Ezekieli 4:1-17, Ezekieli 5:1-17, Ezekieli 6:1-14 NEN

Ezekieli 4:1-17

Kuzingirwa Kwa Yerusalemu Kwaonyeshwa Kwa Mfano

“Mwanadamu, sasa chukua tofali, uliweke mbele yako na uchore juu yake ramani ya mji wa Yerusalemu. 4:2 Yer 6:6; Dan 11:15; Eze 21:22; Yer 33:4; Eze 17:17Kisha uuzingire: Simamisha askari dhidi yake kuuzunguka, uzunguke kwa majeshi, weka kambi dhidi yake pande zote pamoja na magogo ya kubomolea boma vitani. 4:3 Eze 20:3; Yer 13:1-7; 39:1; Isa 8:18; Law 2:5; Eze 20:46; 12:3-6Kisha chukua bamba la chuma, ukalisimamishe liwe kama ukuta wa chuma kati yako na huo mji, nawe uuelekeze uso wako. Huo mji utakuwa katika hali ya kuzingirwa, nawe utauzingira. Hii itakuwa ishara kwa nyumba ya Israeli.

“Kisha ulale kwa upande wako wa kushoto na uweke dhambi za nyumba ya Israeli juu yake. Utazibeba dhambi zao kwa idadi ya siku utakazolala kwa huo upande mmoja. 4:5 Hes 14:34Nimekupangia idadi ya siku kama miaka ya dhambi yao. Kwa hiyo kwa siku 390 utabeba dhambi za nyumba ya Israeli.

4:6 Hes 14:34; Dan 12:11-12; 9:24-26; Kut 28:38“Baada ya kumaliza hili, lala chini tena, wakati huu ulale chini kwa upande wa kuume, uchukue dhambi za nyumba ya Yuda. Nimekupangia siku arobaini, siku moja kwa kila mwaka mmoja. 4:7 Eze 6:2; 13:17Geuza uso wako uelekeze kwenye kuzingirwa kwa Yerusalemu na mkono wako ambao haukuvikwa nguo tabiri dhidi yake. 4:8 Eze 3:25Nitakufunga kwa kamba ili usiweze kugeuka kutoka upande mmoja hadi upande mwingine, mpaka hapo utakapokuwa umetimiza siku za kuzingirwa kwako.

4:9 Isa 28:25“Chukua ngano na shayiri, maharagwe na dengu, mtama na mawele, uviweke na kuvihifadhi vyote kwenye gudulia la kuhifadhia, na uvitumie kujitengenezea mkate. Utaula mkate huo kwa hizo siku 390 utakazokuwa umelala kwa upande mmoja. 4:10 Kut 30:13Pima shekeli ishirini4:10 Shekeli 20 ni sawa na gramu 200. za chakula utakachokula kwa kila siku, nawe utakula kwa wakati uliopangwa. 4:11 Eze 4:16Pia pima maji moja ya sita ya hini,4:11 Moja ya sita ya hini ni sawa na mililita (ml) 600. nawe utakunywa kwa wakati uliopangwa. 4:12 Isa 36:12Nawe utakula chakula kama vile ambavyo ungekula mkate wa shayiri, uoke mkate mbele ya macho ya watu, ukitumia kinyesi cha mwanadamu.” 4:13 Hos 9:3; Amo 7:17Bwana akasema, “Hivi ndivyo watu wa Israeli watakavyokula chakula kilicho najisi miongoni mwa mataifa ninakowapeleka.”

4:14 Eze 20:49; Law 11:39; Dan 1:8; Mdo 10:14; Kum 14:3; Hos 9:3-4; Eze 20:49Ndipo nikasema, “Sivyo Bwana Mwenyezi! Kamwe mimi sijajitia unajisi. Tangu ujana wangu hadi sasa sijala kamwe kitu chochote kilichokufa au kilichoraruliwa na wanyama wa mwituni. Hakuna nyama yeyote najisi iliyoingia kinywani mwangu.”

Akasema, “Vema sana, basi nitakuruhusu uoke mkate wako kwa kutumia kinyesi cha ngʼombe badala ya kinyesi cha mwanadamu.”

4:16 Za 105:16; Eze 5:16; Law 26:26; Isa 3:1; Eze 12:19Ndipo Mungu akaniambia, “Mwanadamu, mimi nitakatilia mbali upatikanaji wa chakula katika Yerusalemu. Watu watakula chakula cha kupimwa kwa wasiwasi pamoja na maji ya kupimiwa kwa kukata tamaa, 4:17 Law 26:39; Eze 33:10; 24:23; 5:16; 12:18-19; Amo 4:8kwa kuwa chakula na maji vitakuwa adimu. Watastajabiana kila mmoja, nao watadhoofika kwa sababu ya dhambi yao.

Read More of Ezekieli 4

Ezekieli 5:1-17

Upanga Dhidi Ya Yerusalemu

5:1 Law 21:5; Isa 7:20; Eze 44:20; Hes 6:5; 2Sam 10:14“Mwanadamu, sasa chukua upanga mkali na uutumie kama wembe wa kinyozi ili kunyolea nywele za kichwa chako na ndevu zako. Kisha uchukue mizani ya kupimia ukazigawanye nywele hizo. 5:2 Law 26:33; Yer 39:1-2; Zek 13:8; Yer 21:10; Eze 15:7; Yer 13:24; 9:16Wakati siku zako za kuzingirwa zitakapokwisha, choma theluthi moja ya hizo nywele zako kwa moto ndani ya mji. Chukua theluthi nyingine ya hizo nywele uzipige kwa upanga kuuzunguka mji wote na theluthi nyingine ya mwisho utaitawanya kwa upepo. Kwa kuwa nitawafuatia kwa upanga uliofutwa. 5:3 Yer 40:6; 39:10; 2Fal 25:12; Za 74:11Lakini chukua nywele chache uzifungie ndani ya pindo la vazi lako. 5:4 Eze 10:7; 15:7Tena chukua nywele nyingine chache uzitupe motoni uziteketeze. Moto utaenea kutoka humo na kufika katika nyumba yote ya Israeli.

5:5 Kum 4:6; Mao 1:1; Eze 16:14“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Huu ndio Yerusalemu ambao nimeuweka katikati ya mataifa ukiwa umezungukwa na nchi pande zote. 5:6 Neh 9:17; Zek 7:11; Rum 1:25; Eze 16:16; 2Fal 17:15; Yer 11:10Lakini katika uovu wake umeasi sheria na amri zangu kuliko mataifa na nchi zinazouzunguka. Umeasi sheria zangu wala haukufuata amri zangu.

5:7 2Fal 21:9; 2Nya 33:9; Yer 2:10-11“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninyi mmekuwa wakaidi kuliko mataifa yanayowazunguka na hamkufuata amri zangu wala kuzishika sheria zangu. Wala hamkuweza hata kuzifuata kawaida za mataifa yanayowazunguka.

5:8 Yer 21:5; Zek 14:2; Yer 24:9; Eze 11:9; 15:7“Kwa hiyo, hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo, Mimi mwenyewe, niko kinyume nanyi Yerusalemu, nitawapiga kwa adhabu yangu mbele ya mataifa. 5:9 Dan 9:12; Amo 3:2; Mt 24:21Kwa ajili ya sanamu zenu zote za machukizo, nitawafanyia kile ambacho kamwe sijawafanyia kabla wala kamwe sitawafanyia tena. 5:10 Law 26:29; Mao 2:20; Yer 13:14; Zek 2:6; Za 44:11; Eze 12:14Kwa hiyo katikati yenu baba watakula watoto wao na watoto watakula baba zao. Nitawapiga kwa adhabu, nami nitawatawanya watu wenu walionusurika pande zote za dunia. 5:11 Eze 7:20; 8:6; 2Nya 36:14; Eze 11:18-21; Yer 16:18; Ay 27:22; Hes 14:21; Law 15:2; 15:31; Mao 2:17Kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, kwa kuwa mmenajisi mahali pangu patakatifu kwa sanamu zenu mbaya sana na desturi zenu za machukizo, mimi mwenyewe nitaondoa fadhili zangu kwenu. 5:12 Ufu 6:8; Za 107:39; Eze 12:14; Zek 13:8; Eze 6:11-12; Yer 21:9; 13:24Theluthi ya watu wako watakufa kwa tauni au kwa njaa humu ndani yako, theluthi nyingine itaanguka kwa upanga nje ya kuta zako, nayo theluthi nyingine nitaitawanya kwenye pande nne kuwafuatia kwa upanga uliofutwa.

5:13 2Nya 12:7; Ay 20:23; Isa 1:24; Mao 4:11; Eze 21:17; 24:13; Hos 10:10“Ndipo hasira yangu itakapokoma na ghadhabu yangu dhidi yao itatulia, nami nitakuwa nimelipiza kisasi. Baada ya kuimaliza ghadhabu yangu juu yao, watajua kuwa mimi Bwana nimenena katika wivu wangu.

5:14 Mik 3:12; Isa 64:11; Neh 2:17; Za 74:3-10; Eze 22:4; Dan 9:16“Nitakuangamiza na kukufanya kitu cha kudharauliwa miongoni mwa mataifa yanayokuzunguka, machoni pa watu wote wapitao karibu nawe. 5:15 Kum 28:20; 1Fal 9:7; Yer 23:40; Eze 25:17; Mao 2:15; Isa 43:28; Yer 22:8-9Utakuwa kitu cha kudharauliwa na cha aibu, cha dhihaka, ovyo na kitu cha kutisha kwa mataifa yanayokuzunguka, nitakapokupiga kwa adhabu yangu katika hasira na ghadhabu yangu kwa kukukemea kwa ukali. Mimi Bwana nimesema. 5:16 Law 26:26; Kum 32:24; Eze 14:21Nitakapokupiga kwa mishale yangu ya kufisha na yenye kuharibu ya njaa, nitaipiga ili kukuangamiza. Nitaleta njaa zaidi na zaidi juu yako na kukomesha upatikanaji wa chakula kwako. 5:17 Eze 38:23; Law 26:25; Eze 28:22Nitapeleka njaa na wanyama wa mwituni dhidi yenu, navyo vitawaacha bila watoto. Tauni na umwagaji wa damu utapita katikati yenu, nami nitaleta upanga juu yenu. Mimi Bwana nimenena haya.”

Read More of Ezekieli 5

Ezekieli 6:1-14

Unabii Dhidi Ya Milima Ya Israeli

Neno la Bwana likanijia kusema, 6:2 Eze 36:1; Mik 6:1; Eze 18:6; 4:7; 36:4; Law 26:30“Mwanadamu, elekeza uso wako kukabili milima ya Israeli, utabiri dhidi yake na useme: ‘Ee milima ya Israeli, sikia neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi aliambiayo milima na vilima, magenge na mabonde: Ninakaribia kuleta upanga dhidi yenu, nami nitapaharibu mahali penu pote pa juu pa kuabudia miungu. 6:4 2Nya 14:5; Yer 44:28; Eze 9:4; 14:3Madhabahu yenu yatabomolewa na madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatavunjavunjwa, nami nitawachinja watu wenu mbele ya sanamu zenu. 6:5 Hes 19:16; Za 53:5; Yer 8:1-2Nitazilaza maiti za Waisraeli mbele ya sanamu zao, nami nitatawanya mifupa yenu kuzunguka madhabahu yenu. 6:6 Mik 1:7; Zek 13:2; Law 26:30; Isa 6:11; 1Sam 5:4; Kut 12:20; Hos 10:8; Eze 30:13Popote mnapoishi, miji hiyo itafanywa ukiwa na mahali pa juu pa kuabudia miungu patabomolewa, ili madhabahu yenu ifanywe ukiwa na kuharibiwa, sanamu zenu zitavunjavunjwa na kuharibiwa, madhabahu yenu ya kufukizia uvumba yatabomolewa na kila mlichokifanya kitakatiliwa mbali. 6:7 Eze 9:7; 6:13; 7:4, 9; 11:10, 12; 12:15Watu wenu watachinjwa katikati yenu, nanyi mtatambua Mimi ndimi Bwana.

6:8 Za 68:20; 44:11; Yer 44:28; Mwa 11:4; Isa 6:13; Eze 7:16; 12:16; 14:22“ ‘Lakini nitawabakiza hai baadhi yenu, kwa kuwa baadhi yenu watanusurika kuuawa watakapokuwa wametawanyika katika nchi na mataifa. 6:9 Za 78:40; Yer 8:21; Isa 7:13; Mik 5:13; Kut 22:20; Ay 42:6; Eze 36:31Ndipo katika mataifa ambamo watakuwa wamechukuliwa mateka, wale ambao watanusurika watanikumbuka, jinsi ambavyo nimehuzunishwa na mioyo yao ya uzinzi, ambayo imegeukia mbali nami na macho yao ambayo yametamani sanamu zao. Watajichukia wenyewe kwa ajili ya uovu walioutenda na kwa ajili ya desturi zao za kuchukiza. 6:10 Zek 10:9; Eze 20:43; Kum 28:52; Yer 40:2Nao watajua kuwa Mimi ndimi Bwana, sikuwaonya bure kuwa nitaleta maafa hayo yote juu yao.

6:11 Yer 42:22; Eze 22:13; 21:14-17; 25:6“ ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Piga makofi, kanyaga chini kwa mguu na upige kelele, “Ole!” kwa sababu ya maovu yote na machukizo yote yanayofanywa na nyumba ya Israeli, kwa kuwa wataanguka kwa upanga, njaa na tauni. 6:12 Eze 5:12; 7:15; Ay 20:23Yeye aliye mbali sana atakufa kwa tauni, naye aliye karibu atauawa kwa upanga, naye yule atakayenusurika na kubaki atakufa kwa njaa. Hivyo ndivyo nitakavyotimiza ghadhabu yangu dhidi yao. 6:13 Isa 1:29; 57:5; Hos 4:13; Eze 18:6; Law 26:30; 1Fal 14:23; Yer 2:20; Eze 20:28Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, wakati maiti za watu wao zitakapokuwa zimelala katikati ya sanamu zao kuzunguka madhabahu yao, juu ya kila kilima kilichoinuka na juu ya vilele vyote vya milima, chini ya kila mti uliotanda na kila mwaloni wenye majani, yaani, sehemu walizofukizia uvumba kwa sanamu zao zote. 6:14 Kut 7:5; Ay 30:21; Eze 14:13; Isa 5:25; Yer 6:12; Eze 12:19; 20:34Nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yao na kuifanya nchi yao ukiwa, kuanzia jangwani hadi Dibla, kila mahali wanapoishi. Ndipo watakapojua ya kwamba Mimi ndimi Bwana.’ ”

Read More of Ezekieli 6