Mhubiri 7:1-29, Mhubiri 8:1-17, Mhubiri 9:1-12 NEN

Mhubiri 7:1-29

Hekima

7:1 Ufu 14:13; Wim 1:3; Mit 22:1; Ay 10:18Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,

nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.

7:2 Za 90:12; Mit 11:19; Mhu 2:14Afadhali kwenda kwenye nyumba ya msiba

kuliko kwenda kwenye nyumba ya karamu,

kwa kuwa kifo ni hatima ya kila mwanadamu,

imewapasa walio hai kuliweka hili mioyoni mwao.

7:3 2Kor 7:10; Mit 14:13Huzuni ni afadhali kuliko kicheko,

kwa sababu uso wenye huzuni wafaa kwa moyo.

7:4 Mhu 2:1; Yer 16:8Moyo wa wenye hekima uko katika nyumba ya msiba,

lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya anasa.

7:5 Za 141:5; Mit 13:18; 15:31-32Afadhali kusikia karipio la mtu mwenye hekima,

kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.

7:6 Za 58:9; Mhu 2:2; Mit 14:13Kama ilivyo kuvunjika kwa miiba chini ya sufuria,

ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu.

Hili nalo pia ni ubatili.

7:7 Kut 18:21; 23:8; Kum 16:19Dhuluma humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu,

nayo rushwa huuharibu moyo.

7:8 Mit 14:29; Gal 5:22Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake,

uvumilivu ni bora kuliko kiburi.

7:9 Mit 16:32; 14:17, 29; Mt 5:22Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako,

kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.

Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?”

Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo.

7:11 Mit 8:10-11; Mhu 2:13; 11:7Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema

na huwafaidia wale walionalo jua.

Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi,

lakini faida ya maarifa ni hii:

kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

7:13 Isa 14:27; Mhu 2:24; 1:15Tafakari kile Mungu alichokitenda:

Nani awezaye kunyoosha

kile ambacho yeye amekipinda?

7:14 Ay 1:21; Mhu 2:24Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi,

lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:

Mungu amefanya hiyo moja,

naam, sanjari7:14 Sanjari hapa maana yake mwandamano wa vitu, wanyama au watu. na hiyo nyingine.

Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua

kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.

7:15 Mhu 8:14; Yer 12:1; Ay 21:7; 7:7Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili:

mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake,

naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake.

Usiwe mwenye haki kupita kiasi,

wala usiwe na hekima kupita kiasi:

kwa nini kujiangamiza mwenyewe?

7:17 Ay 15:32; Za 55:23Usiwe mwovu kupita kiasi,

wala usiwe mpumbavu:

kwa nini kufa kabla ya wakati wako?

7:18 Mhu 3:14Ni vyema kushika hilo moja

na wala usiache hilo jingine likupite.

Mtu amchaye Mungu ataepuka huko kupita kiasi.7:18 Au: atafuata hayo yote mawili.

7:19 Mhu 2:13; 9:13-18; Mit 8:14Hekima humfanya yeye aliye nayo kuwa na uwezo zaidi

kuliko watawala kumi katika mji.

7:20 1Fal 8:46; Rum 3:12, 23; Gal 3:22; Za 14:3; Mit 20:9; Ay 4:17Hakuna mtu mwenye haki duniani

ambaye hufanya mambo ya haki

na kamwe asitende dhambi.

7:21 Mit 30:10Usitie maanani kila neno linalosemwa na watu,

la sivyo, waweza kumsikia

mtumishi wako akikulaani:

kwa kuwa unafahamu moyoni mwako

kwamba wewe mwenyewe mara nyingi

umewalaani wengine.

7:23 Mhu 1:17; Rum 1:22Yote haya niliyajaribu kwa hekima, nikasema,

“Nimeamua kuwa na hekima”:

lakini hii ilikuwa nje ya uwezo wangu.

7:24 Ay 28:12; 11:12; Isa 55:8-9Vyovyote hekima ilivyo,

hekima iko mbali sana na imejificha,

ni nani awezaye kuigundua?

7:25 Ay 28:3; Mhu 1:17Nikageuza fikira zangu ili kuelewa,

kuchunguza na kuitafuta hekima

na kusudi la mambo,

na ili kuelewa ujinga wa uovu,

na wazimu wa upumbavu.

7:26 Kut 10:7; Amu 14:15; Mit 7:23; 22:14; 2:16-19; 5:3-5Nimeona jambo lililo chungu kuliko mauti,

mwanamke ambaye ni mtego,

ambaye moyo wake ni wavu wa kutegea

na mikono yake ni minyororo.

Mtu ampendezaye Mungu atamkwepa,

bali mwenye dhambi atanaswa naye.

Mhubiri anasema, “Tazama, hili ndilo nililogundua:

“Nimegundua kitu kimoja baada ya kingine nilipokuwa katika kusudi la mambo:

7:28 1Fal 11:3ningali natafiti

lakini sipati:

nilimpata mwanaume mmoja mnyofu miongoni mwa elfu,

lakini hakuna mwanamke mmoja mnyofu miongoni mwao.

Hili ndilo peke yake nililolipata:

Mungu amemuumba mwanadamu mnyofu,

lakini mwanadamu amebuni mambo mengi.”

Read More of Mhubiri 7

Mhubiri 8:1-17

Ni nani aliye kama mtu mwenye hekima?

Ni nani ajuaye maelezo ya mambo?

Hekima hungʼarisha uso wa mtu na kubadili ugumu wa uso wake.

Mtii Mfalme

Nawaambia, Tii amri ya mfalme, kwa sababu uliapa mbele za Mungu. 8:3 Rum 13:5; Mhu 10:4Usiharakishe kuondoka mbele ya mfalme. Usiendelee kutenda lililo baya, kwa maana mfalme atafanya lolote apendalo. 8:4 Ay 9:12; 34:18; Dan 4:35; Es 1:18-19Kwa kuwa neno la mfalme ndilo lenye mamlaka ya mwisho, nani awezaye kumwambia, “Je, wewe unafanya nini?”

Yeyote anayetii agizo lake hatadhurika,

moyo wa hekima utajua wakati muafaka

na jinsi ya kutenda.

8:6 Mhu 3:1Kwa maana kuna wakati muafaka

na utaratibu wa kila jambo,

ingawa huzuni ya mwanadamu

huwa nzito juu yake.

Kwa vile hakuna mtu ajuaye siku zijazo,

ni nani awezaye kumwambia linalokuja?

Hakuna mwanadamu

awezaye kushikilia roho yake asife,

wala hakuna mwenye uwezo

juu ya siku ya kufa kwake.

Kama vile hakuna yeyote arudishwaye nyuma wakati wa vita,

kadhalika uovu hautawaweka huru wale wautendao.

8:9 1Sam 18:12Yote haya niliyaona, nilipokuwa natafakari kila kitu kinachotendeka chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu hujifanya bwana juu ya wengine kwa madhara yake mwenyewe. Ndipo pia, nikaona waovu wakizikwa, wale ambao walizoea kuingia na kutoka mahali patakatifu na kupewa sifa katika mji ambapo walikuwa wamefanya haya. Hili nalo ni ubatili.

8:11 Ay 21:14-15; Rum 2:4-5; Isa 26:10Wakati hukumu juu ya tendo ovu haitekelezwi upesi, mioyo ya watu hujaa mipango ya kutenda maovu. 8:12 Za 37:18-19; Isa 3:10-11; 65:20; Mhu 3:14; Kum 4:40Ingawa mtu mwovu hufanya maovu mia moja na akaendelea kuishi maisha marefu, najua kwamba itakuwa bora zaidi kwa watu wanaomwogopa Mungu, wamchao Mungu. 8:13 Mhu 3:14; Kum 4:40; Ay 5:26; Za 34:12; Isa 65:20Lakini kwa sababu waovu hawamwogopi Mungu, hawatafanikiwa, maisha yao hayatarefuka kama kivuli.

8:14 Za 73:14; Mal 3:15; Mhu 2:14; 7:15; Ay 21:7Kuna kitu kingine ambacho ni ubatili kinachotokea duniani: Watu waadilifu kupata yale yanayowastahili waovu, nao waovu kupata yale yanayowastahili waadilifu. Hili nalo pia, nasema ni ubatili. 8:15 Law 26:5; Mhu 3:12-13; Kut 32:6; Za 42:8Kwa hiyo mimi ninasifu kufurahia maisha, kwa sababu hakuna kitu bora zaidi kwa mwanadamu chini ya jua kuliko kula, kunywa na kufurahi. Kisha furaha itafuatana naye kazini mwake siku zote za maisha yake ambazo amepewa na Mungu chini ya jua.

8:16 Mhu 1:13-17Nilipotafakari akilini mwangu ili nijue hekima na kuangalia kazi ya mwanadamu duniani, jinsi ambavyo macho yake hayapati usingizi mchana wala usiku, 8:17 Ay 5:9; 28:3, 23; Isa 40:28; Rum 11:33ndipo nikaona yale yote ambayo Mungu ameyafanya. Hakuna yeyote awezaye kuelewa yale yanayotendeka chini ya jua. Licha ya juhudi zake zote za kutafuta, mtu hawezi kugundua maana yake. Hata ingawa mtu mwenye hekima anadai kuwa anafahamu, kwa hakika hawezi kutambua.

Read More of Mhubiri 8

Mhubiri 9:1-12

Hatima Ya Wote

9:1 Mhu 8:14; 10:14; Kum 33:3; Ay 12:10Kwa hiyo niliyatafakari yote haya nikafikia uamuzi kwamba waadilifu na wenye hekima na yale wanayoyafanya yako mikononi mwa Mungu, lakini hakuna mtu ajuaye kama anangojewa na upendo au chuki. 9:2 Ay 9:22; Mhu 2:14; 6:6Wote wanayo hatima inayofanana, mwadilifu na mwovu, mwema na mbaya, aliye safi na aliye najisi, wale wanaotoa dhabihu na wale wasiotoa.

Kama ilivyo kwa mtu mwema,

ndivyo ilivyo kwa mtu mwenye dhambi;

kama ilivyo kwa wale wanaoapa,

ndivyo ilivyo kwa wale wasioapa.

9:3 Mhu 2:14; Yer 11:8; 17:9; Ay 21:26; 9:22; Yer 13:10; 16:12Huu ni ubaya ulio katika kila kitu kinachotendeka chini ya jua: Mwisho unaofanana huwapata wote. Zaidi ya hayo, mioyo ya watu, imejaa ubaya na kuna wazimu mioyoni mwao wangali hai, hatimaye huungana na waliokufa. Yeyote aliye miongoni mwa walio hai analo tumaini, hata mbwa hai ni bora kuliko simba aliyekufa!

9:5 Ay 14:21; Mhu 2:16; Za 9:6; Isa 26:14; 63:16Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa,

lakini wafu hawajui chochote,

hawana tuzo zaidi,

hata kumbukumbu yao imesahaulika.

9:6 Ay 21:21Upendo wao, chuki yao na wivu wao

vimetoweka tangu kitambo,

kamwe hawatakuwa tena na sehemu

katika lolote linalotendeka chini ya jua.

9:7 Mhu 2:24; 8:15; Hes 6:20Nenda, kula chakula chako kwa furaha, unywe divai yako kwa moyo wa shangwe, kwa maana sasa Mungu anakubali unachofanya. 9:8 Za 23:5; Ufu 3:4Daima uvae nguo nyeupe na daima upake kichwa chako mafuta. 9:9 Mit 5:18; Ay 31:2Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua. 9:10 Isa 38:18; 1Sam 10:7; Rum 12:11; Za 6:5; Mhu 2:24; 11:6; Hes 16:33Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima.

9:11 Amo 2:14-15; Yer 9:23; Kum 8:18; Ay 32:13; Isa 47:10; Mhu 2:14Nimeona kitu kingine tena chini ya jua:

Si wenye mbio washindao mashindano

au wenye nguvu washindao vita,

wala si wenye hekima wapatao chakula

au wenye akili nyingi wapatao mali,

wala wenye elimu wapatao upendeleo,

lakini fursa huwapata wote.

9:12 Mit 29:6; Za 73:22; Mhu 8:7; 2:14Zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ajuaye wakati saa yake itakapokuja:

Kama vile samaki wavuliwavyo katika wavu mkatili,

au ndege wanaswavyo kwenye mtego,

vivyo hivyo wanadamu hunaswa na nyakati mbaya

zinazowaangukia bila kutazamia.

Read More of Mhubiri 9