Isaya 29:1-24, Isaya 30:1-18 NEN

Isaya 29:1-24

Ole Wa Mji Wa Daudi

29:1 Isa 22:12-13; 1:14; 2Sam 5:7; Isa 28:1Ole wako, wewe Arieli, Arieli,

mji alimokaa Daudi!

Ongezeni mwaka kwa mwaka,

na mzunguko wa sikukuu zenu uendelee.

29:2 Mao 2:5; Isa 3:26; Eze 43:15Hata hivyo nitauzunguka Arieli kwa jeshi,

utalia na kuomboleza,

utakuwa kwangu kama mahali

pa kuwashia moto madhabahuni.

29:3 Lk 19:43-44; 2Fal 25:1Nitapiga kambi pande zote dhidi yako,

nitakuzunguka kwa minara

na kupanga mazingirwa yangu dhidi yako.

29:4 Isa 8:19; 47:1; 52:2; 26:16; Law 19:31Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini,

utamumunya maneno yako kutoka mavumbini.

Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu,

utanongʼona maneno yako toka mavumbini.

29:5 Isa 17:13; 1The 5:3; Za 55:15; Kum 9:21; Za 78:39; Isa 51:12; Za 103:15Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini,

kundi la wakatili watakuwa

kama makapi yapeperushwayo.

Naam, ghafula, mara moja,

29:6 Mk 13:8; Ufu 6:12; Isa 26:21; Zek 14:1-5; Kut 19:16; Mt 24:7; Za 83:13-15Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuja

na ngurumo, tetemeko la ardhi, na kwa sauti kuu,

atakuja na dhoruba, tufani na miali ya moto iteketezayo.

29:7 Mik 4:11-12; Zek 12:9; Ay 20:8Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli,

yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi,

watakuwa kama ilivyo ndoto,

kama maono wakati wa usiku:

29:8 Za 73:20; Yer 30:16; Isa 17:12-14; Zek 12:3; Isa 54:17kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,

lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,

kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,

lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.

Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa

yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni.

29:9 Yer 13:13; Isa 63:9; Law 10:9; Yer 4:9; Isa 6:10; 63:6; Za 60:3; Yer 13:13; Isa 51:22Duwaeni na kushangaa,

jifanyeni vipofu wenyewe na msione,

leweni, lakini si kwa mvinyo,

pepesukeni lakini si kwa kileo.

29:10 2The 2:9-11; Za 69:23; Mik 3:6; Amu 4:21; Isa 44:18; 6:9-10; Rum 11:8Bwana amewaleteeni usingizi mzito:

Ameziba macho yenu (ninyi manabii);

amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).

29:11 Dan 8:26; Mt 13:11; Isa 28:7; Ufu 5:1-2; Isa 8:16; Dan 12:9Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.” Au kama mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”

29:13 Yer 12:2; Kol 2:22; Eze 33:31; Mt 15:8-9; Mk 7:6-7; Isa 58:2; Za 119:70; Yer 14:11Bwana anasema:

“Watu hawa hunikaribia kwa vinywa vyao

na kuniheshimu kwa midomo yao,

lakini mioyo yao iko mbali nami.

Ibada yao kwangu inatokana na maagizo

waliyofundishwa na wanadamu.

29:14 Yer 49:7; Ay 10:16; 5:13; Isa 6:9-10; 1Kor 1:19; Yer 8:9; Isa 6:9-10Kwa hiyo mara nyingine tena nitawashangaza watu hawa,

kwa ajabu juu ya ajabu.

Hekima ya wenye hekima itapotea,

nayo akili ya wenye akili itatoweka.”

29:15 Ay 22:13-14; Eze 8:12; 2Fal 21:16; Ay 22:13; Isa 28:15; Ay 8:3; Za 10:11-13Ole kwa wale wanaokwenda kwenye vilindi virefu

kumficha Bwana mipango yao,

wafanyao kazi zao gizani na kufikiri,

“Ni nani anayetuona? Ni nani atakayejua?”

29:16 Yer 18:6; Rum 9:20-21; Za 94:9; Ay 10:9; Isa 10:15; 45:9; Ay 9:12; Yer 18:6; Mwa 2:7Mnapindua mambo juu chini,

kana kwamba mfinyanzi aweza kufikiriwa kuwa kama udongo wa mfinyanzi!

Je, kile kilichofinyangwa chaweza kumwambia yule aliyekifinyanga,

“Wewe hukunifinyanga mimi?”

Je, chungu kinaweza kumwambia mfinyanzi,

“Wewe hujui chochote?”

29:17 Za 84:6; Isa 32:15; 10:25; 2:13; Za 107:33Kwa muda mfupi sana, je, Lebanoni haitageuzwa kuwa shamba lenye rutuba,

na shamba lenye rutuba liwe kama msitu?

29:18 Mk 7:37; Za 146:8; Mt 11:5; Lk 7:22; Isa 32:3; Za 107:14Katika siku ile viziwi watasikia maneno ya kitabu,

na katika utusitusi na giza

macho ya kipofu yataona.

29:19 Za 72:4; 25:9; Isa 5:19; 12:6; 3:15; Yak 2:5; Mt 5:5; 11:29; Mwa 42:26Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana,

wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.

29:20 2Nya 36:16; Isa 28:22; Eze 11:2; Isa 13:11; 59:4; Ay 15:35; Za 7:14Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea,

nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali,

29:21 Amo 5:10-15; Isa 5:23; Hab 1:4; Mit 21:28wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia,

wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama,

na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki

yeye asiye na hatia.

29:22 Mwa 11:16; Yoe 2:26; Yos 24:3; Sef 3:11; Kut 6:6; Mwa 17:16; Isa 41:8; 51:2Kwa hiyo hili ndilo Bwana, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo:

“Yakobo hataaibishwa tena,

wala nyuso zao hazitabadilika sura tena.

29:23 Isa 53:10; 54:1-4; 19:25; 49:20-26; 5:19; Mt 6:9Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao,

kazi ya mikono yangu,

watalitakasa Jina langu takatifu;

wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo,

nao watamcha Mungu wa Israeli.

29:24 Mit 12:8; Ebr 5:2; Isa 60:16; 42:16; Za 95:10; Isa 28:7; 32:4Wale wanaopotoka rohoni watapata ufahamu,

nao wale wanaolalamika watayakubali mafundisho.”

Read More of Isaya 29

Isaya 30:1-18

Ole Wa Taifa Kaidi

30:1 Isa 29:15; 8:12; Kum 29:19; 21:18; 2Fal 17:4Bwana asema,

“Ole kwa watoto wakaidi,

kwa wale wanaotimiza mipango ambayo si yangu,

wakifanya makubaliano, lakini si kwa Roho wangu,

wakilundika dhambi juu ya dhambi,

30:2 Mwa 25:22; Hes 27:21; 2Fal 25:26; Isa 36:6; Yer 2:18, 36; 42:14; Eze 17:15; 29:16wale washukao kwenda Misri

bila kutaka shauri langu,

wanaotafuta msaada wa ulinzi wa Farao,

watafutao kivuli cha Misri kwa ajili ya kimbilio.

30:3 Yer 37:5-7; Isa 20:4-5; Amu 9:8-15; Za 44:13Lakini ulinzi wa Farao utakuwa kwa aibu yenu,

kivuli cha Misri kitawaletea fedheha.

30:4 Hes 13:22; Isa 19:11Ingawa wana maafisa katika Soani

na wajumbe wamewasili katika Hanesi,

30:5 Isa 20:5; 36:6; 2Fal 18:21; Za 108:12; Yer 37:3-5; Eze 17:15kila mmoja ataaibishwa

kwa sababu ya taifa lisilowafaa kitu,

ambalo haliwaletei msaada wala faida,

bali aibu tu na fedheha.”

30:6 Kut 1:3; Yer 11:4; Kum 8:15; Hos 8:9; Kut 5:10; Isa 13:1; 5:30; 5:29; Mwa 42:26Neno kuhusu wanyama wa Negebu:

Katika nchi ya taabu na shida,

ya simba za dume na jike,

ya nyoka mwenye sumu kali na nyoka warukao,

wajumbe huchukua utajiri wao juu ya migongo ya punda,

hazina zao juu ya nundu za ngamia,

kwa lile taifa lisilokuwa na faida,

30:7 Yer 2:36; Ay 9:13; 2Fal 18:2kuvipeleka Misri,

ambaye msaada wake haufai kabisa.

Kwa hiyo nimemwita “Rahabu Asiyefanya Chochote.”

30:8 Kut 17:14; Hab 2:2; Kum 27:8; Yer 25:13; Yos 24:26-27; Isa 8:1; Yer 30:2Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,

liandike kwenye kitabu,

ili liweze kuwa shahidi milele

kwa ajili ya siku zijazo.

30:9 Isa 28:15; Kum 32:20; Isa 59:3-4; Za 78:8; Eze 2:6Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,

watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana.

30:10 Amo 7:13; Yer 11:21; 32:3; 1Sam 9:9; 1Fal 22:8; Yer 4:10; Eze 13:7; Rum 16:18; 2Tim 4:4Wanawaambia waonaji,

“Msione maono tena!”

Nako kwa manabii wanasema,

“Msiendelee kutupatia maono

ambayo ni ya kweli!

Tuambieni mambo ya kupendeza,

tabirini mambo ya uongo.

30:11 Mdo 13:8; Ay 21:14; Isa 35:8-9; Mit 3:6; Isa 29:19; 48:17Acheni njia hii,

ondokeni katika mapito haya,

nanyi acheni kutukabili pamoja

na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”

30:12 Isa 5:19; 5:24; Za 10:7; 12:5; Isa 5:7, 24Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:

“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,

mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu,

30:13 Neh 2:17; Za 80:12; 1Fal 20:30; Isa 17:14; Za 62:3dhambi hii itakuwa kwenu

kama ukuta mrefu,

wenye ufa na wenye kubetuka,

ambao unaanguka ghafula,

mara moja.

30:14 Za 2:9; 2Pet 2:4-5Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo

ukipasuka pasipo huruma

ambapo katika vipande vyake

hakuna kipande kitakachopatikana

kwa kuukulia makaa kutoka jikoni

au kuchotea maji kisimani.”

30:15 Isa 32:17; 2Nya 20:12; Mt 23:37Hili ndilo Bwana Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:

“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,

katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,

lakini hamkutaka.

30:16 Yer 46:6; Kum 17:16; 1Fal 10:28-29Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’

Kwa hiyo mtakimbia!

Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’

Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!

30:17 Kum 28:25; 2Fal 7:7; Law 26:8; Yos 23:10Watu 1,000 watakimbia

kwa ajili ya kitisho cha mtu mmoja,

kwa vitishio vya watu watano

wote mtakimbia,

hadi mtakapoachwa kama mlingoti wa bendera

juu ya kilele cha mlima,

kama bendera juu ya kilima.”

30:18 Mwa 43:31; 2Pet 3:9, 15; Za 27:14; Mao 3:25; Isa 5:16; 42:14; 48:9; Yon 3:10Hata hivyo Bwana anatamani kutupatia neema,

anainuka ili kuwaonyesha huruma.

Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki.

Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!

Read More of Isaya 30