:37; 1Fal 8:48“Mimi mwenyewe nitayakusanya mabaki ya kundi langu kutoka nchi zote ambazo nimewafukuzia, nami nitawarudisha katika malisho yao, mahali ambapo watazaa na kuongezeka idadi yao. 23:4 Mwa 48:15; Isa 31:4; Yer 46:26-28; Yn 6:39; Yer 30:10; 31:10Nitaweka wachungaji juu yao ambao watawachunga, nao hawataogopa tena au kutishwa, wala hatapotea hata mmoja,” asema Bwana.

23:5 2Fal 19:26; Eze 17:22; Mwa 18:19; Zek 6:12; Dan 9:24; Isa 4:2Bwana asema, “Siku zinakuja,

nitakapomwinulia Daudi Tawi lenye haki,

Mfalme atakayetawala kwa hekima,

na kutenda lililo haki na sawa katika nchi.

23:6 Kut 23:21; Ezr 9:15; Zek 14:11; 1Kor 1:30; Law 25:18; Kum 32:8; Hos 2:8; Yer 33:16; Rum 3:21-22; Isa 42:6Katika siku zake, Yuda ataokolewa

na Israeli ataishi salama.

Hili ndilo jina atakaloitwa:

Bwana Haki Yetu.

23:7 Kum 15:15; Yer 16:14; 30:3“Hivyo basi, siku zinakuja, wakati ambapo watu hawatasema tena, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewapandisha Waisraeli kutoka Misri,’ 23:8 Eze 34:13; Isa 43:5-6; Yer 30:10; Eze 20:42; Amo 9:14-15bali watasema, ‘Hakika kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wazao wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote alizokuwa amewafukuzia,’ asema Bwana. Ndipo wataishi katika nchi yao wenyewe.”

Read More of Yeremia 23