Isaya 27:1-13, Isaya 28:1-29 NEN

Isaya 27:1-13

Wokovu Kwa Ajili Ya Israeli

27:1 Eze 29:3; Mwa 3:24; Hes 3:15; Ufu 12:9; Isa 2:11; Kum 32:41; Ay 26:13; Za 68:30; Isa 28:5; 31:8; 34:6; 66:16; Eze 21:3; Ay 3:8Katika siku ile,

Bwana ataadhibu kwa upanga wake,

upanga wake mkali, mkubwa na wenye nguvu,

ataadhibu Lewiathani27:1 Lewiathani ni mnyama mkubwa wa baharini mwenye magamba anayefanana na joka kubwa, mwenye umbo la kutisha, asiyeweza kuvuliwa. yule nyoka apitaye kwa mwendo laini,

Lewiathani yule nyoka mwenye kujipinda;

atamuua joka huyo mkubwa sana wa baharini.

27:2 Yer 2:21; Isa 24:21; 5:1Katika siku ile:

“Imbeni kuhusu shamba la mizabibu lililozaa:

27:3 Isa 58:11; Za 91:4; Yn 6:39; Isa 5:2Mimi, Bwana, ninalitunza,

nalinyweshea maji mfululizo.

Ninalichunga usiku na mchana

ili mtu yeyote asije akalidhuru.

27:4 Isa 10:17; Mt 3:12; 2Sam 23:6; Ebr 6:8Mimi sijakasirika.

Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!

Ningepambana dhidi yake katika vita,

ningeliichoma moto yote.

27:5 Isa 25:4; Efe 2:12-14; Ay 22:21; Za 119:165; Rum 5:1; 2Kor 5:20Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,

wao na wafanye amani nami,

naam, wafanye amani nami.”

27:6 Mwa 40:10; Hos 14:5-8; Za 72:16; 2Fal 19:30; Eze 17:23; 36:8; Isa 11:1Katika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,

Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,

naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.

27:7 Isa 10:26; 37:36-38Je, Bwana amempiga

vile alivyowapiga wale waliompiga?

Je, yeye ameuawa

vile walivyouawa wale waliomuua yeye?

27:8 Isa 49:14; Yer 10:24; Ay 23:6; Isa 54:7; Mwa 41:6; Isa 50:1Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye:

kwa mshindo wake mkali anamfukuza,

kama siku ile uvumapo upepo wa mashariki.

27:9 Kut 34:13; Rum 11:27; Za 78:38; Kut 23:24; 2Nya 14:5; Law 26:30Kwa hili, basi, hatia ya Yakobo itafanyiwa upatanisho,

nalo hili litakuwa matunda ya utimilizo wa kuondolewa kwa dhambi yake:

Wakati atakapoyafanya mawe yote ya madhabahu

kuwa kama mawe ya chokaa yaliyopondwa vipande vipande,

hakuna nguzo za Ashera au madhabahu za kufukizia uvumba

zitakazobaki zimesimama.

27:10 Kum 13:16; Isa 17:2; 5:5, 17; Mao 5:18; Yer 26:6; 10:22; Isa 32:14; Mwa 1:2; Kum 13:16; Isa 5:6; 32:14; Yer 10:22; Law 1:4; 5:18; Isa 5:5; 5:17; 17:2Mji ulio na boma umebaki ukiwa,

makao yaliyotelekezwa, yaliyoachwa kama jangwa.

Huko ndama hulisha,

huko hujilaza,

wanakwanyua matawi yake.

27:11 Kum 32:18, 38; Yer 8:7; 4:22; Isa 9:17; 10:33; Yer 11:16; Isa 33:12; 41:8; 44:21-24Wakati vijiti vyake vimekauka, huvunjwa

nao wanawake huja na kuwasha navyo moto.

Kwa kuwa hili ni taifa lisilo na ufahamu,

kwa hiyo yeye aliyewafanya hana huruma juu yao,

Muumba wao hawaonyeshi fadhili.

27:12 Mwa 15:18; Kum 30:4; Isa 1:9; Mt 3:12; Isa 21:10; 17:6Katika siku ile Bwana atapura kutoka matiririko ya Mto Frati hadi Kijito cha Misri, nanyi ee Waisraeli, mtakusanywa mmoja mmoja. 27:13 Hes 10:2; Amu 3:27; Mt 24:31; Isa 10:19; Hos 8:1; Law 25:9; Za 106:47Katika siku ile tarumbeta kubwa italia. Wale waliokuwa wakiangamia katika nchi ya Ashuru, nao wale waliokuwa uhamishoni katika nchi ya Misri watakuja na kumwabudu Bwana katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

Read More of Isaya 27

Isaya 28:1-29

Ole Wa Efraimu

28:1 Isa 7:2; Law 10:9; Amo 6:6; Isa 10:5; 9:9; Hos 7:5; Isa 5:11; 8:7Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,

kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:

kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!

28:2 Isa 30:30; 40:10; Yos 10:11; Eze 13:11; Isa 29:6; 8:7; Dan 9:26Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.

Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,

kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,

atakiangusha chini kwa nguvu.

28:3 Ay 40:12; Isa 5:5Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,

kitakanyagwa chini ya nyayo.

28:4 Wim 2:13; Nah 3:12; Hos 9:10Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,

uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,

litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:

mara mtu aionapo, huichuma na kuila.

28:5 Zek 9:16; Eze 21:26; Isa 10:20; 1:9; 29:18; Yer 13:18; Eze 16:12; Isa 62:3Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote

atakuwa taji la utukufu,

taji zuri la maua

kwa mabaki ya watu wake.

28:6 Amu 9:44-45; 2Sam 14:20; 2Nya 32:8; Yn 5:30; Isa 11:2-4Atakuwa roho ya haki

kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,

chanzo cha nguvu

kwa wale wazuiao vita langoni.

28:7 Law 10:9; Isa 56:10-12; Efe 5:18; Za 107:27; Isa 24:2; 3:12; 22:13; 9:15Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,

wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:

Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,

wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;

wanapepesuka wanapoona maono,

wanajikwaa wanapotoa maamuzi.

28:8 Yer 48:26Meza zote zimejawa na matapishi

wala hakuna sehemu hata ndogo

isiyokuwa na uchafu.

28:9 Yer 6:10; 1Pet 2:2; Za 32:8; Ebr 5:12-13; Yer 31:34; Isa 30:20; 48:17; 54:13“Yeye anajaribu kumfundisha nani?

Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?

Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?

Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini?

28:10 Isa 29:13Kwa maana ni:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;

hapa kidogo, kule kidogo.”

28:11 Yer 5:15; 1Kor 14:21; Mwa 11:7; Eze 3:5; Isa 33:19Sawa kabisa, kwa midomo migeni

na kwa lugha ngeni,

Mungu atasema na watu hawa,

28:12 Yos 1:13; Mt 11:28-29; 2Nya 14:7; Kut 14:14; Ay 11:18; Isa 11:10wale ambao aliwaambia,

“Hapa ni mahali pa kupumzika,

waliochoka na wapumzike,”

na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”

lakini hawakutaka kusikiliza.

28:13 Mt 21:44; Isa 8:14-15Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa:

Amri juu ya amri, amri juu ya amri,

kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,

hapa kidogo, kule kidogo:

ili waende na kuanguka chali,

wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.

28:14 Isa 1:10; 2Nya 36:16Kwa hiyo sikieni neno la Bwana, enyi watu wenye dharau

mnaotawala watu hawa wa Yerusalemu.

28:15 Dan 11:22; Isa 9:15; 10:26; Ay 5:23; Isa 8:19; Amu 9:35; Isa 29:15; Yer 23:24Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti,

tumefanya mapatano na kuzimu.

Wakati pigo lifurikalo litakapopita,

haliwezi kutugusa sisi,

kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu

na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.”

28:16 Zek 12:3; Efe 2:20; Rum 9:33; 1Pet 2:6; Isa 54:4; 14:32; Za 118:22; Isa 8:14-15; Dan 2:34-45; Mdo 4:11; Yer 51:26; 1Kor 3:11Kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Mwenyezi asemavyo:

“Tazama, ninaweka jiwe katika Sayuni,

jiwe lililojaribiwa,

jiwe la pembeni la thamani kwa ajili ya msingi thabiti.

Yeye atumainiye kamwe hatatiwa hofu.

28:17 Isa 5:16; Za 11:7; 2Fal 21:13; Yos 10:11Nitaifanya haki kuwa kamba ya kupimia

na uadilifu kuwa timazi;

mvua ya mawe itafagia kimbilio lenu, huo uongo,

nayo maji yatafurikia mahali penu pa kujificha.

28:18 Isa 63:18; Dan 8:13; Isa 7:7Agano lenu na kifo litabatilishwa,

patano lenu na kuzimu halitasimama.

Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba,

litawaangusha chini.

28:19 2Fal 24:2; Ay 18:11; Za 5:3Kila mara lijapo litawachukua,

asubuhi baada ya asubuhi,

wakati wa mchana na wakati wa usiku,

litawakumba tangu mwanzo hadi mwisho.”

Kuuelewa ujumbe huu

utaleta hofu tupu.

28:20 Isa 59:6Kitanda ni kifupi mno kujinyoosha juu yake,

nguo ya kujifunikia ni nyembamba mno

mtu hawezi kujifunikia.

28:21 2Sam 5:20; Mwa 38:29; 1Nya 14:11-16; Lk 19:41-44; Yos 9:3; Isa 65:7Bwana atainuka kama alivyofanya kwenye Mlima Perasimu,

ataghadhibika kama alivyofanya katika Bonde la Gibeoni:

ili kufanya kazi yake, kazi yake ya ajabu,

ili kutimiza kazi yake, kazi yake ngeni.

28:22 Isa 10:22; Yer 29:18; 2Nya 36:16; Mao 2:15; Sef 2:15Sasa acheni dharau zenu,

la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.

Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia

habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote.

28:23 Isa 32:9Sikilizeni msikie sauti yangu,

tegeni masikio na msikie niyasemayo.

28:24 Mhu 3:2Wakati mkulima alimapo ili apande,

je, hulima siku zote?

Je, huendelea kubomoa ardhi

na kusawazisha udongo?

28:25 Kut 9:32; Mt 23:23; Eze 4:9Akiisha kusawazisha shamba,

je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?

Je, hapandi ngano katika sehemu yake,

shayiri katika eneo lake,

na nafaka nyingine katika shamba lake?

28:26 Za 94:10Mungu wake humwelekeza

na kumfundisha njia iliyo sahihi.

28:27 Isa 21:10; Ay 41:30; Isa 10:5Iliki haipurwi kwa nyundo,

wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;

iliki hupurwa kwa fimbo,

na jira kwa ufito.

28:28 Isa 21:10Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,

kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.

Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,

farasi wake hawasagi.

28:29 Yer 32:19; Za 92:5; Rum 11:33; Isa 9:5Haya yote pia hutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote,

mwenye mashauri ya ajabu, na anayepita wote kwa hekima.

Read More of Isaya 28