Isaya 63:1-19, Isaya 64:1-12, Isaya 65:1-16 NEN

Isaya 63:1-19

Siku Ya Mungu Ya Kisasi Na Ukombozi

63:1 Mwa 36:33; Amo 1:12; Yer 42:11; Sef 3:17; 2Nya 28:17; Isa 11:14; Ufu 19:13; Ay 9:4Ni nani huyu anayekuja kutoka Edomu,

kutoka Bosra, mwenye mavazi yaliyotiwa madoa mekundu?

Ni nani huyu, aliyevikwa joho la kifahari,

anayetembea kwa ukuu wa nguvu zake?

“Mimi ndimi, nisemaye katika haki,

mwenye nguvu wa kuokoa.”

63:2 Ufu 19:13; Mwa 49:11Kwa nini mavazi yako ni mekundu,

kama ya yule akanyagaye shinikizo la zabibu?

63:3 Amu 6:11; Ufu 19:15; Mao 1:15; Ufu 19:13; 14:19-20; Za 108:13“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu;

kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami.

Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu

na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu;

damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu,

na kutia madoa nguo zangu zote.

63:4 Isa 1:24; Yer 50:15Kwa kuwa siku ya kisasi ilikuwa moyoni mwangu,

mwaka wa ukombozi wangu umefika.

63:5 2Fal 14:26; Isa 41:28; 59:16; Za 44:3; Yn 16:32; Isa 33:2Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia,

nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada;

hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu,

na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.

63:6 Isa 29:9; Mao 4:21; Isa 34:3; Ay 40:12Nilikanyaga mataifa kwa miguu katika hasira yangu,

katika ghadhabu yangu niliwalewesha,

na kumwaga damu yao juu ya ardhi.”

Kusifu Na Kuomba

63:7 Isa 54:8; Efe 2:4; Kut 18:9Nitasimulia juu ya wema wa Bwana,

kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa,

sawasawa na yote ambayo Bwana

ametenda kwa ajili yetu:

naam, mambo mengi mema aliyoyatenda

kwa ajili ya nyumba ya Israeli,

sawasawa na huruma zake

na wema wake mwingi.

63:8 Mdo 9:4; Kut 14:19; 33:14; Kum 7:7-8; Ezr 9:9; Za 28:9; Ay 37:23Alisema, “Hakika wao ni watu wangu,

wana ambao hawatanidanganya”;

hivyo akawa Mwokozi wao.

63:9 Kut 14:19; 33:14; Kum 7:7-8; Ezr 9:9; Isa 48:20; Kum 1:31; 32:7; Za 28:9; Ay 37:23Katika taabu zao zote naye alitaabika,

na malaika wa uso wake akawaokoa.

Katika upendo wake na rehema zake aliwakomboa,

akawainua na kuwachukua siku zote zilizopita.

63:10 Eze 20:8; Mdo 7:39-42; Efe 4:30; Za 106:40; 78:17; Isa 10:4; Yos 10:14Lakini waliasi,

na kumhuzunisha Roho Mtakatifu wake.

Hivyo aligeuka na kuwa adui yao,

na yeye mwenyewe akapigana dhidi yao.

63:11 Kut 14:22, 30; Hes 11:17; Za 77:20Ndipo watu wake wakazikumbuka siku zilizopita,

siku za Mose na watu wake:

yuko wapi yeye aliyewaleta kupitia katikati ya bahari,

pamoja na wachungaji wa kundi lake?

Yuko wapi yule aliyeweka

Roho wake Mtakatifu katikati yao,

63:12 Kut 14:21-22; Isa 11:15; Mwa 49:24aliyetuma mkono wake uliotukuka wenye nguvu

kuwa katika mkono wa kuume wa Mose,

aliyegawa maji ya bahari mbele yao,

ili kujipatia jina milele,

63:13 Kum 32:12; Yer 31:9; Kut 14:24; Za 119:11aliyewaongoza kupitia kwenye vilindi?

Kama farasi katika nchi iliyo wazi,

wao hawakujikwaa,

63:14 Kut 33:14; Kum 12:9kama ngʼombe washukao bondeni kwenye malisho,

walipewa pumziko na Roho wa Bwana.

Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako

ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.

63:15 Za 80:14; Mao 3:50; 1Fal 22:19; 2:26; Hos 11:8; Kum 26:15; Isa 64:12Tazama chini kutoka mbinguni ukaone

kutoka kiti chako cha enzi

kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu.

Uko wapi wivu wako na uweza wako?

Umetuzuilia wema wako na huruma zako.

63:16 Ay 14:21; Gal 3:28; Isa 44:6; Kut 4:22; Yer 3:4; Yn 8:41; Isa 59:20Lakini wewe ni Baba yetu,

ingawa Abrahamu hatufahamu sisi

wala Israeli hatutambui;

wewe, Ee Bwana, ndiwe Baba yetu,

Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.

63:17 Isa 6:10; 29:13; Hes 10:36; Mt 13:15; Mwa 20:13; Mao 3:9; Kut 4:21; 34:9Ee Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako,

na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu?

Rudi kwa ajili ya watumishi wako,

yale makabila ambayo ni urithi wako.

63:18 Law 26:31; Dan 8:24; Za 74:3-8; Kum 4:26; Isa 28:18; Lk 21:24; Dan 8:13Kwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu,

lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.

63:19 Isa 43:7; Yer 14:9Sisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe,

kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.

Read More of Isaya 63

Isaya 64:1-12

64:1 Kut 19:18; Mik 1:3; Za 18:9Laiti ungelipasua mbingu na kushuka chini,

ili milima ingelitetemeka mbele zako!

64:2 Za 119:120; Yer 5:22; Isa 30:27; Yer 33:9Kama vile moto uteketezavyo vijiti

na kusababisha maji kuchemka,

shuka ukafanye jina lako lijulikane kwa adui zako,

na kusababisha mataifa yatetemeke mbele zako!

64:3 Za 65:5; 18:7Kwa maana ulipofanya mambo ya kutisha ambayo hatukuyatazamia,

ulishuka, nayo milima ikatetemeka mbele zako.

64:4 Za 31:19; Isa 30:18; 1Kor 2:9-10; Kol 1:26-27; Isa 43:10-11; 30:18Tangu nyakati za zamani hakuna yeyote aliyesikia,

hakuna sikio lililotambua,

hakuna jicho lililomwona Mungu mwingine ila wewe,

anayetenda mambo kwa ajili ya wale wamngojeao.

64:5 Isa 26:8; Mdo 10:35; Isa 10:4Uliwasaidia watu wale watendao yaliyo haki kwa furaha,

wale wazikumbukao njia zako.

Lakini wakati tulipoendelea kutenda dhambi kinyume na njia zako,

ulikasirika.

Tutawezaje basi kuokolewa?

64:6 Isa 46:12; Za 90:5-6; Yer 4:12; Law 12:2Sisi sote tumekuwa kama mtu aliye najisi,

nayo matendo yetu yote ya uadilifu ni kama matambaa machafu;

sisi sote tunasinyaa kama jani,

na kama upepo maovu yetu hutupeperusha.

64:7 Eze 22:30; Yer 8:6; Isa 9:18; Eze 22:18-22; Isa 41:28; Kum 31:18; Za 14:4Hakuna yeyote anayeliitia jina lako

wala anayejitahidi kukushika,

kwa kuwa umetuficha uso wako

na kutuacha tudhoofike kwa sababu ya dhambi zetu.

64:8 Yer 18:6; Kut 4:22; Isa 63:16; 29:16; Yer 3:4; Rum 9:20-21; Ay 10:3Lakini, Ee Bwana, wewe ndiwe Baba yetu.

Sisi ni udongo, wewe ndiye mfinyanzi;

sisi sote tu kazi ya mkono wako.

64:9 Isa 54:8; Mao 5:22; Isa 43:25; Za 100:3; Isa 51:4; 57:17Ee Bwana, usikasirike kupita kiasi,

usizikumbuke dhambi zetu milele.

Ee Bwana, utuangalie, twakuomba,

kwa kuwa sisi sote tu watu wako.

64:10 Za 78:54; Isa 1:26; Kum 29:23Miji yako mitakatifu imekuwa jangwa;

hata Sayuni ni jangwa, Yerusalemu ni ukiwa.

64:11 2Fal 25:9; Eze 24:21; Mao 1:7-10Hekalu letu takatifu na tukufu, mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe,

limechomwa kwa moto,

navyo vitu vyote tulivyovithamini vimeharibika.

64:12 Mwa 43:31; Za 74:10-11; Es 4:14; Za 50:21Ee Bwana, baada ya haya yote, utajizuia?

Je, utanyamaza kimya na kutuadhibu kupita kiasi?

Read More of Isaya 64

Isaya 65:1-16

Hukumu Na Wokovu

65:1 Rum 10:20; Efe 2:12-13; Rum 9:30; Za 22:27; Hos 1:10; Rum 9:24-26; Isa 43:7“Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’

65:2 Za 78:8; Rum 10:21; Za 81:11-12; Mit 24:2; Isa 66:18Mchana kutwa nimeinyoosha mikono yangu

kwa watu wakaidi,

wanaokwenda katika njia ambazo si nzuri,

wafuatao mawazo yao wenyewe:

65:3 Isa 1:29; Law 17:5; Ay 1:11; Yer 41:5; Eze 23:41; Yer 44:17taifa ambalo daima hunikasirisha

machoni pangu,

wakitoa dhabihu katika bustani

na kufukiza uvumba juu ya madhabahu za matofali;

65:4 Law 11:7; Isa 8:19; Law 19:31; Kum 18:11watu waketio katikati ya makaburi

na kukesha mahali pa siri,

walao nyama za nguruwe,

nazo sufuria zao zina mchuzi wa nyama zilizo najisi,

65:5 Za 40:4; Lk 7:39; Yud 19; Mt 9:11; Lk 18:9-12; Mit 10:26wasemao, ‘Kaa mbali; usinikaribie,

kwa maana mimi ni mtakatifu mno kwako!’

Watu wa aina hiyo ni moshi katika pua zangu,

ni moto uwakao mchana kutwa.

65:6 2Nya 6:23; Kum 32:34; Za 50:3; Yer 16:18; Lk 6:38; Isa 59:18; Za 79:12; Eze 9:10“Tazama, jambo hili hubakia limeandikwa mbele zangu:

sitanyamaza, bali nitalipiza kwa ukamilifu;

nitalipiza mapajani mwao:

65:7 Kut 20:5; Yer 32:18; Law 26:39; Isa 22:14; Mit 10:24; Isa 10:12; 57:7dhambi zenu na dhambi za baba zenu,”

asema Bwana.

“Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima

na kunichokoza mimi juu ya vilima,

nitawapimia mapajani mwao

malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”

65:8 Isa 5:2; 54:17; Kut 4:22; Yer 3:4; Isa 29:16; Rum 9:20-21; Ay 10:3Hili ndilo asemalo Bwana:

“Kama vile divai mpya ingali bado inapatikana

katika kishada cha zabibu,

nao watu husema, ‘Usikiharibu,

kwa kuwa bado kuna kitu kizuri ndani yake,’

hivyo ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu;

sitawaangamiza wote.

65:9 Isa 45:19; Hes 34:13; Amo 9:11-15; Isa 32:18; Yer 50:19Nitawaleta wazao kutoka kwa Yakobo,

na kutoka kwa Yuda wale watakaomiliki milima yangu,

nao watu wangu wateule watairithi,

nako huko wataishi watumishi wangu.

65:10 1Nya 27:29; Hos 2:15; Mdo 9:35; Yos 7:26; Isa 35:2; Yer 31:12; Eze 34:13-14Sharoni itakuwa malisho

kwa ajili ya makundi ya kondoo,

na Bonde la Akori mahali pa kupumzikia

kwa makundi ya ngʼombe,

kwa ajili ya watu wangu wanaonitafuta.

65:11 Eze 23:41; Yer 19:4; 1Kor 10:21; Kum 29:24-25; 32:15; Yer 2:13; 19:4“Bali kwenu ninyi mnaomwacha Bwana

na kuusahau mlima wangu mtakatifu,

ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati,65:11 Bahati alikuwa mungu wa Wakaldayo ambaye pia alijulikana kama Gadi.

na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa

kwa ajili ya Ajali,65:11 Ajali au Meni alikuwa mungu wa majaliwa.

65:12 Mit 1:24-25; Yer 7:27; 2Nya 36:15-16; Yer 13:11; Isa 1:20; 30:25; Mik 5:15nitawaagiza mfe kwa upanga,

nanyi nyote mtainama chini ili kuchinjwa;

kwa kuwa niliwaita lakini hamkuitika,

nilisema lakini hamkusikiliza.

Mlitenda maovu machoni pangu,

nanyi mkachagua mambo yale yanayonichukiza.”

65:13 Isa 1:19; Ay 18:12; Lk 6:25; Isa 33:16; 60:5; 44:9Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Watumishi wangu watakula,

lakini ninyi mtaona njaa;

watumishi wangu watakunywa

lakini ninyi mtaona kiu;

watumishi wangu watafurahi,

lakini ninyi mtaona haya.

65:14 Isa 15:2; Lk 13:28; Za 109:28; Sef 3:14-20; Yak 5:13; Mt 8:12Watumishi wangu wataimba

kwa furaha ya mioyo yao,

lakini ninyi mtalia

kutokana na uchungu wa moyoni,

na kupiga yowe kwa sababu

ya uchungu wa roho zenu.

65:15 Hes 5:27; Mdo 11:26; Zek 8:13; Za 102:8; Mwa 32:28; Ufu 2:17Mtaliacha jina lenu

kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa;

Bwana Mwenyezi atawaua ninyi,

lakini watumishi wake atawapa jina jingine.

65:16 Za 31:5; Ufu 3:14; Isa 19:18; Kum 29:19; Ay 11:16; Za 63:11Yeye aombaye baraka katika nchi

atafanya hivyo kwa Mungu wa kweli;

yeye aapaye katika nchi

ataapa kwa Mungu wa kweli.

Kwa kuwa taabu za zamani zitasahaulika

na kufichwa kutoka machoni pangu.

Read More of Isaya 65