Wagalatia 3:26-29, Wagalatia 4:1-20 NEN

Wagalatia 3:26-29

Watoto Wa Mungu

3:26 Rum 8:14; Yn 1:12; Rum 8:15, 16; Gal 4:5; 1Yn 3:1Kwa maana ninyi nyote mmekuwa watoto wa Mungu katika Kristo Yesu kwa njia ya imani. 3:27 Rum 6:3; 13:14; Mt 28:19Kwa maana wote mliobatizwa ndani ya Kristo, mmemvaa Kristo. 3:28 1Kor 12:13; Kol 3:11; Mwa 1:27; 5:2; Yoe 2:29; Yn 10:16Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Kristo Yesu. 3:29 1Kor 3:22; Gal 3:16; Lk 3:8; Rum 8:17; Gal 3:16Nanyi mkiwa ni mali ya Kristo, basi ninyi ni wa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ile ahadi.

Read More of Wagalatia 3

Wagalatia 4:1-20

Lile nisemalo ni kwamba wakati wote mrithi bado ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ndiye mmiliki wa mali yote. Yeye huwa yuko chini ya uangalizi wa walezi na wadhamini mpaka ufike wakati uliowekwa na baba yake. 4:3 Gal 4:9; 5:1; Kol 2:8, 20; Ebr 9:10Vivyo hivyo na sisi, tulipokuwa bado watoto wadogo, tulikuwa utumwani chini ya taratibu za kawaida za ulimwengu. 4:4 Mk 1:15; Rum 5:6; Efe 1:10; Yn 3:17; 1:14; Lk 2:27Lakini ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe, ambaye alizaliwa na mwanamke, akazaliwa chini ya sheria, 4:5 Rum 3:24; Yn 1:12; Rum 8:14kusudi awakomboe wale waliokuwa chini ya sheria, ili tupate kupokea zile haki kamili za kufanywa watoto wa Mungu. 4:6 Mdo 16:7; Rum 5:5; 8:15, 16Kwa sababu ninyi ni watoto wa Mungu, Mungu amemtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, anayelia, “Abba,4:6 Abba ni neno la Kiaramu ambalo maana yake ni Baba; lingeweza kutumiwa tu na mtoto wa kuzaa. Baba.” 4:7 Rum 8:17; Gal 3:29Kwa hiyo, wewe si mtumwa tena, bali ni mtoto, kwa kuwa wewe ni mtoto, Mungu amekufanya wewe pia kuwa mrithi kwa kupitia Kristo.

Paulo Awashawishi Wagalatia

4:8 Rum 1:28; 1Kor 1:21; 15:34; 1The 4:5; 2The 1:8; Gal 4:3Zamani, mlipokuwa hammjui Mungu, mlikuwa watumwa wa viumbe ambavyo kwa asili si Mungu. 4:9 1Kor 8:3; Gal 4:3; Kol 2:20Lakini sasa kwa kuwa mmemjua Mungu, au zaidi mmejulikana na Mungu, inakuwaje mnarejea tena katika zile kanuni za kwanza zenye udhaifu na upungufu? Mnataka ziwafanye tena watumwa? 4:10 Rum 14:5; Kol 2:16Mnaadhimisha siku maalum, miezi, nyakati na miaka! 4:11 1The 3:5; Gal 2:2; 5:2, 4Nina hofu juu yenu, kwamba kazi niliyofanya kwa ajili yenu inaweza kuwa nimejitaabisha bure.

4:12 Rum 7:1; Gal 6:18; 2Kor 2:5Ndugu zangu, nawasihi mwe kama mimi, kwa sababu mimi nimekuwa kama ninyi. Hamkunitendea jambo lolote baya. 4:13 1Kor 2:3; 2Kor 11:30; 12:7, 9; Gal 1:6Ninyi mwajua kwamba ni kwa ajili ya udhaifu wangu niliwahubiria Injili. 4:14 Mt 10:40; 2Sam 19:27; Mal 2:7; Zek 12:8; Mt 10:40; Lk 10:16Ingawa hali yangu iliwatia majaribuni, hamkunidharau wala kunidhihaki, bali mlinikaribisha kama malaika wa Mungu, kama vile Kristo Yesu. Ile hali ya furaha mliyokuwa nayo imekwenda wapi? Naweza kushuhudia kwamba, kama ingewezekana mngengʼoa macho yenu na kunipa mimi. 4:16 Gal 2:5, 14; Amo 5:10Je, sasa nimekuwa adui yenu kwa kuwaambia kweli?

4:17 Gal 2:4, 12; Rum 10:12; 1Kor 11:2Hao wana shauku ya kuwapata lakini si kwa kusudi zuri. Wanachotaka ni kuwatenga mbali nasi, ili ninyi mpate kuwaonea wao shauku. 4:18 Gal 4:13, 14Ni vizuri wakati wote kuwa na shauku kwa ajili ya kusudi zuri, si wakati nikiwa pamoja nanyi tu. 4:19 1The 2:11; Rum 8:29; Efe 4:13Watoto wangu wapendwa, ambao kwa mara nyingine ninawaonea utungu, ninatamani kwamba Kristo aumbike ndani yenu. Natamani kama ningekuwa pamoja nanyi sasa, pengine ningebadilisha sauti yangu. Kwa maana nina wasiwasi kwa ajili yenu.

Read More of Wagalatia 4