Waebrania 6:13-20, Waebrania 7:1-10 NEN

Waebrania 6:13-20

Uhakika Wa Ahadi Ya Mungu

6:13 Mwa 22:16, 17; Lk 1:73; Za 105:9Mungu alipompa Abrahamu ahadi yake, kwa kuwa hakuwepo mwingine aliyekuwa mkuu kuliko yeye ambaye angeweza kuapa kwa jina lake, aliapa kwa nafsi yake, 6:14 Mwa 22:17akisema, “Hakika nitakubariki na kukupa wazao wengi.” 6:15 Mwa 21:5Abrahamu naye, baada ya kungoja kwa saburi, alipokea kile kilichoahidiwa.

6:16 Kut 22:10Wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuwaliko, nacho kiapo hicho huthibitisha kile kilichosemwa na hivyo humaliza mabishano yote. 6:17 Ebr 6:18; Za 110:4; Rum 4:16; Ebr 11:9; Rum 11:29Mungu alipotaka kuonyesha kwa udhahiri zaidi ile asili ya kutokubadilika kwa ahadi yake kwa warithi wa ahadi, aliithitibisha kwa kiapo. 6:18 Hes 23:19; Tit 1:2; Ebr 3:6Mungu alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyobadilika, yaani ahadi yake na kiapo chake, ambavyo kwavyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi ambao tumemkimbilia ili tulishike lile tumaini lililowekwa mbele yetu tuwe na faraja thabiti. 6:19 Law 16:2; Ebr 9:2, 3, 7Tunalo tumaini hili kama nanga ya roho iliyo imara na thabiti. Tumaini hili huingia katika sehemu takatifu iliyopo nyuma ya pazia, 6:20 Ebr 4:14; 2:17; 5:6mahali ambapo Yesu mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki.

Read More of Waebrania 6

Waebrania 7:1-10

Kuhani Melkizedeki

7:1 Za 76:2; Mk 5:7; Ebr 7:6; Mwa 14:18-20Kwa kuwa huyu Melkizedeki alikuwa mfalme wa Salemu na kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. Alipokutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwashinda hao wafalme, Melkizedeki alimbariki, naye Abrahamu alimpa sehemu ya kumi7:2 Sehemu ya kumi mahali pengine huitwa fungu la kumi au zaka; sehemu ya kumi ya pato hutolewa kwa Mungu. ya kila kitu. Kwanza, jina hilo Melkizedeki maana yake ni “mfalme wa haki.” Na pia “mfalme wa Salemu” maana yake ni “mfalme wa amani.” 7:3 Ebr 7:6; Mt 4:3; Za 110:4Hana Baba wala mama, hana ukoo, hana mwanzo wala mwisho wa siku zake. Kama Mwana wa Mungu, yeye adumu akiwa kuhani milele.

7:4 Mwa 14:20; Mdo 2:29Tazama jinsi alivyokuwa mkuu: Hata Abrahamu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya nyara zake. 7:5 Hes 18:21, 26Basi sheria inawaagiza wana wa Lawi ambao hufanyika makuhani kupokea sehemu ya kumi kutoka kwa watu ambao ni ndugu zao, ingawa ndugu zao ni wazao wa Abrahamu. 7:6 Mwa 14:19, 20; Rum 4:13Huyu Melkizedeki, ingawa hakufuatia ukoo wake kutoka kwa Lawi, lakini alipokea sehemu ya kumi kutoka kwa Abrahamu na kumbariki yeye aliyekuwa na zile ahadi. Wala hakuna shaka kwamba mdogo hubarikiwa na aliye mkuu kumliko yeye. 7:8 Ebr 5:6; 6:20Kwa upande mmoja, sehemu ya kumi hupokelewa na wale ambao hupatikana na kufa; lakini kwa upande mwingine hupokelewa na yeye ambaye hushuhudiwa kuwa yu hai. Mtu anaweza hata kusema kwamba Lawi, ambaye hupokea sehemu ya kumi, alitoa hiyo sehemu ya kumi kupitia kwa Abrahamu, kwa sababu Melkizedeki alipokutana na Abrahamu, Lawi alikuwa bado katika viuno vya baba yake wa zamani.7:10 Yaani, alikuwa hajazaliwa.

Read More of Waebrania 7