Yeremia 14:1-22, Yeremia 15:1-21 NEN

Yeremia 14:1-22

Ukame, Njaa Na Upanga

Hili ndilo neno la Bwana kwa Yeremia kuhusu ukame:

14:2 Isa 3:26; Yer 8:21; Mit 21:13“Yuda anaomboleza,

miji yake inayodhoofika;

wanaomboleza kwa ajili ya nchi,

nacho kilio kinapanda kutoka Yerusalemu.

14:3 Kum 28:48; 2Fal 18:31; 2Sam 15:30; Es 6:12; Ay 6:19-20Wakuu wanawatuma watumishi wao maji;

wanakwenda visimani

lakini humo hakuna maji.

Wanarudi na vyombo bila maji;

wakiwa na hofu na kukata tamaa,

wanafunika vichwa vyao.

14:4 Amo 4:8; Zek 14:17; Yer 3:3; 12:11Ardhi imepasuka nyufa

kwa sababu hakuna mvua katika nchi;

wakulima wana hofu

na wanafunika vichwa vyao.

14:5 Isa 15:6Hata kulungu mashambani

anamwacha mtoto wake aliyezaliwa wakati huo huo

kwa sababu hakuna majani.

14:6 Ay 39:5-6; Yer 2:24; Za 104:11; Mwa 47:4Punda-mwitu wanasimama juu ya miinuko iliyo kame

na kutweta kama mbweha;

macho yao yanakosa nguvu za kuona

kwa ajili ya kukosa malisho.”

14:7 Isa 3:9; Hos 5:5; Yer 2:19; 8:14; Za 25:11; 79:9; 1Sam 12:22Ingawa dhambi zetu zinashuhudia juu yetu,

Ee Bwana, tenda jambo kwa ajili ya jina lako.

Kwa kuwa kukengeuka kwetu ni kukubwa,

nasi tumetenda dhambi dhidi yako.

14:8 Za 9:18; Mdo 28:20; Yer 17:13; 50:7; Za 18:46; Isa 25:9Ee Tumaini la Israeli,

Mwokozi wake wakati wa taabu,

kwa nini unakuwa kama mgeni katika nchi,

kama msafiri anayekaa kwa usiku mmoja tu?

14:9 Isa 50:2; Mwa 17:7; Yer 8:19; 15:16; Kut 29:45; Isa 63:19; Za 27:9Mbona unakuwa kama mtu aliyeshtukizwa,

kama shujaa asiye na uwezo wa kuokoa?

Wewe uko katikati yetu, Ee Bwana,

nasi tunaitwa kwa jina lako;

usituache!

14:10 Yer 2:25; Za 119:101; Yer 6:20; Hes 8:13; Ebr 8:12; Amo 5:22; Hos 7:2; 9:9; Yer 44:21Hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu hawa:

“Wanapenda sana kutangatanga,

hawaizuii miguu yao.

Hivyo Bwana hawakubali;

sasa ataukumbuka uovu wao

na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.”

14:11 Kut 32:10; 1Sam 2:25Kisha Bwana akaniambia, “Usiombe kwa ajili ya mafanikio ya watu hawa. 14:12 Kum 1:45; 1Sam 8:18; Yer 7:21; Law 1:1-17; Yer 11:11; Amo 5:22; Isa 51:19; Yer 9:16Ingawa wanafunga, sitasikiliza kilio chao; hata wakitoa dhabihu za kuteketezwa na dhabihu za nafaka, sitazikubali. Badala yake, nitawaangamiza kwa upanga, njaa na tauni.”

Lakini nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, manabii wanaendelea kuwaambia, ‘Hamtaona upanga wala kukabiliwa na njaa. Naam, nitawapa amani ya kudumu mahali hapa.’ ”

14:14 Yer 23:25; 2The 2:9-11; Eze 13:2-6; Yer 23:16; Mao 2:9; Eze 12:24; Yer 27:14Ndipo Bwana akaniambia, “Manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwatuma, wala sikuwaweka, wala sikusema nao. Wanawatabiria maono ya uongo, maaguzi, maono ya sanamu zisizofaa kitu, na madanganyo ya mawazo yao wenyewe. 14:15 Yer 20:6; Eze 14:9; Yer 16:4; Mao 1:19; Yer 23:15; 5:12-13Kwa hiyo, hili ndilo Bwana asemalo kuhusu manabii wanaotabiri kwa jina langu: Mimi sikuwatuma, lakini wanasema, ‘Hakuna upanga wala njaa itakayoigusa nchi hii.’ Manabii hao hao watakufa kwa upanga na njaa. 14:16 Yer 17:10; Mit 1:31; Yer 7:33; Za 79:3; Mt 15:14Nao watu hao wanaowatabiria watatupwa nje katika barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga. Hapatakuwepo yeyote wa kuwazika wao au wake zao, wana wao au binti zao. Nitawamwagia maafa wanayostahili.

14:17 Za 119:136; Yer 8:21; Mao 1:16; 2Fal 19:21; Yer 23:12“Nena nao neno hili:

“ ‘Macho yangu na yatiririkwe na machozi

usiku na mchana bila kukoma;

kwa kuwa binti yangu aliye bikira, yaani watu wangu,

amepata jeraha baya,

pigo la kuangamiza.

14:18 Eze 7:14-15; 2Nya 36:10; Yer 13:17Kama nikienda mashambani,

ninaona wale waliouawa kwa upanga;

kama nikienda mjini,

ninaona maangamizi ya njaa.

Nabii na kuhani kwa pamoja

wamekwenda katika nchi wasiyoijua.’ ”

14:19 Yer 7:29; 30:12-13; 8:15; Isa 1:6Je, umemkataa Yuda kabisa?

Umemchukia Sayuni kabisa?

Kwa nini umetuumiza

hata hatuwezi kuponyeka?

Tulitarajia amani,

lakini hakuna jema lililotujia;

tulitarajia wakati wa kupona

lakini kuna hofu kuu tu.

14:20 Amu 10:10; Dan 9:7-8; Yer 3:13; Law 26:40; 1Fal 8:47; Ezr 9:6Ee Bwana, tunatambua uovu wetu

na kosa la baba zetu;

kweli tumetenda dhambi dhidi yako.

14:21 Yer 17:12; Yos 7:9; Isa 62:7; Yer 3:17; Kut 2:24Kwa ajili ya jina lako usituchukie kabisa;

usikidharau kiti chako cha enzi kilichotukuka.

Kumbuka agano lako nasi

na usilivunje.

14:22 1Fal 8:36; Isa 30:23; Za 135:7; Isa 41:24; 44:10; Yer 10:15Je, kuna sanamu yoyote isiyofaa kitu ya mataifa

iwezayo kuleta mvua?

Je, anga peke yake zaweza kutoa mvua?

La hasha, ni wewe peke yako,

Ee Bwana, Mungu wetu.

Kwa hiyo tumaini letu liko kwako,

kwa kuwa wewe ndiwe ufanyaye haya yote.

Read More of Yeremia 14

Yeremia 15:1-21

Adhabu Isiyoepukika

15:1 Kut 32:11; Hes 14:13-20; 1Sam 7:9; Eze 14:14, 20; 2Fal 17:20; Yer 16:13; 7:16Kisha Bwana akaniambia: “Hata kama Mose na Samweli wangesimama mbele zangu, moyo wangu usingewaelekea watu hawa. Waondoe mbele za macho yangu! Waache waende! 15:2 Yer 42:22; 44:13; Zek 11:9; Mao 4:9; Eze 12:11; Ufu 13:10; Yer 14:12Nao kama wakikuuliza, ‘Twende wapi?’ Waambie, ‘Hili ndilo Bwana asemalo:

“ ‘Wale waliowekwa kwa ajili ya kufa, wakafe;

waliowekwa kwa ajili ya upanga, kwa upanga;

waliowekwa kwa ajili ya njaa, kwa njaa:

waliowekwa kwa ajili ya kutekwa, watekwe.’ ”

15:3 Law 26:16; Hes 33:4; Kum 28:26; Eze 33:27; 14:21; 2Fal 9:36; 1Fal 21:19Bwana asema, “Nitatuma aina nne za waharabu dhidi yao: nazo ni upanga ili kuua na mbwa ili wakokote mbali, ndege wa angani na wanyama wa nchi ili kula na kuangamiza. 15:4 Eze 23:46; Yer 29:18; 34:17; Ay 17:6; 2Fal 21:2, 11; 23:26-27; Yer 24:9Nitawafanya wawe machukizo kwa falme zote za dunia kwa sababu ya kile alichofanya Manase mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda huko Yerusalemu.

15:5 Isa 27:11; Nah 3:7; Isa 51:19; Yer 13:14; 16:13; 21:7“Ni nani atakayekuhurumia, ee Yerusalemu?

Ni nani atakayeomboleza kwa ajili yako?

Ni nani atakayesimama ili kuuliza

kuhusu hali yako?

15:6 Kum 32:15; Yer 6:19; Isa 31:3; Hos 13:14; Yer 7:20; Amo 7:8Umenikataa mimi,” asema Bwana.

“Unazidi kukengeuka.

Hivyo nitanyoosha mkono wangu juu yako na kukuangamiza,

siwezi kuendelea kukuonea huruma.

15:7 Isa 9:13; Yer 18:21; Isa 41:16; 3:26; 2Nya 28:22Nitawapepeta kwa uma wa kupepetea

kwenye malango ya miji katika nchi.

Nitaleta msiba na maangamizi juu ya watu wangu,

kwa maana hawajabadili njia zao.

15:8 Isa 47:9; Yer 6:4; Ay 18:11Nitawafanya wajane wao kuwa wengi

kuliko mchanga wa bahari.

Wakati wa adhuhuri nitamleta mharabu

dhidi ya mama wa vijana wao waume;

kwa ghafula nitaleta juu yao

maumivu makuu na hofu kuu.

15:9 1Sam 2:5; Yer 21:7; 25:31; 7:19; Amo 8:9; 2Fal 25:7; Yer 19:7Mama mwenye watoto saba atazimia

na kupumua pumzi yake ya mwisho.

Jua lake litatua kungali bado mchana,

atatahayarika na kufedheheka.

Wale wote waliobaki nitawaua kwa upanga

mbele ya adui zao,”

asema Bwana.

15:10 Ay 10:18-19; Law 25:36; Neh 5:1-12; Ay 3:1; Yer 6:10; 1:19Ole wangu, mama yangu, kwamba ulinizaa,

mtu ambaye ulimwengu wote

unashindana na kugombana naye!

Sikukopa wala sikukopesha,

lakini kila mmoja ananilaani.

15:11 Yer 40:4; 37:3; 42:1-3; 21:1-2Bwana akasema,

“Hakika nitakuokoa kwa kusudi jema,

hakika nitawafanya adui zako wakuombe msaada

nyakati za maafa na nyakati za dhiki.

15:12 Mao 1:14; Hos 10:11; Kum 28:48; Yer 28:14“Je, mtu aweza kuvunja chuma,

chuma kitokacho kaskazini, au shaba?

15:13 Yer 17:3; Za 44:12; Eze 38:12-13; 2Fal 24:13; 25:15Utajiri wako na hazina zako nitavitoa kuwa nyara,

bila gharama,

kwa sababu ya dhambi zako zote

katika nchi yako yote.

15:14 Kum 28:36; Yer 16:13; Kum 32:22; Za 21:9; Yer 5:19Nitakufanya uwe mtumwa wa adui zako

katika nchi usiyoijua,

kwa kuwa katika hasira yangu moto umewashwa

utakaowaka juu yako daima.”

15:15 Yn 21:15-17; Yer 12:3; Za 69:7-9; 119:84; 44:22; Kut 34:6Wewe unafahamu, Ee Bwana,

unikumbuke na unitunze mimi.

Lipiza kisasi juu ya watesi wangu.

Kwa uvumilivu wako usiniondolee mbali;

kumbuka jinsi ninavyoshutumiwa.

15:16 Ay 23:12; 15:11; Eze 2:8; Ufu 10:10; Za 119:72, 103; Yer 14:9; Isa 43:7Maneno yako yalipokuja, niliyala;

yakawa shangwe yangu

na furaha ya moyo wangu,

kwa kuwa nimeitwa kwa jina lako,

Ee Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote.

15:17 Rut 3:3; Za 26:4-5; Yer 16:8; 2Fal 3:15Kamwe sikuketi katika kundi la wafanyao sherehe,

wala kamwe sikujifurahisha pamoja nao;

niliketi peke yangu kwa sababu mkono wako ulikuwa juu yangu,

na wewe ulikuwa umenijaza hasira.

15:18 Mik 1:9; Ay 6:4; Za 9:10Kwa nini maumivu yangu hayakomi,

na jeraha langu ni la kuhuzunisha,

wala haliponyeki?

Je, utakuwa kwangu kama kijito cha udanganyifu,

kama chemchemi iliyokauka?

15:19 Zek 3:7; Eze 22:26; Kut 4:16Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama ukitubu, nitakurejeza

ili uweze kunitumikia;

kama ukinena maneno yenye maana,

wala si ya upuzi,

utakuwa mnenaji wangu.

Watu hawa ndio watakaokugeukia,

wala si wewe utakayewageukia wao.

15:20 Yer 42:11; Eze 3:8; Isa 50:7; Za 129:2; Yer 20:11Nitakufanya wewe uwe ukuta kwa watu hawa,

ngome ya ukuta wa shaba;

watapigana nawe

lakini hawatakushinda,

kwa maana mimi niko pamoja nawe

kukuponya na kukuokoa,”

asema Bwana.

15:21 Yer 50:34; Mwa 48:16; Isa 49:25; Yer 1:8; Za 97:10“Nitakuokoa kutoka mikono ya waovu,

na kukukomboa kutoka makucha ya watu wakatili.”

Read More of Yeremia 15