Mwanzo 14:1-24, Mwanzo 15:1-21, Mwanzo 16:1-16 NEN

Mwanzo 14:1-24

Abramu Amwokoa Loti

14:1 Mwa 10:10, 20Wakati huu Amrafeli mfalme wa Shinari, Arioko mfalme wa Elasari, Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu 14:2 Mwa 10:19; 13:10kwa pamoja walikwenda kupigana vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha mfalme wa Gomora, Shinabu mfalme wa Adma, Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari). 14:3 Hes 34:3-12; Kum 3:17; Yos 3:16; 12:3; 15:2-5; 18:19Hawa wote waliotajwa mwishoni waliunganisha majeshi yao kutoka Bonde la Sidimu (yaani Bahari ya Chumvi). Walikuwa wametawaliwa na Mfalme Kedorlaoma kwa miaka kumi na miwili, lakini mwaka wa kumi na tatu waliasi.

14:5 Mwa 15:20; Kum 2:10, 11, 20; 3:11-13; Yos 12:4; 13:12; 17:15; 1Nya 20:4Mnamo mwaka wa kumi na nne, Mfalme Kedorlaoma na wafalme waliojiunga naye walikwenda kupigana na kuwashinda Warefai katika Ashtaroth-Kanaimu, Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe-Kiriathaimu, 14:6 Mwa 21:21; 36:20; 32:3; 33:14-16; 36:8; Kum 2:11, 22; Yos 11:17; 24:4; 1Nya 4:42; Isa 34:5; Eze 25:8; 35:2; Amo 1:6; Hes 12:16; 10:12; 13:3, 26; Hab 3:3na Wahori katika nchi ya kilima cha Seiri, hadi El-Parani karibu na jangwa. 14:7 Mwa 16:14; 20:1; Hes 13:26; 20:1; 32:8; Kum 1:2; 25:17; 29:23; Yos 10:41; Amu 3:13; 6:3; 10:12; 12:15; 11:16; Za 29:8; 83:7; Kut 17:8; Hes 13:29; 14:25; 24:20; 1Sam 14:48; 15:2; 28:18; 2Sam 1:1; 1Nya 4:43; Hos 11:8Kisha wakarudi wakaenda En-Misfati (yaani Kadeshi), wakashinda nchi yote ya Waamaleki, pamoja na Waamori waliokuwa wakiishi Hasason-Tamari.

14:8 Mwa 13:10; 19:17-29; Hos 11:8; Kum 29:23Ndipo mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela (yaani Soari) wakatoka kupanga majeshi yao kwenye Bonde la Sidimu 14:9 Mwa 10:22dhidi ya Kedorlaoma, mfalme wa Elamu, Tidali mfalme wa Goimu, Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, yaani wafalme wanne dhidi ya wafalme watano. 14:10 Mwa 11:3; Za 11:1; Yos 2:16; 19:17, 30Basi Bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, nao wafalme wa Sodoma na wa Gomora walipokimbia, baadhi ya watu walitumbukia huko na wengine wakakimbilia vilimani. Wale wafalme wanne wakateka mali yote ya Sodoma na Gomora pamoja na vyakula vyao vyote, kisha wakaenda zao. 14:12 Mwa 11:27Pia walimteka Loti mwana wa ndugu yake Abramu pamoja na mali zake, kwa kuwa alikuwa akiishi Sodoma.

14:13 Mwa 13:18; 37:28; 39:14-17; 40:15; 41:12; 43:32; Kut 3:18; 1Sam 4:6; 14:11; Hes 13:23; 32:9; Kum 1:24Mtu mmoja aliyekuwa ametoroka akaja kumpa Abramu Mwebrania taarifa. Wakati huu Abramu alikuwa anaishi karibu na mialoni ya Mamre Mwamori, aliyekuwa ndugu yake Eshkoli na Aneri, ambao wote walikuwa wameungana na Abramu. 14:14 Kum 4:9; 34:1; Mit 22:6; Mwa 12:5; Amu 18:29; 1Fal 15:20Abramu alipopata habari kwamba jamaa yake amechukuliwa mateka, akawaita watu 318 wa nyumbani mwake waliokuwa wamefunzwa kupigana vita, wakawafuatilia hadi Dani. 14:15 Amu 1:3-8; 7:16; 15:2; 2Sam 8:5; 1Fal 20:34; 2Fal 16:9; Isa 7:8; 8:4; 10:9; 17:1; Yer 49:23, 27; Eze 27:18Wakati wa usiku Abramu aliwagawa watu wake katika vikosi ili awashambulie, na akawafuatilia, akawafukuza hadi Hoba, kaskazini ya Dameski. 14:16 1Sam 30:8, 18Akarudisha mali zote, na akamrudisha Loti jamaa yake na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.

14:17 2Sam 18:18Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme).

14:18 Za 7:8; 76:2; 104:15; 110:4; Ebr 7:2, 17, 21; 5:6; Mwa 3:19; Amu 9:13; 19:19; Es 1:10; Mit 31:6; Mhu 10:19; Wim 1:2; Dan 7:27Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana. 14:19 Ebr 7:6; Mwa 1:1; 24:3; Yos 2:11; Za 148:5; Mt 11:25Naye akambariki Abramu, akisema,

“Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye Juu Sana,

Muumba wa mbingu na nchi.

14:20 Mwa 9:26; 24:27; 28:22; Kum 14:22; 26:12; Lk 18:12; Ebr 7:4Abarikiwe Mungu Aliye Juu Sana,

ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.”

Ndipo Abramu akampa Melkizedeki sehemu ya kumi ya kila kitu.

Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, “Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe.”

14:22 Kut 6:8; Hes 14:30; Neh 9:15; Kum 32:40; Eze 20:5; Dan 12:7; Ufu 10:5-6Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua mkono wangu kwa Bwana, Mungu Aliye Juu Sana, Muumba wa mbingu na dunia, na nimeapa 14:23 1Sam 15:3, 19; 2Fal 5:16; Es 8:11; 9:10-15kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, ‘Nimemtajirisha Abramu.’ 14:24 Mwa 13:18Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”

Read More of Mwanzo 14

Mwanzo 15:1-21

Agano La Mungu Na Abramu

15:1 1Sam 3:10; 15:10; 2Sam 7:4; 22:3, 31; 1Fal 6:11; 12:22; Yer 1:8, 13; Eze 3:16; Dan 10:1; Mwa 21:17; 26:24; 46:3; 46:2; Rut 1:20; Hes 12:6; 24:4; Ay 33:15; Kut 14:13; 20:20; 2Fal 6:16; Hag 2:5; 2Nya 20:15-17; Za 3:3; 5:12; 18:2, 20; 37:25; 58:11; 28:7; 33:20; 84:11; 119:114; 144:2; 27:1; Isa 7:4; 41:10-14; 43:1, 5; Kum 33:29; Mit 2:7; 30:5Baada ya jambo hili, neno la Bwana likamjia Abramu katika maono:

“Usiogope, Abramu.

Mimi ni ngao yako,

na thawabu yako kubwa sana.”

15:2 Isa 49:22; Yer 44:26; Eze 5:11; 16:48; Mdo 7:5; Mwa 14:15Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” 15:3 Mwa 24:2, 34; 12:5Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.”

15:4 Gal 4:28Ndipo neno la Bwana lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” 15:5 Ay 11:8; 35:5; Za 8:3; 147:4; Yer 30:19; 33:22; Mwa 12:2; Rum 4:18; Ebr 11:12; Kut 32:13Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”

15:6 Za 106:31; Rum 4:3, 20-24; Gal 3:6; Yak 2:23Abramu akamwamini Bwana, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

15:7 Mwa 12:1; 13:17; 17:8; 28:4; 35:12; 48:4; Kut 6:8; 20:2; Mdo 7:3; Ebr 11:8; Kum 9:5Pia akamwambia, “Mimi ndimi Bwana, niliyekutoa toka Uru ya Wakaldayo nikupe nchi hii uimiliki.”

15:8 Lk 1:18; Kum 12:20; 19:8Lakini Abramu akasema, “Ee Bwana Mwenyezi, nitawezaje kujua kwamba nitapata kuimiliki?”

15:9 Hes 19:2; Kum 21:3; Hos 4:16; Amo 4:1; 1Sam 1:24; Law 1:14; 5:7, 11; 12:8Ndipo Bwana akamwambia, “Niletee mtamba wa ngʼombe, mbuzi na kondoo dume, kila mmoja wa miaka mitatu, pamoja na hua na kinda la njiwa.”

15:10 Yer 34:18; Law 1:17; 5:8Abramu akamletea hivi vyote, akampasua kila mnyama vipande viwili, akavipanga kila kimoja kuelekea mwenzake, lakini hata hivyo ndege, hakuwapasua vipande viwili. 15:11 Kum 28:26; Yer 7:33Kisha ndege walao nyama wakatua juu ya mizoga, lakini Abramu akawafukuza.

15:12 Mwa 2:21Wakati jua lilipokuwa linatua, Abramu akashikwa na usingizi mzito, giza nene na la kutisha likaja juu yake. 15:13 Kut 1:11; 3:7; 5:6-14; 12:40; Ay 3:18; Kum 5:15; Mdo 7:6; Hes 20:15; Gal 3:17Kisha Bwana akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. 15:14 Mwa 50:24; Kut 3:8; 6:6-8; 12:25; 12:32-38; Hes 10:29; Yos 1:2; Mdo 7:7Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. 15:15 Mwa 25:8; 35:29; 47:30; 49:29; Kum 31:16; 34:7; 2Sam 7:12; 1Fal 1:21; Za 49:19; 91:16; Kut 23:29; Yos 14:11; Amu 8:32; 1Nya 29:28; Ay 5:26; 21:23; 42:17; Mit 3:16; 9:11; Isa 65:20Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema. 15:16 Kut 3:8, 17; 12:40; Mwa 28:15; 46:4; 48:21; 50:24; Law 18:28; Yos 13:4; Amu 10:11; Eze 16:3; 1Fal 21:26; 2Fal 16:3; 21:11Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

15:17 Amu 7:16-20; 14:4-5Wakati jua lilipokuwa limezama na giza limeingia, tanuru la moshi na mwali wa moto unaowaka vikatokea na kupita kati ya vile vipande vya nyama. 15:18 Mwa 2:14; 4:7; 12:7; 17:2-7; Kut 6:4; 34:10, 27; 1Nya 16:16; Za 105:9; Hes 34:5; Isa 27:12; Yos 15:4, 47; 1Fal 8:65; 2Fal 24:7; 2Nya 7:8; Yer 37:5; 46:2; Mao 4:17; Eze 30:22; 47:19Siku hiyo Bwana akafanya Agano na Abramu, na kumwambia, “Nitawapa wazao wako nchi hii, kuanzia Kijito cha Misri15:18 Kijito cha Misri hapa ina maana Wadi-el-Arish kwenye mpaka wa kusini wa Yuda. hadi mto ule mkubwa, Frati, 15:19 Hes 24:21; Amu 1:16; 4:11; 5:24; 1Sam 15:6; 27:10; 30:29; 1Nya 2:55yaani nchi ya Wakeni, Wakenizi, Wakadmoni, 15:20 Mwa 10:15; Kum 7:1; Mwa 13:7; 14:5Wahiti, Waperizi, Warefai, 15:21 Mwa 10:16; Yos 3:10; 24:11; Neh 9:8Waamori, Wakanaani, Wagirgashi na Wayebusi.”

Read More of Mwanzo 15

Mwanzo 16:1-16

Hagari Na Ishmaeli

16:1 Mwa 11:29, 30; 24:61; 29:24-29; 31:33; 46:18; 21:14; 25:12; 30:2; Lk 1:7, 36; Gal 4:24-25Basi Sarai, mkewe Abramu, alikuwa hajamzalia watoto. Lakini alikuwa na mtumishi wa kike Mmisri jina lake Hagari, 16:2 Mwa 19:31-32; 30:3-10hivyo Sarai akamwambia Abramu, “Bwana amenizuilia kupata watoto. Nenda, ukakutane kimwili na mtumishi wangu wa kike, huenda nitaweza kupata watoto kupitia kwake.”

Abramu akakubaliana na lile Sarai alilosema. 16:3 Mwa 12:4-5Hivyo baada ya Abramu kuishi katika nchi ya Kanaani miaka kumi, Sarai akamchukua mtumishi wake wa kike wa Kimisri, Hagari na kumpa mumewe awe mke wake. 16:4 Mwa 30:1; 1Sam 1:6Akakutana kimwili na Hagari, naye akapata mimba.

Hagari alipojua kuwa ana mimba, alianza kumdharau Sarai. 16:5 Mwa 31:53; Kut 5:21; Amu 11:27; 1Sam 24:12-15; 26:10, 23; Za 50:6; 75:7Ndipo Sarai akamwambia Abramu, “Unawajibika na manyanyaso ninayoyapata. Nilimweka mtumishi wangu mikononi mwako, sasa kwa vile anajua kwamba ana mimba, ananidharau mimi. Bwana na aamue kati yako na mimi.”

16:6 Yos 9:25; Mwa 31:50Abramu akamwambia, “Mtumishi wako yuko mikononi mwako. Mtendee lolote unalofikiri ni bora zaidi.” Ndipo Sarai akamtesa Hagari, hivyo akamtoroka.

16:7 Mwa 21:17; 22:11-15; 24:7, 40; 25:18; 31:11; 48:16; Kut 3:2; 14:19; 15:22; 23:20-23; 32:34; 33:2; Amu 2:1; 6:11; 13:3; Za 34:7; 2Sam 24:16; 21:19; 1Fal 19:5; 2Fal 1:3; 19:35; Zek 1:11; Mdo 5:19; 1Sam 15:7Malaika wa Bwana akamkuta Hagari karibu na chemchemi huko jangwani; ilikuwa chemchemi ile iliyokuwa kando ya barabara iendayo Shuri. 16:8 Mwa 3:9Malaika akamwambia, “Hagari, mtumishi wa Sarai, umetokea wapi, na unakwenda wapi?”

Akamjibu, “Ninamkimbia bibi yangu Sarai.”

Ndipo malaika wa Bwana akamwambia, “Rudi kwa bibi yako ukajishushe chini yake.” 16:10 Mwa 13:16; 17:20Malaika akaendelea akasema, “Nitazidisha wazao wako, hivi kwamba watakuwa wengi mno wasiohesabika.”

16:11 Mdo 5:19; Mwa 3:15; 12:2-3; 18:19; 17:19; 21:3; 37:25-28; 29:32; 31:42; Neh 9:7; Isa 44:1; Amo 3:2; Mt 1:21; Lk 1:13, 31; Amu 8:24; Kut 2:24; 3:7, 9; 4:31; Hes 20:16; Kum 26:7; 1Sam 9:16Pia malaika wa Bwana akamwambia:

“Wewe sasa una mimba

nawe utamzaa mwana.

Utamwita jina lake Ishmaeli,16:11 Ishmaeli maana yake Mungu husikia.

kwa sababu Bwana amesikia juu ya huzuni yako.

16:12 Ay 6:5; 11:12; 24:5; 39:5; Hos 8:9; Za 104:11; Yer 2:24; Mwa 25:18Atakuwa punda-mwitu katikati ya wanadamu,

mkono wake utakuwa dhidi ya kila mtu

na mkono wa kila mtu dhidi yake,

naye ataishi kwa uhasama

na ndugu zake wote.”

16:13 Za 139:1-12; Mwa 32:30; 33:10; Kut 24:10; 33:20-23; Hes 12:8; Amu 6:22; 13:22; Isa 6:5Hagari akampa Bwana aliyezungumza naye jina hili: “Wewe ndiwe Mungu unionaye mimi,” kwa maana alisema, “Sasa nimemwona yeye anayeniona mimi.” 16:14 Mwa 24:62; 25:11; 14:7Ndiyo sababu kisima kile kikaitwa Beer-Lahai-Roi,16:14 Beer-Lahai-Roi maana yake Yeye Aliye Hai Anionaye Mimi. ambacho bado kipo huko hata leo kati ya Kadeshi na Beredi.

16:15 Mwa 21:9; 17:18; 25:12; 28:9; Gal 4:22Hivyo Hagari akamzalia Abramu mwana, naye Abramu akamwita huyo mwana Hagari aliyemzalia, Ishmaeli. 16:16 Mwa 12:4Abramu alikuwa na umri wa miaka themanini na sita wakati Hagari alipomzalia Ishmaeli.

Read More of Mwanzo 16